Jumamosi, 11 Shawwal 1445 | 2024/04/20
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia: Mkutano wa Waandishi Habari

"Mradi huu Unaweza Kuitoa Tunisia kutokana na Mfumo wa Majanga"

Alhamisi, 2 Julai 2020, Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia ilifanya mkutano wa waandishi habari kwa anwani "Mradi huu Unaweza Kuitoa Tunisia kutokana na Mfumo wa Majanga" katika makao yake makuu yaliyoko katika makutano ya Sakra-Ariana katika mji mkuu.

Mkutano huu ulianza kwa Ustadh Khatib Karbaka kuzungumzia janga la utawala nchini Tunisia, ambapo alionyesha kwamba usimamizi wa kikoloni ndio msingi wa maafa yote na kwamba jambo hili limekwenda mbali zaidi ya watu na wala halikufungika kwao. Karbaka pia alitaja kuwa janga hili kina chake kinazidi kuongezeka kwa kuwepo mazingira ya kisiasa ambayo hayatafakari nje ya mipaka ya kifikra na kisiasa walio wekewa na Wamagharibi, na hawaoni mwanya wa kutokea ili kuiokoa nchi kiuchumi ila kupitia ukopaji zaidi kutoka kwa mgeni (IMF).

Kisha Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia, Dkt. Assad Al-Ajili, akatoa hotuba kuu ambayo alizungumzia kuhusu sura za ujanja wa watawala wakoloni, ima kupitia serikali ambayo raisi wake anasisitiza juu ya sera ya madeni, au katika bunge ambalo halioni fedheha yoyote katika kuidhinisha uundwaji wa tawi la nchi zinazo zungumza Kifaransa (Francophone). Nchini Tunisia, mama katika kiongozi wa dola alikuja kwa mmoja wa viongozi pindi alipo ukadiria ukoloni wa Kifaransa kuwa "ulinzi" na kulikadiria hili kuwa ni aibu katika historia ya Tunisia.

Dkt. Assad Al-Ajili alitoa wito wa kutabanniwa chaguo la Uislamu kama msingi wa mabadiliko na badali ya nidhamu zilizoko kwa sasa na kuutekeleza kivitendo na kuutabikisha ndani ya mradi ulio staarabika unao maliza mfumo wa majanga kupitia kusimamisha Dola ya Khilafah, apendapo Mwenyezi Mungu.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu