Wanawake na Watoto wa Kiislamu Wanakumbwa na Njaa Hadi Kufa Nchini Somalia huku Watawala wa Waislamu Wakiunga Mkono Ukandamizaji Ulimwenguni
- Imepeperushwa katika Habari na Maoni
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Mnamo tarehe 5 Oktoba 2022, BBC iliripoti kuwa Somalia inakabiliwa na baa la njaa inayotokana na ukame mbaya zaidi kuwahi kutokea katika kipindi cha miaka 40. Hadithi ya dada mmoja Muislamu inayofichuliwa na waandishi wa habari, ni ile ya Fatima Omar ambaye alimzika mtoto mmoja wa kiume kutokana na njaa na tayari alikuwa ameshamzika bintiye wa miaka 3 ambaye alifariki huku akitembea kwa siku 10 kutafuta msaada. Anawaambia waandishi wa habari kwamba hakuwa na nguvu za kumzika mtoto wake na alilazimika kuuacha mwili wake kando ya barabara huku akijua kuwa Fisi walikuwa wanakaribia kuingia ndani.