Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Kushiriki katika Mazungumzo ya Amani Kunapelekea Kushirikiana na Adui Mbaya Zaidi wa Uislamu na Waislamu

(Imetafsiriwa)

Vita vya uharibifu vya miaka 18 vilivyoanzishwa na Amerika kwa kisingizio cha "Vita dhidi ya Ugaidi" vilivyozinduliwa dhidi ya Waislamu wa Afghanistan vimefikia kizingiti kikubwa. Haiwezekani kwa Amerika kuondoka kwa ghafla na kusalimu amri, kwa sababu kusalimu amri huko kutakuwa na matokeo sawa na yale ya uliokuwa Muungano wa Kisovieti, yaani, vita vya wenyewe kwa wenyewe vya miaka ya tisiini na athari zake zote.

Matokeo yake, baada ya nusu karne ya uhusiano wa kisiasa na Afghanistan, na mapambano katika maeneo ya kisiasa, uchumi na ujasusi, na kugharimu matumizi ya matrilioni ya dolari na kuwatoa kafara maelfu ya wanajeshi kwa ajili ya uvamizi wa Afghanistan kwa kipindi cha miaka 18 iliyopita, Amerika sasa imerudi kwenye mazungumzo ya amani na Taliban kwa kuhofia kushindwa kwa fedheha. Inavyoonekana, lengo la mazungumzo haya ya amani ni kumaliza vita nchini Afghanistan na wakati huo huo kuhakikisha ushawishi wa kikoloni wa Amerika, ili kulitumia kikamilifu eneo la mkakati wa kijografia, maliasili na uzalishaji pesa kutokana na mihadarati.

Inasemekana kuwa, ni jambo la kifahari kwa kundi la Kiislamu lenye silaha kwamba dola kuu inayoongoza duniani imelazimika kukaa mezani nalo kwa mazungumzo ya amani. Hii linajiri katika wakati ambapo kundi hili limetajwa kama la "kigaidi" na taasisi ya sera ya kigeni ya dola hii kuu inayoongoza duniani, ambayo ilitangaza vita kwa kisingizio hicho cha uhadaifu ... Lakini, ikiwa mazungumzo hayo yatapelekea kung'olewa kwa ushawishi wa Amerika kutoka Afghanistan kijeshi, kisiasa na kiuchumi, haiwezekani katika sera ya Amerika isipokuwa ililazimishwa juu yake.

Kujiunga na Mchakato wa Amani wa Amerika kwa vikundi vya kisiasa na vya kijeshi vya Afghanistan hakika kutasababisha kujisalimisha pole pole na kusalimu amri kwa maadui wavamizi wa nchi hii, kusambaratika zaidi na kugawanyika kwa Taliban na kuwahadaa Waislamu wa Afghanistan.

Hakuna shaka kwamba hamu ya kweli na hitaji la Uislamu na Waislamu wa Afghanistan ni kuondolewa kikamilifu kwa vikosi vyote vamizi kutoka nchini, kuondoa nidhamu ya kidemokrasia na utekelezaji kamili wa Sharia. Lengo hili halifuatiliwi tu na Waislamu wa Afghanistan pekee. Badala yake Ulimwengu mzima wa Kiislamu unataka kuondolewa mara moja kwa mifumo na serikali vibaraka, kuziacha huru ardhi zilizokaliwa, kuondolewa kwa kila athari ya vikosi vya uvamizi kutoka kwa ardhi zao na utekelezaji wa Sharia kupitia kusimamisha tena kwa Khilafah. Vikundi vyenye silaha katika nchi zilizokaliwa na Mapinduzi ya Kiarabu ni dhihirisho la wazi zaidi la matakwa na azma ya Umma ya uhuru. Lakini swali ni, je! Lengo hili linaweza kufikiwa kupitia mazungumzo na vikosi vya uvamizi?

Hapana kabisa. Ikiwa hii ingewezekana, Harakati ya Kiislamu ya Tajikistan ingefanikisha lengo hili kupitia kuweka amani na serikali kibaraka na ya kidikteta ya nchi hiyo. Vikosi vya mapinduzi na ukombozi vya Syria vingefikia lengo hili kwa kujadiliana na vikosi vya Urusi, Irani na Uturuki. Waislamu wa Chechen, au hata Hizbi Islami ya Gulbuddin Hekmatyar nchini Afghanistan wangeweza kufikia lengo hili. Vikundi hivi vilijiunga katika michakato ya kidemokrasia ya kikafiri, na baadaye mipango ya kikoloni iliwayeyusha na malengo yao. Matokeo yake, mafanikio yao pekee yalikuwa ni kutamaushwa zaidi na kuzipa nguvu nidhamu za kikafiri juu ya Umma wa Kiislamu. Je! Harakati ya Taliban inataka kufuata mfano huu wa vikundi hivi?

Pia, katika historia yake yote, Amerika ni maarufu mno kwa kuvunja ahadi zake, sio tu na vikundi vyenye silaha na vya kisiasa lakini pia na dola. Ikiwa ukweli huu ni mgumu kuukubali, waulizeni viongozi wa Muungano wa zamani wa Kaskazini na kiongozi wa Hizb-e Islami nchini Afghanistan, waulizeni viongozi wa Iran na Korea Kaskazini. Na waulizeni viongozi wa Uingereza walichokifanya katika BREXIT. Sera ya Kivitendo ya Amerika haina marafiki wa kudumu, wala haina maadui wa kudumu. Kwa Amerika, maslahi yake ya kikoloni yanahalalisha mbinu zake chafu. Ili kuikalia Afghanistan, Amerika kwanza iliwangazeni kama magaidi na ikaangusha serikali yenu. Sasa baada ya miaka mingi ya vita na uharibifu, na kwa sababu ya mahitaji ya dhurufu zilizobadilika katika sera ya kigeni ya Amerika, imeondoa majina yenu kutoka kwa Orodha ya Magaidi ya UN 1267, ambayo sasa inakuiteni kama uasi wa kindani. Kwa hivyo, Amerika imefungua milango ya mazungumzo nanyi ili kudhamini usalama na mwendelezo wa uwepo wake wa kikoloni.

Uhalisia wa vita nchini Afghanistan kabla ya 2014 ulikuwa kwamba watu wa Afghanistan walikuwa wakipambana moja kwa moja na vikosi vya kigeni na washirika wao. Lakini, baada ya kutia saini Makubaliano ya aibu ya Usalama wa Nchi Mbili (BSA), vita vilihamia kwa umwagaji damu kati ya watu wa Afghanistan na kusababisha kuvifanya vita vya Amerika viwe vya wenyewe kwa wenyewe. Tangu wakati huo, wavamizi wamepumzika kwa amani katika kambi zao, wakivipeleka vita kuwa baina ya watu wa Afghanistan kama washauri, wakufunzi na wafuasi, na kwa kuyahami na kuyafadhili majeshi ya Afghanistan. Kwa hivyo, wanacheza dori mbaya huku wakiweka amani na usalama wao. Vikundi vya wapiganaji vya kiajabu pia vimeibuka ambavyo hufanya vitendo vibaya katika vita. Wakati mwingine vita hivi hugeuka kuwa Fitna kamili (kesi na mateso) baina ya Waislamu kwa misingi ya kikabila na kimbari, na wakati mwingine hubadilika kuwa vita vya kudhibiti mikondo ya biashara ya dawa za kulevya, na ilhali wakati mwingine, maumbile yake hubadilika na kuwa ya vita vya wakala wa nchi ambazo zina maslahi nchini Afghanistan na katika eneo hilo.

Kwa kweli, watu wa Afghanistan wanabeba gharama halisi ya vita hivi. Hali hii inatia mashaka juu ya umbile halisi la mapambano ya watu wenye ikhlasi, na Wakoloni hupatiliza fursa kamili ya hilo.

Enyi Wanachama Wenye Ikhlasi wa Mapambano nchini Afghanistan!

Kukaribia shubiri moja karibu na uvamizi wa makafiri ni kwenda mbali zaidi na ukweli. Ikiwa mtafungua milango ya mazungumzo na wanajeshi na kuendelea na mwelekeo huu, itapelekea kupotoka kwenu polepole. Mweleko huu hatimaye utakuunganisheni katika mchakato wa Amerika. Hili litakuja wakati ambao hamna habari ya kupotoka kwenu na hamko tayari hata kukubali. Matokeo yake, hata kama makafiri watamaliza uvamizi wao wa moja kwa moja, wataendelea na sera zao za kikoloni kupitia taasisi za kimataifa, balozi, wanadiplomasia, majasusi na taasisi za kiraia n.k. katika hali hiyo, onyo kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) ambalo lilipewa watu wa pango litafaa hali yetu vilevile.

﴿إِنَّهُمْ إِن يَظْهَرُوا عَلَيْكُمْ يَرْجُمُوكُمْ أَوْ يُعِيدُوكُمْ فِي مِلَّتِهِمْ وَلَن تُفْلِحُوا إِذًا أَبَدًا

“Kwani wao wakikutambueni watakupigeni mawe, au watakurudisheni katika dini yao; na hapo hamtafanikiwa kabisa!”[18:20]

Hakuna shaka kwamba ikiwa mapambano ya moja kwa moja ya kisilaha dhidi ya wavamizi nchini Afghanistan yatakoma, makafiri watatudhalilisha hata zaidi na watatulazimisha kukubali sheria zao za fisadi na duni mno. Matokeo yake, tutakuwa tumejiletea ya ulimwengu huu na Akhera kwa kuacha mapambano yenu dhidi ya uvamizi, kwa kupuuza mapambano ya kifikra na kisiasa dhidi yao na kazi ya kutekeleza Uislamu kupitia kusimamisha Khilafah.

Enyi Watu wa Afghanistan!

Mchakato wa amani na adui hautakuleteeni kiwango cha usalama na maendeleo mnayotaka. Badala yake, mchakato huu utafanya tu hali ya vita na siasa nchini Afghanistan kuwa ngumu zaidi, na vikosi vamizi vitazidi kuimarisha mizizi yake ya kijeshi, kisiasa, kiuchumi na kithaqafa. Baada ya kuachana na mapambano dhidi ya wavamizi, Waislamu wa Afghanistan hawataweza kuwanasihi au kuwalinda wake zao na watot wao, na kila udhalilishaji utamuangukia kila Muislamu wa nchi hii. Nchini Afghanistan - kama vile nchi zingine za Kiislamu - haitawezekana kwa watu kuwapa watoto wao malezi ya Kiislamu, kuanzisha familia kupitia mchakato wa Kisheria wa Nikah (harusi), kuswali, kutoa hotuba za kisias Misikitini na kutekeleza mapambano ya Kisiasa ya Kiislamu katika jamii.

Enyi Waislamu, Enyi Watoto wenye Ikhalsi wa Umma huu!

Amerika inataka kutangaza mwisho wa vita vyake vya muda mrefu katika historia ili chama tawala cha Amerika kiitumie kushinda uchaguzi wa bunge. Kwa upande mwingine, inataka kuzihadaa nchi za eneo hili kwa kujifanya kumaliza vita nchini Afghanistan. Kwa kweli, Amerika inataka kuzuia kushindwa kwake kwa aibu na wazi katika kaburi hili la himaya. Cha kushangaza, katika mchakato huu wa amani, amani sio ajenda kwa vikundi vyengine ishirini vya kigaidi ambavyo majina yao yanatajwa mara kwa mara na wanasiasa wa Amerika na viongozi wao wa vibaraka waliopandikizwa jijini Kabul. Kwa hivyo, inatarajiwa kwamba Afghanistan itabaki kuwa mradi wa vita wa Amerika katika eneo hili. Baada ya ukamilikaji wa mchakato huu mbaya na uhadaifu, jiografia ya vita pekee ndio itakayobadilika; na Amerika itaendelea na utumiaji wa eneo la mkakati wa kijografia la Afghanistan, maliasili na biashara ya dawa za kulevya.

Instahiki kutaja kuwa ushirikiano na uwezeshaji uliopanuliwa na Pakistan, Saudi Arabia, Imarati na Qatar katika mchakato huu haimaanishi kwamba wanaihurumia Taliban au kwamba ni wakweli kwa kundi hili. Badala yake, dola hizi ni njia rahisi za Amerika kuishawishi Taliban. Vilevile, ushirikiano kutoka China, Urusi, India na Iran na pande zinazopigana (Taliban na Amerika) huzidisha hali hiyo kuwa ngumu, na huafikiana na uhalisia wa vipimo vya kikanda vya vita na ukweli kwamba pia kuna vita vya mawakala vinavyoendelea nchini, na kwamba Amerika inataka kuhamisha mzigo wa vita mabegani mwa nchi zingine. Mnamo 2001, Pakistan ilifanya makubaliano na Amerika juu ya kuanguka kwa serikali ya Taliban na kuikalia Afghanistan. Sasa kwa mara nyengine tena, Pakistan inaandaa mazingira ya kurudia njama hiyo na makubaliano hayo. Hivyo basi, Amerika inatumia ala zake zote za kimkakati kutia shinikizo kwa Taliban na kuwashawishi kujisalimisha kwa mchakato wa amani wa Amerika.

Enyi watu wenye ikhlasi wa Ummah ndani ya Harakati ya Taliban na makundi mengine ya Kiislamu!

Malengo ya mapambano na kafara ya mababu zenu dhidi ya Uingereza, na malengo yenu na kafara dhidi ya Muungano wa Kisovieti na dhidi ya Amerika hayakuwa na sio ya kuimarisha mizizi ya nidhamu ya Kidemokrasia na sheria zilizotungwa na wanadamu. Badala yake, kafara hizi zimetolewa kwa ajili kusimamisha Dola ya Kiislamu na utekelezaji wa Sharia. Hivyo basi, sote na tuseme HAPANA kwa sauti moja kwa mchakato wa amani wa Amerika na kwa mipango mengine yote ya makafiri na vibaraka wao- kwa maneno, na kwa vitendo. Hebu na tuyapongeze majeshi na mapambano ya kisilaha dhidi ya makafiri kwa fikra pana na ya kisiasa ya Hizb ut Tahrir, chama kinachoweza kukuongozeni hatua kwa hatua kupitia njama na mikakati ya maadui wetu. Hebu na tufanye kazi kufikia matunda ya kafara za ndugu zetu katika eneo hili kwa kusimamisha tena Khilafah Rashida. Hapo tu ndipo tutakapoweza kusherehekea na kufurahiya nchini Afghanistan na katika nchi zote za Kiislamu ladha ya kweli ya ustawi na usalama unaotokana na ujasiri wa Iman chini ya thaqafa ya kisiasa ya Dola la Kiislamu. Hapo tu ndipo tutakapoweza kufanya kazi kupitia taasisi ya sera ya kigeni ya Dola ya Kiislamu ili kueneza Uislamu ulimwenguni. Hapo tu ndipo Umma wa Kiislamu itakapoweza kuchukua hatua mbali na makafiri na kuwatoa wanadamu kutoka katika giza la mfumo wa Kirasilimali hadi kwenye nuru ya Uislamu na mfumo wa Kiislamu. Basi,

﴿لِمِثْلِ هَٰذَا فَلْيَعْمَلِ الْعَامِلُونَ

“Kwa mfano wa haya nawatende watendao.” [37:61]

﴿وَمَا ذَٰلِكَ عَلَى اللَّهِ بِعَزِيزٍ

“Na hilo kwa Mwenyezi Mungu si jambo gumu.” [14:20] 

H. 1 Jumada II 1440
M. : Jumatano, 06 Februari 2019

Hizb-ut-Tahrir
Wilayah Afghanistan

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.