Alhamisi, 09 Shawwal 1445 | 2024/04/18
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Wilayah Sudan: Ripoti ya Habari 17/04/2021

Kuendelea na amali za umma zilizofanywa na Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika mikoa na wilaya tofauti za nchi ili kuunda rai jumla ya umma ambayo inafahamu hukmu za Uislamu na suluhisho zake zinazohusiana na hali mbaya ambayo watu wanaishi ndani yake, ikiwakilisha utovu wa usalama na mapigano endelevu kati ya makabila tofauti tofauti, na kutoa wito wa kutekelezwa kwa usekula katika dola na jamii, na wanasiasa vibaraka, na wale waliopagawishwa na thaqafa ya Kimagharibi ...

Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan katika eneo la Kosti, katikati ya umati mkubwa wa watu, walitoa kalima ya kisiasa, kwa anwani: "Haki za Wanawake katika Uislamu," mnamo 19 Machi 2021.

Chini ya anwani: "Dori ya Vijana katika Mabadiliko Yanayohitajika," Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, eneo la Omdurman Magharibi, walitoa kalima ya kisiasa katika Msikiti wa Al-Rahma katika Soko la Libya, mnamo 23 Machi 2021.

Kalima nyingine ilifanyika kwa jina la, "Masharti ya Mipaka na Malipo, Khilafah, kuna usalama na usalama katika serikali na jamii," na Shabab ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, Omdurman katika kituo cha basi cha Grand Market, tarehe 23 Machi 2021.

Kalima nyingine ilitolewa kwa anwani, "Hukmu za Hudud na Kisasi, Khilafah, kuna patikana usalama na amani katika dola na jamii," na Mashababu wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Sudan, Omdurman katika kituo cha basi cha Soko Kubwa, tarehe 23 Machi 2021.

Pia katika mwezi wote wa Aprili, kalima nyingi na hotuba za kisiasa zilikuweko kote nchini Sudan ikileta ujumbe zaidi kwa umati juu ya hali nchini na haja ya kufanya kazi ya kusimamisha tena jamii ya Kiislamu kwa kufanya kazi ya kusimamisha Khilafah Rashida ya pili ambayo hutumia Shariah kama kipimo maalum kilichowekwa kusuluhisha mivutano ya kila siku ya umma na kuunganisha makabila kama taifa moja.

Mwakilishi kutoka Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Sudan

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu