Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  29 Sha'aban 1441 Na: 021 / 1441 H
M.  Jumatano, 22 Aprili 2020

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Tangazo la Matokeo ya Mwandamo wa Mwezi wa Ramadhan 1441H

(Imetafsiriwa)

شَهْرُ رَمَضَانَ الَّذِيَ أُنزِلَ فِيهِ الْقُرْآنُ هُدًى لِّلنَّاسِ وَبَيِّنَاتٍ مِّنَ الْهُدَى وَالْفُرْقَانِ فَمَن شَهِدَ مِنكُمُ الشَّهْرَ فَلْيَصُمْهُ وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَى سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ يُرِيدُ اللّهُ بِكُمُ الْيُسْرَ وَلاَ يُرِيدُ بِكُمُ الْعُسْرَ وَلِتُكْمِلُواْ الْعِدَّةَ وَلِتُكَبِّرُواْ اللّهَ عَلَى مَا هَدَاكُمْ وَلَعَلَّكُمْ تَشْكُرُونَ﴿

“Mwezi wa Ramadhani ambao imeteremshwa humo Qur'ani kuwa ni uwongofu kwa watu, na hoja zilizo wazi za uwongofu na upambanuzi. Basi ataye kuwa mjini katika mwezi huu naafunge. Na mwenye kuwa mgonjwa au safarini, basi atimize hisabu katika siku nyengine. Mwenyezi Mungu anakutakieni yaliyo mepesi wala hakutakieni yaliyo mazito, na mtimize hiyo hisabu, na mumtukuze Mwenyezi Mungu kwa kuwa amekuongoeni ili mpate kushukuru.” [Al-Baqara: 185]

Kwa jina la Mwenyezi Mungu Mwingi wa rehma Mwenye kurehemu; Sifa njema zote ni za Mwenyezi Mungu Mola wa walimwengu, Mshindi wa majabari, Mola wa Kiti Kitukufu cha Enzi ('Arsh), Mjuzi kwa waja wake na mpole kwa waumini. 

Rehma na amani zimshukie Mtume wa mwisho kutumilizwa kwa wanadamu, bwana wa wanadamu wote, aliyeteremshiwa Kitabu kwa wahyi, mmiliki wa seerah nzuri ya kunukia, na imam wa Maswahaba wema, ni kiongozi wa Ummah bora ulio tolewa kwa watu; bwana wetu Muhammad, na amani iwashukie jamaa zake na Maswahaba zake.

Amepokea Bukhari katika Sahih yake kutoka kwa Muhammad Bin Ziyad aliye sema: "Nimemsikia Abu Hurayrah radhi za Mwenyezi Mungu ziwe pamoja naye akisema: "Mtume (saw) amesema au Abu al-Qaasim (saw) amesema":

«صُومُوا لِرُؤْيَتِهِ وَأَفْطِرُوا لِرُؤْيَتِهِ فَإِنْ غُبِّيَ عَلَيْكُمْ فَأَكْمِلُوا عِدَّةَ شَعْبَانَ ثَلَاثينَ».

"Fungeni kwa kuonekana mwezi na fungueni kwa kuonekana mwezi. Na ikiwa utafichika kwenu kuuona kutokana na kutanda kwa mawingu basi kamilisheni siku thalathini za Sha'aban."

Na baada ya uchunguzi wa mwandamo wa mwezi wa Ramadhan ulio barikiwa katika usiku huu; usiku wa kuamkia Alhamisi, kwa hakika haukuthubutu kuonekana, muonekano wa kisheria, na hivyo basi kesho Alhamisi, ndio itakamilisha Sha'aban, na kesho kutwa, Ijumaa ndio itakuwa siku ya kwanza ya mwezi wa Ramadhan ulio barikiwa wa mwaka huu wa 1441 H.

Na kwa munasaba huu ni furaha yangu kufikisha pongezi zangu na pongezi za Raisi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na wafanyikazi wake wote kwa Amiri wa Hizb ut Tahrir, mwanachuoni mkubwa Ata Bin Khalil Abu Rashtah, na kwa Waislamu wote kwa mwezi huu mtukufu, tukimuomba Mwenyezi Mungu (swt) atujaaliye miongoni mwa watakao achwa huru na Moto katika mwezi wa msamaha na kheri nyingi.

Enyi Waislamu:

Hakika mwezi wa saumu umefika na ulimwengu umeingia katika kitovu cha janga la kuendelea linalo pasua majumba yake.  Shida hii imekuwa ni funzo kubwa kuhusu maisha ya dunia, na thibitisho lenye gharama la kudhoofika kwa mwanadamu, ni ukumbusho mkali kuwa wale wanao wanyanyasa watu wa ulimwengu huu wao si wenye kumshinda Mwenyezi Mungu. Asema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

لَا تَحْسَبَنَّ الَّذِينَ كَفَرُوا مُعْجِزِينَ فِي الأَرْضِ وَمَأْوَاهُمُ النَّارُ وَلَبِئْسَ الْمَصِيرُ﴿

Msiwadhanie walio kufuru kwamba watashinda katika nchi. Na makaazi yao ni Motoni, na hakika ni maovu kweli marejeo yao.” [An-Nur: 57] 

Janga hili limekuja huku ulimwengu ukiongozwa na nyoka wanao fuatwa na watawala wajinga (Ruwaibidha); na tiba haiko katika kuwaiga nyoka hawa, wala hakuna uzuri katika kuwaiga watawala wajinga (Ruwaibidha)! Sisi hapa tunaziona dola zikitaataa kulia na kushoto, hali zake ni kama hali ya yule anaye taataa kutokana na kuunguzwa na kaa la moto, hajui ni upande upi ulio na uchungu mdogo kwake, wala hajui ni chaguo lipi lenye madhara hafifu kwake! Na licha ya kuwa janga hili huenda likawa limetoka katika nchi na sehemu maalumu na kwa njia maalumu, na licha ya kuwa kusambaa kwake kumenakiliwa katika kamera za habari; na licha ya kuwa ukali wake huenda ukawa umeshuhudiwa na wagonjwa; na licha ya kuwa wito wa tahadhari yake huenda ukawa umethibitishwa na picha za makaburi mengi… Lakini lau wangeisoma Hadith ya Mtume (saw) kuhusu Tauni, wangejua jinsi gani nzuri ya kukabiliana na majanga, na hawange wafungiwa watu wao majumbani mwao, lakini Mwenyezi Mungu ameshapitisha Qadhaa yake kwao na kufichua kufeli na udhaifu wao.    

Hakika Wamagharibi wamefeli kwa sababu utandawazi walio uunda umekuwa mkubwa zaidi kuweza kuukomesha pale wanapotaka. Na hakika Wamagharibi wamefelii kwa sababu mali, na rasilimali, na wafanyikazi wamekuwa ndio dini yao na chimbuko la shajiisho lao. Na hakika wamefeli Wamagharibi kwa sababu wao walidanganyika na elimu zao na kudhani kuwa wamezijaalia kuwa mungu pasi na Mwenyezi Mungu!! Ndio, mabwana wa Wamagharibi, wanafalsafa, na wafuasi wao walidhani kuwa kwa werevu wao hawamuhitaji Mwenyezi Mungu na sheria yake, hivyo basi wakajitungia sheria yao wenyewe na wakavua kutokana nayo nidhamu na kuitengezea siasa, na hivyo basi wakajijengea nyumba kwa utandu wa buibui! Asema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

مَثَلُ الَّذِينَ اتَّخَذُوا مِن دُونِ اللَّهِ أَوْلِيَاء كَمَثَلِ الْعَنكَبُوتِ اتَّخَذَتْ بَيْتاً وَإِنَّ أَوْهَنَ الْبُيُوتِ لَبَيْتُ الْعَنكَبُوتِ لَوْ كَانُوا يَعْلَمُونَ﴿

Mfano wa walio wafanya walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, ni mfano wa buibui alivyo jitandia nyumba. Na hakika nyumba dhaifu mno kuliko zote ni jumba la buibui, laiti kuwa wanajua.” [Al-Ankabut: 41].

Enyi Waislamu: Enyi Ummah Bora muliotolewa kwa Watu

Hakika mapinduzi ya Kiarabu yalikuwa ni dalili kwamba Ummah wa Kiislamu ndani yake una nguvu za kutosha na matakwa mazuri ya kumaliza ushawishi wa Wamagharibi na vibaraka wao. Ama janga hili limekuhakikishieni kwamba adui wenu ni dhaifu katika jengo, na dhaifu katika nidhamu, na kwamba watu wake wamechoshwa na uhadaifu, ulafi na usimamizi wake mbaya, na wana hamu kubwa ya uongozi mpya wa kiulimwengu. Kwa sababu hii basi, mwezi huu ulio barikiwa na uwe ndio mwezi wa kukusanya pamoja nishati zenu, ndio mwezi wa kuamsha ari yenu, na kisha kufanya kazi ya kuziokoa nafsi zenu kwa kuregelea njia (manhaj) ya Utume katika ulimwengu huu, na hilo haliwezekani ila kwa kukazanisha azma ya kurudisha Khilafah kwa njia ya Utume, na kisha kuupa ulimwengu huu ulio dhulumiwa matumaini katika maisha matukufu yanayo stahiki wanadamu.

Ewe Bwana Mwenye kuabudiwa kwa haki, Mmiliki wa ufalme, ewe ambaye mikononi mwake ipo amri ya kila kitu, tuharakishie muungano wa Ummah wa Kiislamu ndani dola ya Kiislamu, hakika Wewe ni Mwenye kusikia dua.

Muwe na mwezi wa baraka, Wasalaamu Alaikum Wa Rahmatullah Wa Barakatuhu

Usiku wa kuamkia Alhamisi ndio wenye kukamilisha mwezi wa Sha'aban ya mwaka 1441 H.

Mhandisi Salah Eddine Adada

Mkurugenzi wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.