Alhamisi, 18 Ramadan 1445 | 2024/03/28
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

Habari na Maoni
Kenya Kusafirisha Mafuta: Faida kwa Kampuni za Kikoloni na Majonzi kwa Raia

Habari:

Rais Uhuru Kenyatta mnamo Jumatatu asubuhi, alizindua rasmi usafirishaji wa mapipa 200,000 ya kwanza kutoka Kenya. Kampuni ya Uchina iliyoko Uingereza ya ChemChina, iliyanunua mafuta hayo ya kundi la kwanza kwa kima cha bilioni Ksh1.2 (USD 12 million). Hii ikiwa ni sehemu ya Mpango wa Mapema wa Majaribio ya Utafutaji Mafuta (EOPS) ambayo ni hatua muhimu ya kuelekea katika kutekeleza mradi Kamili wa Maendeleo ya Lokichar Kusini (FFD). EOPS inaandaa barabara kwa ajili ya uchimbaji na maendeleo kamili ya mafuta nchini, ambayo uligunduliwa ndani ya Kaunti ya Turkana mnamo 2012 na Tullow Oil Kenya B.V na mshirika mwenzake Kampuni ya Africa Oil. Tullow ndiye kinara na anasaidiwa na washirika wake Africa Oil na Total, ambayo wamechukua asilimia 25 katika mradi huo. [The Star, 26/08/2019]

Maoni:

Katika kauli yake Uhuru alisema, "Ninajivunia kusema safari ya Kenya ya kuanza kusafirisha mafuta na gesi imeanza na uzinduzi huu wa mzigo huu unawakilisha mwanzo mpya sio tu kwa Kenya bali pia kwa eneo letu na mwanzo mpya wa ustawi wa Wakenya wote." Kwa kuongezea, alisema. "Tutahakikisha kuwa rasilimali asili za Kenya zinatumika katika hali ambayo itazalisha faida maradufu leo pasina kudhuru maslahi ya kizazi kijacho." Kauli hiyo ni kinyume na hali halisi inayoikumba Afrika kwani wakoloni Wamagharibi wanaitizama kama shamba lao la kikoloni ambalo wanaweza kujinyakulia rasilimali zake wakati wowote! Fauka ya hayo, mataifa ya Afrika ikijumuisha Kenya ni dola tiifu za kisekula za kirasilimali na sheria na sera zao zinapitishwa na mabwana zao wakoloni Wamagharibi kwa pazia ya wawekezaji wa kigeni ambao wanapora rasilimali za kitaifa kwa jina la ushirikiano wa kibiashara kupitia makampuni yao malafi!

Uchumi wa Kenya hivi sasa umo katika shida ya madeni, raia wanataabika kwa umasikini usioingia akilini na pengo kati ya matajiri na masikini linakuwa kwa kasi ya kushtusha mno! Licha ya kubarikiwa na rasilimali nyingi ikiwemo madini kama mafuta, gesi, titanium, ardhi kubwa ya kilimo na idadi kubwa ya watu miongoni mwa mengineyo. Ugunduzi wa mafuta na usafirishaji hakuidhamini Kenya kupata ukombozi wa kiuchumi; bali inatarajiwa kujiunga katika orodha ya nchi ndani ya Afrika zinazo zalisha na kusafirisha mafuta lakini zinadidimia katika umasikini kama vile Nigeria, Angola, Algeria, Libya, Misri n.k. Mfano mzuri, Nigeria imebarikiwa kuwa taifa la kwanza Afrika lenye kuzalisha na kusafirisha mafuta mengi miongoni mwa rasilimali nyingine. Lakusikitisha kwa mujibu wa Benki ya Dunia (WB), Nigeria ni moja kati ya nchi tano duniani ambazo zinachagia kuweko na watu milioni 368, ambayo ni nusu ya watu wanaoishi katika umasikini wa kupindukia duniani. Zaidi ya hayo, WB ilitangaza kuwa Nigeria itaipita India na kuwa nchi yenye idadi kubwa ya watu wanaoishi katika umasikini wa kupindukia! (theeastafrican.co.ke, 06/02/2019) Kinaya chake ni kwa mujibu wa ripoti ya hivi majuzi kutoka Wealth-X, nchi ambazo zinatarajiwa kuzalisha mamilionea wapya kwa kiwango cha juu ndani ya miaka mitano ijayo ndani ya Afrika ya kwanza ni Nigeria! (africabriefing.org, 22/01/2019) Mustakbali wa Kenya wa hivi sasa na katika siku zijazo ni sawa na ile ya Nigeria kwani wote wamebakia kuwa ni dola vibaraka wa kisekula wa kirasilimali wa Uingereza na watawala wao wapo kwa ajili ya kuwatumikia mabwana zao kwa unyenyekevu kwa kutekeleza sera na sheria zinazowapendelea wao!

Hivyo basi lau kwa uhakika Kenya inataka kuzitumia rasilimali zake na kupata faida maradufu kiukweli pasina na kudhuru maslahi ya kizazi kijacho. Ni lazima ikate mahusiano ya kikoloni na kufutilia mbali vibali ilivyotoa kwa kampuni za kikoloni ambazo zinapora rasilimali zake nyingi na kuwafurusha kutoka katika ardhi zao. Kwani ni kupitia mfumo wao muovu na batili wa kisekula wa kirasilimali na nidhamu zake zinazotamausha kama vile demokrasia, mujtama wa kihuria, uchumi wa riba miongoni mwa nyinginezo ndio chanzo cha kuganda kisiasa, kijamii, kiuchumi na kielimu ndani ya Kenya na duniani kwa ujumla. Kwa upande mwingine, tunawalingania wa Kenya wenye akili kukumbatia ulinganizi wa kurudisha tena maisha ya Kiislamu kupitia kusimamisha Khilafah kwa njia ya Utume. Khilafah ndio suluhisho pekee linalodhamini ukombozi wa kweli sio tu kwa Kenya bali duniani kote. Kwani itakwenda mbio kutekeleza Shari'ah (Qur'an na Sunnah) na kuachana na sheria zilizotungwa na wandamu. Hivyo basi, raia wake watatizamwa kwa mtizamo wa kibinadamu pasina kuzingatia dini na rangi zao na watafurahia utulivu, maendeleo na ustawi wa kweli kupitia usambazaji mwema wa rasilimali utakaosimamiwa na Khilafah kinyume na kuzunguka baina ya matajiri wachache kama inavyoshuhudiwa leo katika dunia hii inayoendeshwa kwa mujibu wa maslahi na manufaa!

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Ali Nassoro Ali
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Kenya

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 09 Agosti 2020 06:16

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu