Ijumaa, 19 Ramadan 1445 | 2024/03/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari 23/12/2020

Vichwa vya habari:

Ushindi wa Propaganda wa Urusi

Amerika Yashinikiza dhidi ya Kuwabandika Mahouthi Kibadiko cha Magaidi

Je, Indonesia Itafuata katika Kusawazisha Mahusiano Pamoja na Umbile la Kiyahudi

Maelezo:

Ushindi wa Propaganda wa Urusi

Amerika imeitambua operesheni moja ya ujasusi ya Urusi ambayo ilikuwa ikikusanya siri kutoka kwa kampuni za Amerika na utawala wa Amerika. Maafisa wa Amerika wamethibitisha kufanikiwa kwa operesheni hiyo ya Urusi, Amerika haijafichua kile kilicho patikana. Lakini shambulizi pana la kijasusi la Urusi kwa serikali ya Amerika na kampuni za kibinafsi ambazo zilikuwa zinaendelea tangu msimu wa masika na kugunduliwa wiki chache zilizopita, ni kati ya kasoro kubwa za kijasusi za nyakati hizi. Urusi ambayo haina uwezo wa kikawaida wa kupambana na msimamo wa kiulimwengu wa Amerika imegeukia njia zisizo za kawaida kudhoofisha, kufichua na kutatanisha mipango ya Amerika. Huku Urusi ikitambua hili litakuwa na athari ndogo kwa uwezo wa Amerika, liliipatia Urusi ushindi wa propaganda na ikaonyesha picha ya nguvu. Waamerika wengi wangali wanachukulia urais wa Trump ulitokana na udukuzi wa Urusi wa Chama cha Democrat na kuvuja kwa barua pepe. Kwa kuwa Urusi haina mfumo na haiko katika mapambano ya kimkakati ya kueneza na kuthamini haya ndiyo yote ambayo kihakika inaweza kuyafanya.

Amerika Yashinikiza dhidi ya Kuwabandika Mahouthi Kibadiko cha Magaidi

Shinikizo la utawala wa Trump la kuliita kundi la Houthi la Yemen linaloungwa mkono na Iran kama shirika la kigaidi "litaharibu sana" usalama wa kitaifa wa Amerika, wanadiplomasia wa zamani wa Amerika na maafisa wa Wizara ya Kigeni walifichua wiki hii. Katika barua kwa Waziri wa Kigeni Mike Pompeo aliyotumwa Jumapili, maafisa wakuu 20 wa zamani wakizingatia sera za Amerika katika Mashariki ya Kati waliutaka utawala "kuachana na mipango" ya kuwataja Mahouthi kuwa ni Shirika la Kigaidi la Kigeni. Waliibua wasiwasi kwamba hatua kama hiyo ingeonekana kuwa ya kisiasa na "kudhoofisha uaminifu wa mipango na sera za kukabiliana na ugaidi za Amerika." Utawala wa Trump unaripotiwa kupima jina la kikundi hicho cha kijeshi cha waasi kilichohusika katika vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka sita dhidi ya muungano unaoongozwa na Saudia. Hatua kama hiyo itakuwa sehemu ya kampeni ya "shinikizo kubwa" ya utawala juu ya Iran. Rais Trump alipiga kura ya turufu juu ya juhudi za Bunge la Congress mnamo Aprili 2019 kumaliza msaada wa Amerika kwa vita vya Saudia nchini Yemen. Mahouthi sasa ni sehemu ya utawala unaoondoka wa kuiaibisha na kuifanyia ugumu serikali ya rais mteule. Ukweli ni Amerika kwa muda mrefu iliwasaidia Mahouthi kuingia madarakani, lakini walishindwa kulazimisha mapenzi yao kwa nchi nzima baada ya kutawala mji mkuu Sana'a mnamo 2015. Kipote cha kisiasa nchini Yemen kiliundwa, wakisaidiwa na kuungwa mkono na Uingereza na hili limekuwa suala kubwa kwa mpango mkuu wa Amerika. Licha ya kudhoofisha muundo wa kisiasa ambao uliongozwa na Ali Abdullah Saleh na mshirika wake Abu Mansoor al-Hadi uwekezaji wa Amerika kwa Mahouthi haujatoa gawio.

Je, Indonesia Itafuata katika Kusawazisha Mahusiano Pamoja na Umbile la Kiyahudi

Huku mrundiko wa mataifa yakisawazisha mahusiano na umbile la Kizayuni, Amerika sasa inaning'iniza mabilioni kwa Indonesia ili kusawazisha mafungamano na umbile la Kizayuni. Hivi karibuni mkuu wa shirika la kifedha la Amerika alisema Amerika huenda ikaongeza maradufu uwekezaji wake wa dolari bilioni 1 ikiwa Indonesia itaanzisha mahusiano na Israel. Indonesia inaweza kufungua mabilioni ya dolari katika ufadhili wa ziada wa Amerika endapo itajiunga na msukumo wa Rais Donald Trump kwa nchi za Kiislamu kuanzisha mahusiano na 'Israel', kwa mujibu wa afisa mmoja wa Amerika.

Shirika la Maendeleo ya Kifedha ya Kimataifa la Amerika, wakala wa serikali unaowekeza ng'ambo, linaweza kuongeza zaidi ya mara mbili ya uwekezaji wake wa sasa wa $1 bilioni ikiwa Indonesia itaanzisha mafungamano na 'Israel', Afisa Mkuu Mtendaji wa DFC Adam Boehler alisema katika mahojiano Jumatatu katika Hoteli ya King David jijini Jerusalem. "Tunazungumza nao kuhusu hilo," Boehler alisema. "Ikiwa wako tayari, wako tayari na ikiwa wako tayari basi tutafurahi hata kusaidia zaidi kifedha kuliko kile tunachofanya sasa." Alisema hatashangaa ikiwa ufadhili wa shirika lake kwa Indonesia, taifa kubwa zaidi la Waislamu ulimwenguni, utaongezwa kwa "dolari bilioni moja au mbili zaidi."

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoAlhamisi, 24 Disemba 2020 14:28

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu