Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

 AU kama Mtangulizi wake OAU ni Zana ya Kikoloni ambayo ya

Muhalalisha Muuaji na Mvazi Umbile la Kiyahudi la ‘Israel’

Habari:

Mnamo Alhamisi, 22 Julai 2021 Waziri wa Kigeni wa Israel Yair Lapid alitangaza kwamba Israel imejiunga na Muungano wa Afrika (AU) kama dola mtazamaji. Alisema kuwa Alhamisi ilikuwa ni siku ya sherehe kwa mahusiano ya Israel na Afrika, akitaja kuwa hivi sasa Israel ina mahusiano na nchi 46 za kutoka Afrika. Baada ya tangazo hilo kuthibitishwa na Mwenyekiti wa Tume ya Muungano wa Afrika (AUC), Moussa Faki, lilisababisha patashika kubwa huku Algeria, Misri, Libya, Tunisia, Mauritania, Comoros na Djibouti waliwasilisha upingaji wao wa hatua hiyo iliyochukuliwa na mwenyekiti wa AUC. Barua yao ilitiwa saini na Jordan, Kuwait, Qatar, Palestina na Yemen, na kuongezea uwakilishi wa Ligi ya Kiarabu. Upande mwingine, Botswana na Namibia zilizipinga maamuzi hayo ilhali serikali ya Afrika Kusini ilitoa taarifa ikisema kuwa AUC ilichukuwa maamuzi hayo kibinafsi pasina kuwataka ushauri wanachama wake. (The Star, 07/08/2021)

Maoni:

Patashika hiyo ni njama tu ya nchi hizo kuokoa sura zao mbele ya raia wao. Lakini kiuhalisia wote ni washirika katika uhalifu pamoja na AU kwani sera yake msingi ni ile ya suluhisho la dola mbili! Kama ilivyothibitishwa na kauli ya mwenyekiti wa AUC kwamba ana matumaini kuwa kuidhinishwa kwa ‘Israel’ kuwa dola mtazamaji itazidisha kasi ya mchakato wa AU ya kutimiza msingi wa dola mbili na kurudisha amani baina ya dola mbili na watu kutoka pande mbili!

Umbile la Kiyahudi ‘Israel’ ni kivuli tu ambacho kipo kama natija ya usalama kinaopewa na mataifa iliyokizunguka. Mataifa hayo yanatawaliwa na watawala vibaraka wa wakoloni ambao wameuza roho zao kwa wakoloni Wamagharibi walioko Washington, London na Paris. Hivyo basi, sera zao hutegemea maslahi ya mabwana zao.   Kupinga kwao sio chochote bali ni porojo ili kuwahadaa watu wa Palestina kwamba wana uungwaji mkono kutoka kwao! Badala yake wao ndio wanaopiga njama na kuwachimbia makaburi!

Palestina ni suala la Kiislamu ambalo linahitaji dola huru ya Kiislamu ya Khilafah iliyosimamishwa kwa njia ya Utume ili kuyaunganisha majeshi yake na kuikomboa Al-Aqsa na ardhi nyingine za Waislamu. Kukosekana kwa Khilafah kunatoa nafasi kwa zana za kikoloni kama vile AU na mfano wake ili kuhalalisha kuwepo kwa muuaji na mvamizi umbile la Kiyahudi ‘Israel.’ Ama kuhusu Afrika ni shamba la kikoloni tu, watawala wake vibaraka ni mameneja katika shamba la kikoloni na raia wake ni wafanyakazi wa kikoloni.

Haishangazi, kuona kuwa Uingereza, Amerika, Ufaransa n.k ni dola watazamaji katika AU! Wanadhamini miradi yake, wanachora sera zake na kujenga miundombinu yake kwa gharama kubwa ili wapate nini?! Hakika, inathibitisha ule msemo, ‘mbwa ni mtumwa kwa bwana wake.’ Madhara yasiyo hesabika yanayo sababishwa na dola za kikoloni za Kimagharibi barani Afrika and duniani kwa upana yameanzia katika ukandamizaji wa kifikra hadi uporaji wa rasilimali. Hivi sasa Amerika iko safu ya mbele kuongoza katika mashambulizi dhidi ya kusimamisha tena dola huru ya Kiislamu, Khilafah.

Minong’ono ya mabadiliko haiwezi kupuuziliwa mbali hususan sasa hivi ambapo kuanguka kwa utawala wa Amerika kuko karibu. Matukio yanayotokea ndani ya Amerika, inayojidai kuwa ni ngome ya demokrasia inafichua kufeli kikamilifu kwa mungu wa kidemokrasia. Hivyo basi, dola kuu mbadala iko karibu kuchipuza ili kuwakomboa wanadamu kutoka katika ukandamizaji na maangamivu ya mfumo wa Kimagharibi wa kisekula wa kirasilimali na walinganizi wake. Hakika, mbadala sio nyingine bali ni Khilafah iliyosimamishwa kwa njia ya Utume.

Kwa sababu hiyo, sasa ndio wakati wa kujiunga na kufanyakazi ya mradi wa #TurudisheniKhilafah. Mradi ambao lengo lake ni kuwakomboa wanadamu kutoka katika kuabudu viumbe hadi kumuabudu Muumba wao – Mwenyezi Mungu (swt). Mradi ambao utaitikia vilio vya walioko Al-Aqsa, Kashmir, Syria, Yemen, Afghanistan nk. Kurudisha maisha ya Kiislamu kupitia kusimamisha tena Khilafah kutaleta usalama, amani, utulivu na ustawi wa kweli ambao unahitajika kwa dharura mno. Kwani serikali ya Khilafah itatekeleza kwa ukamilifu nidhamu za Kiislamu zinazochipuza kutoka katika Shari’ah.

Imeandikwa kwa ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Ali Nassoro Ali

                        Mwanachama wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.