Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  30 Rabi' I 1441 Na: HTY- 1441 / 12
M.  Jumatano, 27 Novemba 2019

Taarifa Kwa Vyombo vya Habari

Lini Mtume wa Mwenyezi Mungu(saw) Alisimamisha Dola ya Kiraia?!

(Imetafsiriwa)

Mahmoud Al Junaid, Naibu Waziri Mkuu mpya aliyeteuliwa mnamo 05/11/2019 kwa ajili ya “Ruwaza ya Kitaifa ya Dola ya Kisasa ya Yemen” aliweka wazi kwa mara ya kwanza msamiati wa ‘dola ya kiraia’ pale aliposisitiza katika mkutano na Mawaziri wa Usafiri Zakaria al-Shami, Utawala wa mitaa Ali al-Qaisi, na huduma kwa raia Idris Al-Sharajbi, mnamo Jumanne 19/11/2019 kwamba “taasisi kujibu kwa haraka utekelezaji wa maagizo ya Rais wa Baraza Kuu la Kisiasa linaashiria umakinifu katika kupambana na ufisadi, kuboresha uwazi na kuendelea na ujenzi wa dola ya kiraia iliyo huru kutokamana na ufisadi na watu wafisadi,” Gazeti la Al-Thawra Daily nchini Yemen liliripoti mnamo Jumatano 20/11/2019.

Kwa takribani mwaka, Mahouthi wamekuwa wakitumia neno “dola ya kisasa,” kuwapa matumaini wafuasi wao kwamba njia ya Qur’an itasimamisha dola inayotawala kwa Uislamu. Wamenyamaza kimya kuhusiana na neno dola ya kiraia tangu kutolewa kwa kielelezo cha ruwaza mnamo 29/01/2019 mpaka kupitishwa kwake na baraza la kisiasa mnamo 26/03/2019 na kuendelea kupigiwa debe na vyombo vya habari tofauti tofauti wakipendelea kutumia neno “dola ya kisasa.” Hii ni mara ya kwanza kwa msemaji rasmi kuweka wazi kuhusu nia ya Mahouthi ya kusimamisha dola ya kiraia katika hali ya wazi isiyokuwa na shaka.

Dola ya kiraia ni neno la utawala wa Kimagharibi ambalo linaashiria dola ambayo ndani yake dini haina nafasi katika vipengee vyake, utungaji sheria wake and sheria zake. Badala yake inaitenga na kuiwachia dini watu binafsi kuwa na uhuru wa kufuata dini au la. Hili ndilo linaloonekana na wale walioisoma Ruwaza iliyopitishwa na Baraza Kuu la Kisiasa. Ni haki ya watu wa Yemen watakaotawaliwa na dola ya kiraia kujiuliza: Je Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ambayo siku yake ya kuzaliwa ilisherehekewa hivi majuzi, alisimamisha dola ya kiraia alipowasili Madinah, baada ya kupata nussrah kutoka kwa Ansaari katika kiapo cha pili cha Aqaba?! Au alisimamisha dola inayotawala kwa Uislamu?

Kwani hamujali au hamuhisi madhambi kwa mpango wa kusimamisha dola ya kiraia ndani ya Yemen kuwa umedhihirika ndani ya mwezi wa Rabbi’ al-Awwal ni siku chache tu tangu muliposherehekea kuzaliwa kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), kwamba mumemuhalifu au Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amewaamrisha hususan kusimamisha dola ya kiraia mwisho wa zama?! Nyinyi na waliotangulia kutawala Yemen munashindana katika uovu na kuzitenga sheria za Mwenyezi Mungu!

Maamrisho ya Mwenyezi Mungu (swt) yamekuja kiuwazi kuhusiana na utawala katika Uislamu. Yeye (swt): وَأَنِ احْكُمْ بَيْنَهُمْ بِمَا أَنْزَلَ اللَّهُ ﴿“Basi hukumu baina yao kwa aliyo yateremsha Mwenyezi Mungu na usifuate matamanio yao ukaacha Haki iliyo kujia.” [Al-Ma’idah: 48], na Yeye (swt) pia alisema:  ﴾فَلْيَحْذَرِ الَّذِينَ يُخَالِفُونَ عَنْ أَمْرِهِ أَن تُصِيبَهُمْ فِتْنَةٌ أَوْ يُصِيبَهُمْ عَذَابٌ أَلِيمٌ﴿“Basi nawatahadhari wanao khalifu amri yake, usije ukawapata msiba [hapa duniani] au ikawapata adhabu chungu [huko akhera]. [Al-Noor: 63]. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) naye alituonya dhidi ya kuwafuata wale waliotupa dola ya kiraia alipotuambia (saw): «لَتَتَّبِعُنَّ سَنَنَ مَنْ كَانَ قَبْلَكُمْ شِبْرًا بِشِبْرٍ وَذِرَاعًا بِذِرَاعٍ حَتَّى لَوْ دَخَلُوا جُحْرَ ضَبٍّ لَدَخَلْتُمُوهُ» قالوا: اليهود والنصارى؟ قال: «فَمَنْ؟» “Mutafuata njia za mataifa kabla yenu, shibri kwa shibri na dhira’ kwa dhira’ kiasi kwamba lau wataingia katika tundu la mburukenge, mutawafuata.” Tulisema, “Ewe Nabii wa Mwenyezi Mungu (ﷺ)! (Wamaanisha) Mayahudi na Wakristo?" Akasema, “Nani wengine?”

Dola ya kiraia ni dola ya kisekula ambayo ndani yake utungajisheria sio wa Mwenyezi Mungu na hautawali kwa yaliyoletwa na Mwenyezi Mungu, ni ya kubahatisha, ovu na kidhalimu na sio sehemu ya Uislamu. Ni haramu kuifuata, kuilingania, kuitaka au kuinusuru. Khilafah ni nidhamu ya utawala ndani ya Uislamu ambayo iliondoshwa kwa watu wake mwishoni mwa Vita vya Kwanza vya Dunia. Kwa hiyo tunawalingania watu wa Yemen kufanyakazi na Hizb ut Tahrir kuisimamisha (Khilafah) na kuivunja dola ya kiraia ambayo inaongozwa na Wamagharibi ndani ya Yemen ya Iman na busara.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 735417068
http://www.hizb-ut-tahrir.info
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.