Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Kenya

H.  6 Safar 1442 Na: 1442/02 H
M.  Jumatano, 23 Septemba 2020

Taarifa kwa vyombo vya habari

Ni Khilafah Pekee kwa Mfumo wa Utume Ndio Itakayositisha Ubabe wa Marekani na Kuikomboa Falastin

Utawala wa Marekani umeitaka Kenya kuunga mkono maslahi ya kisiasa na kibiashara ya taifa la ‘Israel’ la sivyo iachane kabisa na mkataba wa kibiashara huria (Free Trade Deal- FTA) iliosaini na taifa hilo kubwa la kiuchumi duniani. Washington imeitaka Kenya kuwa ili kuimarisha ushirikiano wa Kibiashara itapaswa kutounga mkono vitendo vitakavyohujumu biashara katika Marekani na utawala wa Kizayuni.

Matamshi haya ya Amerika kwa Kenya, hayaoneshi tu ubeberu na ubabe wa sera yake ya kigeni bali pia yanaashiria kuwa Marekani ndio inayounga mkono na kudhamini jinai kubwa dhidi ya Waislamu wa ardhi tukufu ya Filastin. Siasa ya nje ya Marekani imejikita katika kuyaingilia mataifa mengine duniani na kuendesha sera zake za kigeni. Kiuhakika kwa kuwa Kenya kama nchi yoyote ile barani Afrika bado ingali chini ya minyororo ya ukoloni mambo leo hivyo katu haitoweza kuhimili kwa nguvu shinikizo la siasa la Kimarekani dhidi yake. Na ni kwa muktadha huu, Kenya tayari imekuwa ikitambua uwepo wa umbo la Kiyahudi na kuunga mkono suluhisho la serikali mbili kwa Filastin na utawala wa Kizayuni.

Ombi hili la kibabe linakuja siku chache tu baada ya mataifa ya Muungano wa falme za Kiarabu na Bahrain kutia saini na utawala haramu wa Kiyahudi kwenye makubaliano ya khiyana kubwa dhidi ya ardhi ya Filastin huko Washington. Ni wazi kwamba Marekani ndio inayoendesha mipango na sera zote za kusimamisha serikali ya kujitawala ya Palestina pamoja na kuifanya Al-Quds ni miliki ya watu wa mataifa yote kuigawanya baina ya Waislamu na Mayahudi.  Amerika aidha, ni mwekaji wa mikakati yote juu ya kadhia ya Filastin na kwamba anafanya kila awezavyo ili Waislamu wapate kudhurika.

Tunasema umbo la Kiyahudi liko ndani ya nchi ya Kiislamu na bila ya ardhi hii umbo hili haliwezi kuweko au pia kuendelea na ukaaji wake wa kimabavu. Utawala huu haramu umenyakua ardhi ya Filastin ambayo ndani yake kuna Msikiti Mtukufu wa Al-Aqsa; kibla cha kwanza kwa Waislamu na Msikiti mtukufu wa tatu. Hivyo basi, kujenga   mahusiano yote ya kimataifa au maslahi ya kibiashara na kuhalalisha uwepo wake ni kitendo cha haramu kinachokataliwa na Dini yetu.

Kadhia ya Filastin ni kadhia ya Kiislamu hivyo tunakataa katakata suluhisho lolote lile la kimagharibi lisilokuwa la Kiiislamu. Kwa kutilia maanani uhalisia huu, ndio tunafanya kazi pasina kuchoka ya kurudisha sheria za Kiislamu katika mataifa ya Kiislamu chini ya utawala muongofu wa Khilafah kupitia kwa mfumo wa utume. Kwa yakini, ni Khilafah pekee ndio itakayoweza kuunganisha wanajeshi wa Kiislamu kuweza kulinda Waislamu wa Filastin na biladi zote za Kiislamu.

Shabani Mwalimu

Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari Hizb ut -Tahrir Kenya

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kenya
Address & Website
Tel:  +254 707458907
E-Mail: mediarep@hizb.or.ke

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.