Jumanne, 07 Shawwal 1445 | 2024/04/16
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Tahnia za Mwanachuoni Mkubwa Ata Bin Khalil Abu Rashtah, Kwa Wanaozuru Kurasa Zake wakati huu adhimu wa Idd ul-Fitr yenye Baraka ya Mwaka wa 1439 H Sawia na Mwaka wa 2018 M
(Imetafsiriwa)

Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu na rehma na amani zimshukie Mtume wa Mwenyezi Mungu, na jamaa zake na maswahaba zake na wale wanaomfuata,


Kwa Ummah wa Kiislamu ambao Mwenyezi Mungu ameukirimu na kuutaja:
 

﴾كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّه﴿ِ

“Nyinyi ni Ummah bora muliotolewa kwa ajili ya watu. Munaamrishana mema na munakatazana mabaya na munamuamini Mwenyezi Mungu” [Al-i-Imran: 110]


Kwa wabebaji ulinganizi wema na wenye ikhlasi na wala hatumtakasi yeyote kwa Mwenyezi Mungu, wanaolingania kwa Mwenyezi Mungu na kufanya matendo mema:


 ﴾وَمَنْ أَحْسَنُ قَوْلًا مِمَّنْ دَعَا إِلَى اللَّهِ وَعَمِلَ صَالِحًا وَقَالَ إِنَّنِي مِنَ الْمُسْلِمِين﴿

“Na ni nani mwenye kauli njema zaidi kuliko yule alinganiaye kwa Mwenyezi Mungu na kufanya amali njema na akasema, ‘mimi ni miongoni mwa Waislamu” [Fussilat: 33]

Kwa waheshimiwa wanaozuru mitandao wanaoingia katika kurasa kwa haki na ikhlasi, wakitafuta kheri ndani yazo, Mwenyezi Mungu awalipeni kheri.


Nawapa tahnia nyote katika sikukuu hii yenye Baraka ya Idd ul-Fitr, na namuomba Mwenyezi Mungu (swt) azikubali saumu zenu, na awajaaliye miongoni mwa wale watakaookolewa na Moto wa Jahannam katika mwezi huu mtukufu. Pia namuomba Mwenyezi Mungu (swt) kwamba Idd hii iwe ndio mwanzo wa kheri na Baraka kwa Waislamu, na kwamba katika Idd ijayo tuwe chini ya kivuli cha Khilafah Rashida, bendera ya Raya ya La Ilaha Ila Mwenyezi Mungu Muhammad Rasool Mwenyezi Mungu, na jambo hili ni rahisi kwa Mwenyezi Mungu kulitimiza.


Mwisho, natuma salamu na dua zangu kwenu nyinyi kupata kheri hii, na Mwenyezi Mungu azikubali ibada zetu tiifu, na Mwenyezi Mungu awahifadhi na kuwalinda kutokana na kila uovu.


 ﴾فَاللَّهُ خَيْرٌ حَافِظًا وَهُوَ أَرْحَمُ الرَّاحِمِينَ﴿

“Na Mwenyezi Mungu ni mbora wa kuhifadhi na Yeye ni Mwingi wa kurehemu.” [Yusuf: 64]

Wassalaam Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakaatuhu


Usiku wa Idd ul-Fitr, 1 Shawwal 1439 H                                                                  Ndugu Yenu,
15/6/2018 M                                                                                                Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumatatu, 23 Disemba 2019 15:45

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu