Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  19 Shawwal 1434 Na: 1434/161
M.  Jumatatu, 26 Agosti 2013

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Yemen isiyokuwa na Ubwana yatafuta Ulinzi kupitia Droni!

 (Imetafsiriwa)

Rais wa Yemen Abd Rabbo Hadi katika hotuba yake katika Chuo cha Polisi huko Sana'a siku ya Alhamisi, 22 Agosti 2013 na kutangazwa na vyombo vya habari rasmi kuwa alitaka Droni zaidi za Amerika kwa sababu, kulingana na madai yake anataka kukuza na kuimarisha jeshi la Yemen kukabiliana na al-Qa’ida. Taarifa hizi ziliambatana na ripoti kwenye chaneli za habari na magazeti kwamba Pentagon imetenga dola milioni 35 kwa ajili ya droni, kufuatilia na kudhibiti vifaa ili kupambana na al-Qa'ida ndani ya Yemen. Hotuba hii iliambatana na ujio wa kamanda Amiri jeshi mkuu wa Amerika nchini Yemen siku ya Jumamosi, 24 Agosti 2013 ili kuanzisha vyumba vitatu vya opareshini kwa kushirikiana na Yemen kupambana na ugaidi.

Rais Hadi anajua kwamba maneno haya "kukuza au kuimarisha Jeshi la Yemen" yanaweza kuwadanganya watu duni wa Yemen na Wanasiasa wachanga. Ama wale wanaofuata vitendo vya kisiasa vya Wamagharibi, malengo yao na vibaraka wao na kuyaunganisha na maneno ya Mwenyezi Mungy (swt):

 ((إن الذين كفروا ينفقون أموالهم ليصدوا عن سبيل الله فسينفقونها ثم تكون عليهم حسرة ثم يغلبون))

“Hakika, wale walio kufuru hutoa mali yao ili kuzuilia Njia ya Mwenyezi Mungu. Basi watayatoa; kisha yatakuwa juu yao majuto; na kisha watashindwa.” [Al-Anfal: 36]

Na pia maneno Yake:

((ولن ترضى عنك اليهود ولا النصارى حتى تتبع ملتهم))

“Mayahudi hawawi radhi nawe, wala Wakristo, mpaka ufuate mila yao." [Al-Baqarah: 120]

Wanajua kuwa taarifa hizi sio chochote bali ni kuwakengeusha watu katika ukweli, Ambao ni, Amerika inafanya kazi kufanikisha manufaa yake pekee na inataka kuwa na vituo vya kijeshi ndani ya Yemen kupata ushawishi zaidi kwa kisingizio cha kupambana na al-Qa'ida, kwa hili inaiweka Yemen na watu wake kulengwa na droni kama vilevile ilivyo Misri na Pakistan. Kwa namna droni zitakavyo kuwa ngao kwa Amerika katika eneo kushambulia watu wa Yemen ikiwa wafanya kazi kurudisha maisha ya Kiislamu, na hiyo ni kwa sababu kwa uthibitisho kuwa ulimwengu unajua kuwa watu wa Yemen ni watu wanaopigiadebe Uislamu na Khilafah yake ijayo, karibuni kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.

Labda Rais Hadi atatueleza katika siku zijazo kwa kutumia akili yake na atasema kuwa droni ni kwa usalama wa watu wa Yemen kutokamana na mvuke wa jua!

Haishangazi kwamba katika hotuba zilizopita, Rais alisema kuwa al-Qa'ida inafanywa kuwa kubwa kuliko vile ilivyo, si hivyo tu, pia alisema kuwa aliivunja, na sasa anataka kuagiza hizi droni kuilinda nchi kutokamana na hatari zake!

Lakushangaza zaidi ni kuwa anaagiza hizi droni kulingana na maagizo ya Amerika kwa wao kutumika kumfuatilia yeye ili kupima uaminifu wake kwao, na kisha wachukue uamuzi wa kumuongezea muda au kumuondoa ipasavyo, kama wale waliomtangulia yeye.

Enyi watu wa Imani na busara, je wanawakejeli akili zenu?! Katika mambo haya, hakuna mmoja anayekubali hili isipokuwa kwa wasiokuwa na akili. Kwa nini mumenyamaza wakati ndio nyinyi mulioasi dhidi ya ukosefu wa haki? Na wakati Waamerika wanapokuja na suala likawa suala la hatima ya kuamua mumedhalilishwa kimya na kusimama na Wakandamizaji.

Yako wapi makabila ya kweli yasiyo kubali udhalimu? Wako wapi majenerali wakweli? Wako wapi Wanavyuoni wanaofuata njia ya Mwenyezi Mungu?

Viko wapi vyama vya kisiasa vinavyo kemea na kupiga kelele juu ya mambo yanayo hitaji kukemewa au kupigiwa kelele yanayo tia uziwi masikio yetu kwa kauli mbiu kama "Kifo kwa Amerika, Kifo kwa Israel"? Lakini hawachangamki katika mambo haya makubwa bali wanasubiri hisa yao ya keki katika mjadala ambao unaendeshwa na Wamagharibi, ni kama hawataki kusimama kwa upinzani kwa yule atakaye gawanya keki, kwa ajili ya kupokea hisa kubwa?! Na bunge likowapi kutokamana na makubaliano na vitendo vyote hivi, ni vipi iwe imepitishwa na wao wakati jambo hili halikuwahusu wao, sio wao wawakilishi wa watu kama wanavyodai.?!

Hizb ut Tahrir inawalingania nyinyi Enyi watu wa Yemen kusimama mbele ya agenda za Wamagharibi na kuwahesabu wahalifu wanaofanya kazi dhidi ya Umma wao na Dini yao na kufanya kazi kubadilisha kwa kuanzisha mradi wa Umma ambao Mtume (saw) alipeana bishara

"...ثم تكون خلافة راشدة على منهاج النبوة" "

"Kisha itakua Khilafah ya uongofu kwa njia ya Utume."

Hususan baada ya kushindwa serikali ya kiraia ya Kidemokrasia na uongo wake ulio dhahiri. Wamagharibi wameupeleka Ummah katika mzozo kwa kutumia mapinduzi kwa ajili ya kufanikisha manufaa yake. Lakini ole wao, hawatoweza wakati wako wakweli ambao watapiga marufuku ufisadi. Hali za Waislamu hazito makinika mpaka Khilafah yao isimamishwe na utabiri wa Mtume (saw) utimie:

((والله غالب على أمره ولكن أكثر الناس لا يعلمون))

"Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini watu wengi hawajui." [Yusuf: 21]

Abdul-Mumin Az-Zaila'i

Mkuu wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 735417068
http://www.hizb-ut-tahrir.info
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.