Ijumaa, 19 Ramadan 1445 | 2024/03/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vichwa vya Habari 21/07/2021

Vichwa vya Habari:

India Yafikia Mazungumzo na Taliban

Uingereza Yatuma Manuari Kuikabili China

Amerika, Washirika Waishutumu China kwa 'Shughuli Chafu' ya Udukuzi wa Mitandao

Maelezo:

India Yafikia Mazungumzo naTaliban

Kulingana na taarifa za vyombo vya habari serikali ya India inajiandaa kutengeza njia ya mawasiliano na Taliban ingawa kwa muda mrefu imekuwa ikiisaidia serikali iliyoongozwa na Rais Ashraf Ghani. Kwa miaka, New Delhi imeisaidia serikali ya Afghan kwa pesa, silaha na wataalamu, na kutoijali harakati ya Taliban na washirka wake. Hivi sasa India inajitahidi kuanzisha mazungumzo na Taliban, ikiwa ni juhudi mpya zinazoongozwa na Modi kurudisha ushawishi katika nchi iliyoharibiwa vibaya na vita. Taliban imekataa ombi hilo, Suhail Shaheen, msemaji wa kundi hilo alisema, “Tuna taarifa kutoka kwa makamanda wetu kwamba India inaupa  silaha upande wa pili. Inawezekena vipi kwamba wanahitaji kuzungumza na Taliban lakini kivitendo wanatoa silaha, ndege zisizo na rubani (droni), na kila kitu kwa Kabul? Hili linakinzana.” Lengo kuu la India nyuma ya hatua hizi ni kuhakikisha Afghanistan inabaki kuwa dola ya kisekula na kuzuia Uislamu usiichukue nchi hiyo.

Uingereza Yatuma Manuari Kuikabili China

Uingereza imetangaza mpango wa kupeleka manuari zake hadi Japan, zikisafiri kupitia katika Bahari ya Kusini ya China, kwa kile kinachoonekana nchi za Kimagharibi kujiingiza katika ukanda wa Pacifiki. Uingereza imetangaza kwamba baadaye mwaka huu itapeleka kwa njia ya kudumu manuari mbili katika habari zinazoizunguka Japan kabla ya HMS ‘Queen Elizabeth’- yenye kubeba ndege za mashambulizi kuwasili Japan. “ikifuatia baada ya kuzindua upelekaji wa chombo cha ubebaji ndege za mashambulizi, Uingereza itaziweka manuari zake mbili katika eneo hilo kwa njia ya kudumu baadaye mwaka huu“, Waziri wa Ulinzi wa Uingereza Ben Wallace alisema akiwa jijini Tokyo akifanya mkutano wa pamoja wa waandishi wa habari na mwenzake wa Japan, Nobuo Kishi. Japan ni mshirika wa kimkakati wa Uingereza na Amerika, ikishiriki katika mafunzo ya kijeshi ya pamoja na ikiwa mwenyeji wa mkusanyiko mkubwa wa vikosi vya Amerika nje ya majimbo yake 50. Manuari kubwa zaidi ya jeshi la wanamaji la Ufalme wa Uingereza, chombo cha ubebaji ndege za mashambulizi kwa jina ‘Malkia Elizabeth’, pamoja na mfumo wa mashambulizi wa Uingereza zinatarajiwa kuwasili Japan mnamo Septemba kwa ajili ya kushiriki katika mazoezi ya pamoja na majeshi ya ulinzi ya Tokyo. Hatua hii, iliyo wasilishwa na Kishi na Wallace, imeundwa kwa ajili ya kupambana na shughuli za kimipaka zinazofanywa na China katika eneo hilo.

Amerika, Washirika Waishutumu China kwa 'Shughuli Chafu' ya Udukuzi wa Mitandao

Amerika iliwaongoza washirika wake katika kuishutumu China juu ya shughuli "chafu" ya udukuzi wa mitandao, ikiituhumu China kwa ukusanyaji pesa kihalifu, utoaji wa matakwa ya ridhaa kwa kampuni za kibinafsi na kuhatarisha usalama wa taifa. Katika maoni ambayo yataongeza chachu katika uhusiano mbaya kati ya Washington na Beijing, afisa mmoja wa ngazi ya juu wa Amerika alisema kwamba China “tabia mbaya ya China ya udukuzi wa anga ya mitandao haiwiani na lengo lake lililoelezwa la kuonekana kama kiongozi muwajibikaji ulimwenguni.” Amerika, Muungano wa Ulaya, Uingereza, Australia, Canada, New Zealand, Japan na NATO waliungana dhidi ya tishio hilo, alisema afisa huyo wa Amerika, na watafichua namna ambavyo China inavyoilenga mitandao ya kimataifa. Pia Amerika itawatuhumu rasmi wadukuzi wa mitandaoni wenye uhusiano na Wizara ya Ulinzi ya China kwa kufanya udukuzi mkubwa katika server za ubadilishanaji za Microsoft mnamo Machi. Udukuzi huo, ambao ulipatiliza dosari zilizokuwa katika mfumo wa huduma za mabadilishano wa Microsoft, umeathiri kwa uchache mashirika 30,000 ya Amerika zikiwemo serikali za mitaa na ulikuwa tayari imepewa sifa ya "ujasiri usio wa kawaida" wa kampeni ya kijasusi ya China mitandaoni. Vita vya nani atakuwa kiongozi wa kiulimwengu vimepamba moto.

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu