Alhamisi, 09 Shawwal 1445 | 2024/04/18
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Vipi Khilafah Itatatua Umasikini: SEHEMU 1

• Licha ya rasilimali na nguvu kazi nyingi, pamoja na utajiri mkubwa kabisa wa mafuta duniani na hifadhi ya madini katika ardhi za Waislamu, wengi wa Ummah wa Waislamu wanateseka katika umasikini mkubwa, wakiwa na pato la chini ya dolari 1.9 za kimarekani kwa siku ili kukidhi mahitaji yao msingi. Ukosefu mkubwa wa ajira unaokua, uzorotaji wa ukulima na viwanda, ongezeko la ushuru, kupanda mara kwa mara kwa bei pamoja na gharama ya juu ya umeme na kudumu kukosekana kwake, ni ushahidi wazi wa usimamizi mbaya na ufujaji katika ardhi zetu na ugavi mkubwa wa kimakosa wa utajiri wetu. Uwekezaji wa serikali katika miundombinu na huduma za Ummah ili kushibisha mahitaji msingi ya watu ni mchache au haupo. 

Kimsingi hizi ni najita ya sera zisizokuwa za Kiislamu kwa mujibu wa maelekezo ya ajenda za kisiasa za dola za kikoloni za kirasilimali zinazo tekelezwa na watawala ndani ya ardhi za Waislamu, ikiwemo mikopo ya IMF na Benki ya Dunia, inayo lazimisha sio tu viwango vya juu vya riba lakini pia sera haribifu za uchakachuaji uchumi ndani ya ardhi zetu Waislamu.

• Ukweli ni kuwa; ugavi wa kiusawa na wa kibinadamu wa utajiri ili kutoa mahitaji ya kila mtu sio miongoni mwa malengo ya uchumi wa kirasilimali. Fauka ya hayo, udumishaji mwanya mkubwa katika utajiri baina ya tajiri na masikini hunufaisha mfumo wa kirasilimali, kwa kuwa uwepo wake umejengwa juu ya utumiaji watu vibaya, na ukuzaji wa kipote kichache cha wamiliki rasilimali, wanaowakilisha, kudumisha, na kutawala kwa mfumo wa kirasilimali, na wale waliopagawishwa na nguvu za kimada wakiongezeka kila uchao. Hivyo basi ulafi, ushindani wa kidhulma, utumizi mbaya na muungozo wa kiuchumi wa “Samaki Mkubwa Humla Samaki Mdogo” umewanyima wanadamu haki zao na mahitaji yao msingi.  

“Kwa mujibu wa shirika la msaada wa Oxfam, mabilionea wakubwa zaidi 26 wanamiliki rasilimali nyingi zaidi kuliko wanazomiliki watu bilioni 3.8 ambao ndiyo nusu ya idadi ya mafukara duniani. Utajiri wa asilimia 1 ya matajiri zaidi duniani ni sawa na utajiri jumla wa asilimia 99 waliosalia.” “Takriban watu 10,000 kwa siku hufa kwa ukosefu wa matibabu na watoto milioni 262 hawako shuleni, kwa sababu wazazi wao hawawezi kumudu gharama ya karo, sare za shule au vitabu. Wanawake wanakufa kwa ukosefu wa huduma stahiki za uzazi na watoto wananyimwa elimu ambayo ingekuwa ndiyo njia yao ya kujitoa katika umasikini.” (Ripoti ya Oxfam ya 2019: https://www.oxfam.org.nz/reports/public-good-or-private-wealth) Khilafah Haitazuia Tu Umasikini Pekee Bali Inalenga Kuimarisha Kiwango cha Maisha cha Kila Raia Wake!     

• Kwanza; nidhamu ya kiuchumi ya Kiislamu imejengwa kwa msingi safi wa Qur’an na Sunnah pekee, inayotaka kutoka kwa mtu binafsi na dola kulinda mipaka ya Mwenyezi Mungu (swt). Uislamu unaikataa nadharia ya ongezeko la mahitaji ya wanadamu na uhaba wa rasilimali kama inavyo wasilishwa na urasilimali. Uislamu unaeleza waziwazi kuwa Mwenyezi Mungu (swt) ameumba rasilimali za kutosha ili kukidhi mahitaji ya kila mtu.

(وَسَخَّرَ لَكُم مَّا فِي السَّمَاوَاتِ وَمَا فِي الْأَرْضِ جَمِيعًا مِّنْهُ إِنَّ فِي ذَلِكَ لَآيَاتٍ لَّقَوْمٍ يَتَفَكَّرُونَ)

“Na amefanya vikutumikieni vilivyomo mbinguni na vilivyomo katika ardhi, vyote vimetoka kwake. Hakika katika haya zimo ishara kwa wale watu wanaofikiri.” [Al-Jathiyah: 13]

• Mtume wetu Muhammad (saw) amesema yafuatayo kuhusiana na mahitaji msingi ya mtu binafsi:

«لَيْسَ لِابْنِ آدَمَ حَقٌّ فِي سِوَى هَذِهِ الْخِصَالِ بَيْتٌ يَسْكُنُهُ وَثَوْبٌ يُوَارِي عَوْرَتَهُ وَجِلْفُ الْخُبْزِ وَالْمَاءِ»

“Mwanadamu hana haki zaidi kuliko mambo haya; nyumba anayoishi, na nguo anazostiri uchi wake, na kipande cha mkate na maji.” [Tirmidhi]

Hizi ndizo haki ambazo Uislamu unamhakikishia kila mtu na hizi ndizo haki ambazo urasilimali umewanyima wanadamu… Mwenyezi Mungu (swt) ameufanya kuwa wajib juu ya Khilafah kumsahilishia kila mtu kuweza kushibisha mahitaji yake msingi. Dola yapaswa kuhakikisha kuwa mja wa Mwenyezi Mungu anaweza kutimiza jukumu lake la utafutaji riziki, na kufanya juhudi za kuchuma riziki. Mwanamume mwenye uwezo ana jukumu la kufanya kazi ili kushibisha mahitaji yake mwenyewe. Ama kwa wanawake, na wale wanaume ambao hawana uwezo wa kufanya kazi, ni jukumu kuwapa masrufu yao na hii ni haki kwao, na Dola inawajibika kuwapa mahitaji yao endapo wasimamizi wao wa kiume hawana uwezo wa kufanya hivyo. Zaidi ya hayo, kutoa masrufu kwa mke ni jukumu juu ya mume. Kutoa masrufu juu ya watoto ni jukumu juu ya baba.

(وَعَلَى ٱلْمَوْلُودِ لَهُ رِزْقُهُنَّ وَكِسْوَتُهُنَّ بِٱلْمَعْرُوفِ) “Na juu ya baba yake chakula  cha kina mama, na nguo zao kwa mujibu wa ada.” [Al-Baqara: 233]

Mtume (saw) amesema:

«كَفَى بِالْمَرْءِ إِثْمًا أَنْ يُضَيِّعَ مَنْ يَقُوتُ» “Yatosheleza kuwa ni kosa kwa mume kumtelekeza aliye chini ya usimamizi wake.” (Abu Dawud, Al-Nawawi) Hii yamaanisha kuwa kazi ni wajib juu ya huyu mwanamume aliye na uwezo na endapo hatafanya kazi ataadhibiwa kama ilivyo hali kwa kila jukumu.

Kunapokosekana yeyote aliye wajibishwa kulipia masrufu, au endapo watakuwepo lakini hawana uwezo wa kulipia masrufu hayo, Shari'ah imewajibisha masrufu haya juu ya Bait al-Mal (Hazina ya Dola), kwa maana nyengine, juu ya Dola ya Khilafah. Kwani Rasulullah (saw) amesema:

«أَنَا أَوْلَى بِالْمُؤْمِنِينَ مِنْ أَنْفُسِهِمْ مَنْ تَرَكَ مَالاً فَلأَهْلِهِ وَمَنْ تَرَكَ دَيْنًا أَوْ ضَيَاعًا فَإِلَيَّ وَعَلَيَّ»

“Mimi ni bora kwa waumini kuliko nafsi zao. Yeyote anayeacha mali, basi ni ya watu wake, na anayeacha deni, au wanaomtegemea basi hilo ni langu na juu yangu,” (imeripotiwa na Muslim kutoka kwa Jabir)

Hii pia ni dalili kuwa miongoni mwa kadhia muhimu zaidi kwa Khilafah ni kusimamia mambo ya Ummah au kubuni nafasi za kazi kwa wale walio na uwezo wa kufanya kazi lakini hawana kazi.

• Ushibishaji wa Mahitaji yasiyo msingi Mahitaji ya Ziada ni lazima pia usahilishwe na Khilafah, katika njia ile ile kama katika mahitaji msingi. Dola huwarahisishia raia wote ili kuweza kushibisha mahitaji yao ya ziada (yasiyo msingi), na kuleta usawa katika mujtama kwa njia ifuatayo:

a) Kupitia kuwapa rasilimali taslimu na ziso taslimu kutoka katika fedha za Bait al-Mal, na kutoka katika ngawira za kivita, na chengine chochote mfano wa haya.

b) Kuwagawanyia baadhi ya ardhi yake ya ukulima wale wasiokuwa na ardhi ya kutosha. Wale wanaomiliki ardhi lakini hawaitumii hawapewi zaidi. Wale wasiokuwa na uwezo wa kulima ardhi zao wanapewa usaidizi wa kifedha ili kuwawezesha kuzilima.

c) Kuwapa usaidizi wale wasiokuwa na uwezo wa kulipa madeni yao kupitia kuwapa pesa za Zakah, na ngawira za kivita, na chengine chochote mfano wa haya.

Hizi ni aina zote za usaidizi ambazo hatuwezi kuzipata chini ya serikali za kirasilimali katika ardhi zetu.

• Usalama, aina zote za huduma za Ummah kama huduma za afya na elimu, ni jukumu linalopaswa kutekelezwa na Khilafah, ikiongezewa na kuhakikisha mahitaji ya watu binafsi. Haya hayana budi kufadhiliwa na hazina ya Dola (Bait al-Mal) kwa kila raia wake, bila ya kujali dini zao, rangi, jinsia au kabila.

Inapaswa kuzingatiwa kuwa ukosefu wa usalama hupelekea kushindwa kutimiza majukumu mengine yote. Hiyo ndiyo sababu ahadi ya mwanzo kabisa ya Rasulullah (saw) aliyowapa maswahaba zake, pindi alipowajuza kuhusu Hijrah, ilikuwa ni usalama:

«إِنَّ اللَّهَ عَزَّ وَجَلَّ جَعَلَ لَكُمْ إِخْوَاناً وَدَاراً تَأْمَنُونَ بِهَا»

“Allah Azza wa Jalla amewajaalieni kuwa ndugu na ardhi ambamo munapata amani ndani yake.” [Sirah, Ibn Ishaq] Kutokana na hayo, masalihi na huduma za Ummah ni lazima zitekelezwe na Dola ya Khilafah, kwa mujibu wa maneno ya Rasulullah (saw): 

«الإِمَامُ رَاعٍ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ» “Imamu (mtawala) ni mchungaji, na yeye ataulizwa kuhusu raia wake.” (imeripotiwa na Al-Bukhari kutoka kwa Abdullah Bin Umar).

• Nidhamu ya kiuchumi ya Kiislamu hairuhusu ulimbikizaji wa mali mikononi mwa wachache. Hivyo basi, wakati wowote kunapotokea mwanya, Khalifah ni lazima afanye kazi kuleta usawa kupitia kuitekeleza kivitendo aya hii:

(كَيْ لَا يَكُونَ دُولَةً بَيْنَ الْاَغْنِيَٓاءِ مِنْكُمْ)

“Ili yasiwe yakizunguka baina ya matajiri tu miongoni mwenu.” [Al-Hashr: 7]

• Uislamu kwa ujumla umeharamisha ufichaji utajiri na kufaradhisha Zakah, ili kuhakikisha kuwa utajiri unagawanywa miongoni mwa watu. Mwenyezi Mungu (swt) anaonya katika jambo hili:

(وَٱلَّذِينَ يَكْنِزُونَ ٱلذَّهَبَ وَٱلْفِضَّةَ وَلَا يُنفِقُونَهَا فِى سَبِيلِ ٱللَّهِ فَبَشِّرْهُم بِعَذَابٍ أَلِيمٍ)

“Na wanao kusanya dhahabu na fedha, wala hawazitumii katika njia ya Mwenyezi Mungu, wabashirie habari ya adhabu iliyo chungu.” [At-Tawbah: 34]

• Tunayokumbana nayo ya usimamizi mbaya na ukosefu wa miundombinu hayata kuwepo chini ya Khilafah. Chini ya Khilafah, Uislamu utaachilia kiwango kikubwa cha kipekee cha pesa katika uchumi na kuimarisha kilimo na maendeleo ya kiviwanda, pasi na kuongeza ushuru, kupitia uundaji upya wa kimsingi wa muundo wa dola, umilikaji wa Ummah na wa kibinafsi miongoni mwa hatua nyenginezo.

• Uislamu unawajibisha kuundwa kwa msingi imara wa viwanda vizito, ukisaidiwa kupitia utafiti unaoongoza wa kiulimwengu, ili kusukuma mbele Khilafah katika dori yake kama dola inayoongoza. Ukulima chini ya Khilafah ulikuwa ukionewa wivu ulimwenguni kwa karne nyingi na utaonewa tena wivu! Kwani Uislamu utaunganisha umilikaji wa ardhi pamoja na ulimaji wake wa kivitendo, utaondoa umilikaji wa kigeni wa ardhi ya ukulima, pamoja na utozaji mzito wa ushuru juu ya pembejeo za ukulima. Huu utakuwa ni utiaji nguvu usalama wa chakula pamoja na ufanisi wa kindani kama Ummah walivyofurahia kwa karne nyingi chini ya utawala wa Kiislamu. Hivyo basi leo Khilafah itayapa kipaumbele mazao yanayo waruhusu raia wake kupata mahitaji yao msingi ya chakula na mavazi kikamilifu, huku uzalishaji wa ziada ukitumiwa kwa ajili ya biashara ya kigeni. Itabuni maeneo thabiti ya malisho ili kusaidia ongezeko la uwepo wa mifugo. 

• Kwa sasa, umeme, makaa ya mawe, mafuta na gesi ya kimaumbile ni ghali na mara nyingi havipatikani kutokana na kubinafsishwa na warasilimali. Khilafah itaondoa umilikaji wa kibinafsi wa rasilimali za kawi na kuziregesha katika umilikaji wa Ummah ili nishati ipeanwe kwa usahali na vile vile kwa urahisi. Itaondoa ushuru juu ya nishati na mafuta ambao umefumua zaidi bei zake. Hivyo basi Khilafah itaonyesha ukweli wa Dini ya Uislamu kivitendo kwa ulimwengu uliosambaratishwa kutokana na mfumo fisadi wa urasilimali ambao unaporomoka.  

• Mojawapo ya ala za ukandamizaji mbaya zaidi wa uchumi wa kirasilimali ni utozaji ushuru! Ambapo ndani ya Khilafah, hakuna ushuru wa mapato wala ushuru wa mauzo, kwa sababu mali ya mtu binafsi kiasili ni haramu kuchukuliwa pasi na haki. Utozaji ushuru hufanywa kwa utajiri wa ziada fauka ya unaohitajika kushibisha mahitaji msingi na hili pia liko chini ya masharti makali. Kinachoruhusu sera hii ya utozaji wa chini wa ushuru ni kule kuwa Khilafah ina vyanzo vya kutosha vya mapato kutoka katika mali ya Ummah na Dola, pamoja na mkusanyiko wa hukmu za kipekee za uzalishaji mapato kutoka katika ukulima na viwanda. 

• Baada ya kuunyima Ummah mapato yake stahiki na pia kuyanyonga machumo yake na uwezo wa kununua na kuzalisha, serikali vibaraka katika ardhi zetu zimechukua mikopo ya riba kutoka katika nchi za kikoloni za kikafiri. Mikopo hii ni mtego wa kinyama, ulioundwa ili kuzidumisha ardhi za Waislamu ndani ya mikopo, kuzipokonya rasilimali zetu, na kupunguza pakubwa uwezo wetu wa kusimama kwa miguu yetu kupambana na Magharibi.

• Ongezeko la mara kwa mara la mfumko wa bei katika ardhi zetu ni kutokana na pesa zinazo pungua thamani yake daima, kwa kuwa hazikujengwa juu ya dhahabu na fedha kama inavyo wajibishwa na Shari'ah. Pesa za dola zitaasisiwa tena juu ya kipimo cha dhahabu na fedha ambacho ndiyo ngome ya kweli ya kuondoa mfumko wa bei kwa mzizi wake. Khilafah itatoa pesa yake huru, iliyofungwa kwa dhahabu na fedha, na haitafungamanishwa kwa pesa yoyote ya kigeni kwa njia yoyote ile. Khilafah haitachukua mikopo yoyote ya riba kutoka katika nchi za kikoloni za kikafiri.

• Khilafah itarudisha tena ardhi zetu katika ufanisi na neema kama zilivyokuwa katika zama za nyuma chini ya utawala wa Uislamu. Maneno ya Rasulullah (saw) sio tu ni dalili ya majukumu na wajibu wa Khilafah, ni ahadi na bishara njema.

«الإِمَامُ رَاعٍ وَهُوَ مَسْئُولٌ عَنْ رَعِيَّتِهِ» “Imamu ni mchungaji na yeye ni mwenye kuulizwa kuhusu raia wake”

• Afrika, kwa mfano, ilikuwa mbali kabisa na kuwa sehemu masikini na yenye njaa zaidi ya ulimwengu huu wakati wa zama za Khalifa Umar ibn Abdul Aziz, kwa sababu hakutekeleza chochote isipokuwa hukmu na qaida za Dini ya Uislamu.

Imesimuliwa na Yahya bin Said, aliyekuwa Wali wa wakati huo katika zama za utawala wa Khalifa Umar bin Abdulaziz (ra), kuwa alisema: “Nilitumwa na Umar bin Abdul Aziz kukusanya zaka kutoka Afrika. Baada ya kuzikusanya, nilidhamiria kuwapa masikini. Lakini, sikumpata yeyote. Umar bin Abdul Aziz amewafanya watu wote kuwa matajiri wakati wa zama zake. Hatimaye, niliamua kutumia hazina hiyo ya zaka kuwanunua na kuwaacha huru watumwa” Ibn Abd Hakam, Abdullah (1994) Al-Khalifat al-Adil Umar ibn Abd Aziz: Khamis al-Khulafa al-Rasyidin. Dar al-Fadilat, Kaherah 78

• Kwa hivyo yasadikisheni maneno ya Mwenyezi Mungu (swt), kwa sababu tayari muna imani kwayo, ili sisi kama Ummah na waliosalia ulimwenguni tufurahie matunda ya Uislamu haraka iwezekanavyo, inshaallah!

(يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُواْ أَنَّ اللّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ)

“Enyi mulio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapokuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal: 24]

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Zehra Malik
Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Kwa maelezo zaidi na ya kina, tafadhali soma:

Kielelezo cha Katiba au Dalili Zake Muhimu – Sehemu ya 2 - (Nidhamu ya Kiuchumi, Sera ya Elimu, Sera ya Kigeni) na Hizb ut Tahrir
http://www.hizbut-tahrir.org/PDF/EN/en_books_pdf/16_Muqaddimat_V2_Eng_07.05_.2013_.pdf

Uchumi wa Pakistan chini ya Khilafah na Hizb ut Tahrir / Wilayah Pakistan
http://www.hizbut-tahrir.org/PDF/EN/en_books_pdf/PK_Revival_of_the_Economy_in_Pakistan_EN_22.06_.2013_.pdf

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 26 Aprili 2020 10:55

Andika maoni

Hakikisha umejaza (*) habari zinazohitajika palipoashiriwa. Kodi za HTML haziruhusiwi.

rudi juu

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu