Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Silsila ya Maswali Yaliyowasilishwa kwa

Amiri wa Hizb ut Tahrir

Sheikh Ata Bin Khalil Abu Al-Rashtah Katika Ukurasa Wake wa Facebook

Jibu la Swali
Habari za Zama za Mwisho na Kushuka kwa Masihi (AS)

Kwa: Hamzeh Shihadeh

Swali:

Assalam Aleykum wa Rahmatullah wa Barakatuh

Twamuomba Mwenyezi Muungu, ewe Sheikh wetu, kwamba uwe na afya njema na ustawi, na kwamba akupe wewe, sisi, na Waislamu wote Khilafah kwa njia ya Utume...

Tumechanganyikiwa na visa na simulizi za kushuka kwa Nabii Isa, amani iwe juu yake, zama za mwisho, kuja kwa Mahdi anayesubiriwa, na habari za Dajjal mwenye jicho moja, na watu wa Juj na Majuj. Ni yapi sahihi na yapi ya kukataliwa katika haya?

Jibu:

Waaleykum Salaam wa Rahmatullah wa Barakatuh,

Mwenyezi Mungu akubariki kwa dua yako njema kwetu, na sisi tunakuombea kheri.

Kwanza, ni lazima ieleweke kwamba taarifa zilizomo katika maandiko ya Kiislamu, iwe kuhusu matukio ya zamani au yajayo, lazima zithibitishwe ili zikubaliwe; yaani, hazipaswi kuwa dhaifu au za kubuniwa. Nitataja baadhi ya dalili sahihi zinazohusiana na swali lako, lakini sitataja zote; Unaweza kupata zaidi katika vitabu vinavyohusika vya fiqh ya Kiislamu:

A- Kuhusu Yajuj na Majuj, wametajwa katika Quran Tukufu:

Katika Surah Al-Kahf:

﴿قَالُوا يَا ذَا الْقَرْنَيْنِ إِنَّ يَأْجُوجَ وَمَأْجُوجَ مُفْسِدُونَ فِي الْأَرْضِ فَهَلْ نَجْعَلُ لَكَ خَرْجاً عَلَى أَنْ تَجْعَلَ بَيْنَنَا وَبَيْنَهُمْ سَدّاً * قَالَ مَا مَكَّنِّي فِيهِ رَبِّي خَيْرٌ فَأَعِينُونِي بِقُوَّةٍ أَجْعَلْ بَيْنَكُمْ وَبَيْنَهُمْ رَدْماً * آتُونِي زُبَرَ الْحَدِيدِ حَتَّى إِذَا سَاوَى بَيْنَ الصَّدَفَيْنِ قَالَ انْفُخُوا حَتَّى إِذَا جَعَلَهُ نَاراً قَالَ آتُونِي أُفْرِغْ عَلَيْهِ قِطْراً * فَمَا اسْطَاعُوا أَنْ يَظْهَرُوهُ وَمَا اسْتَطَاعُوا لَهُ نَقْباً * قَالَ هَذَا رَحْمَةٌ مِنْ رَبِّي فَإِذَا جَاءَ وَعْدُ رَبِّي جَعَلَهُ دَكَّاءَ وَكَانَ وَعْدُ رَبِّي حَقّاً * وَتَرَكْنَا بَعْضَهُمْ يَوْمَئِذٍ يَمُوجُ فِي بَعْضٍ وَنُفِخَ فِي الصُّورِ فَجَمَعْنَاهُمْ جَمْعاً

Wakasema: Ewe Dhul-Qarnaini! Hakika Juju-wa-maajuju wanafanya uharibifu katika nchi. Basi je, tukulipe ujira ili utujengee baina yetu na wao ngome? Akasema: Yale Mola wangu aliyo niwezesha ni bora zaidi. Lakini nyinyi nisaidieni kwa nguvu zenu. Nitakujengeeni kizuizi baina yenu na wao. Nileteeni vipande vya chuma. Hata alipo ijaza nafasi iliyo kati ya milima miwili, akasema: Vukuteni. Hata alipo kifanya (chuma) kama moto akasema: Nileteeni shaba iliyo yayuka niimwagie. Basi hawakuweza kuukwea, wala hawakuweza kuutoboa. Akasema: Hii ni rehema itokayo kwa Mola wangu Mlezi. Na itapo fika ahadi ya Mola wangu Mlezi atauvunja vunja. Na ahadi ya Mola wangu Mlezi ni kweli tu. Na siku hiyo tutawaacha wakisongana wao kwa wao. Na baragumu litapulizwa, na wote watakusanywa pamoja.” [Al-Kahf: 94 – 99]

B- Kuhusu kushuka kwa Nabii Isa, amani iwe juu yake, zama za mwisho, kuja kwa Mahdi anayesubiriwa, na habari za Dajjal mwenye jicho moja, tumewasilisha mambo haya katika majibu yaliyopita, na nitanukuu kutoka kwayo:

* Jibu la swali la tarehe 1 Februari 2014, ambalo lilisema:

[... Ahmad amesimulia katika Musnad yake kutoka kwa Abu Sa'id al-Khudri, ambaye alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), amesema:

«أُبَشِّرُكُمْ بِالْمَهْدِيِّ يُبْعَثُ فِي أُمَّتِي عَلَى اخْتِلَافٍ مِنَ النَّاسِ وَزَلَازِلَ، فَيَمْلَأُ الْأَرْضَ قِسْطاً وَعَدْلاً، كَمَا مُلِئَتْ جَوْراً وَظُلْماً، يَرْضَى عَنْهُ سَاكِنُ السَّمَاءِ وَسَاكِنُ الْأَرْضِ، يَقْسِمُ الْمَالَ صِحَاحاً»

“Ninakupa habari njema za Mahdi. Atatumwa kwa Umma wangu wakati wa mzozo na ghasia miongoni mwa watu. Ataijaza dunia kwa haki na usawa, kama vile ilivyojaa udhalimu na ukandamizaji. Wakaazi wa mbinguni na wakaazi wa ardhini wataridhika naye, atagawanya mali kwa swihah.”] mtu mmoja akamuuliza: maana ya swihah ni nini? Akasema,

«بِالسَّوِيَّةِ بَيْنَ النَّاسِ...»].

 “Sawa kwa sawa miongoni mwa watu…”

* Jibu la swali la Aprili 1, 2016, ambalo lilisema:

[... * Kuhusu Mahdi, kuna hadith kuhusu maudhui hii: sahih, hasan, dhaifu, na za kubuniwa... wengi katika historia wamejidai kuwa Mahdi... Si vigumu kwa mtu kutofautisha mema na mabaya katika jambo hili. Inatosha, kama ilivyotajwa katika hadith sahih, kwamba Mahdi ni mtawala mwadilifu ambaye atakuja zama za mwisho na kupata dhulma, kwa hivyo atatawala kwa haki na kuondoa dhulma. Jina lake litakuwa sawa na jina la Mtume (saw) na jina la baba yake, yaani, “Muhammad ibn Abdullah.” Atapewa kiapo cha utiifu (bay’ah) baina ya Jiwe Jeusi (Hajar al-Aswad) na Maqaam Ibrahim... Huenda akawa mmoja wa makhalifa wa Khilafah Rashida ya pili, na Mwenyezi Mungu mjuzi zaidi na mwingi wa hekima:

- Nu'aym ibn Hammad amesimulia katika Al-Fitan kutoka kwa Abu Hurayrah (ra) ambaye alisema:

«يُبَايعُ الْمَهْدِيُّ بَيْنَ الرُّكْنِ وَالْمَقَامِ، لَا يُوقِظُ نَائِماً، وَلَا يُهْرِيقُ دَماً»،

“Mahdi atapewa kiapo cha utiifu (bay’ah) baina ya Jiwe Jeusi na Maqaam Ibrahim, naye hataamshwa aliyelala, na wala hatamwaga damu.” Katika simulizi nyingine kutoka kwa Qatadah, alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«إِنَّهُ يَخْرُجُ مِنَ الْمَدِينَةِ إِلَى مَكَّةَ فَيَسْتَخْرِجُهُ النَّاسُ مِنْ بَيْنِهِمْ، فَيُبَايعُونَهُ بَيْنَ الرُّكْنِ وَالْمَقَامِ وَهُوَ كَارِهٌ»...

“Ataondoka Madina kwenda Makka, na watu watamtoa miongoni mwao, na watatoa kiapo cha utiifu (bay’ah) kwake baina ya Jiwe Jeusi na Maqaam Ibrahim, ilhali yeye hataki.”

... Ibn Hibban alisimulia katika Sahih yake kutoka kwa Asim, kutoka kwa Zirr, kutoka kwa Abdullah, ambaye alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«لَا تَقُومُ السَّاعَةُ حَتَّى يَمْلِكَ النَّاسَ رَجُلٌ مِنْ أَهْلِ بَيْتِي، يُوَاطِئُ اسْمُهُ اسْمِي، وَاسْمُ أَبِيهِ اسْمَ أَبِي، فَيَمْلَؤُهَا قِسْطاً وَعَدْلاً».

“Kiyama hakitasimama mpaka mtu kutoka kwa watu wa Nyumba yangu atawale, ambaye jina lake litakuwa sawa na langu, na jina la baba yake litakuwa sawa na langu, naye atajaza uadilifu na usawa.”

- Al-Hakim amepokea katika Mustadrak 'ala al-Sahihayn yake hadith kutoka kwa Abu Sa'id al-Khudri (ra) kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«يَخْرُجُ فِي آخِرِ أُمَّتِي الْمَهْدِيُّ يَسْقِيهِ اللَّهُ الْغَيْثَ، وَتُخْرِجُ الْأَرْضُ نَبَاتَهَا، وَيُعْطِي الْمَالَ صِحَاحاً، وَتَكْثُرُ الْمَاشِيَةُ وَتَعْظُمُ الْأُمَّةُ، يَعِيشُ سَبْعاً أَوْ ثَمَانِياً»

“Mahdi atatokea mwishoni mwa Umma wangu. Mwenyezi Mungu atamnyesheza mvua, ardhi itatoa mimea yake, utajiri utagawanywa kwa usawa, mifugo itaongezeka, na Umma utakuwa mkubwa. Ataishi kwa miaka saba au minane.” ... Kuna hadith zengine pia.

Na pindi tunapomwona mtu mwenye sifa hizi, tunaweza kuchunguza kama yeye ni Mahdi au la. Hata hivyo, ikiwa hana sifa hizi, hatuwezi kuchunguza kama yeye ni Mahdi au la; badala yake, anaangukia katika kundi la udanganyifu na madai ya uongo...] Mwisho wa nukuu.

* Jibu la swali la tarehe 17 Aprili 2014, ambalo lilisema:

[...Kuhusu maudhui ya Isa, amani iwe juu yake, kushuka kwake Duniani, na kuuawa kwa Dajjal... kuna hadith sahih kuhusu maudhui hii zinazoonyesha kwamba Dajjal ni mtu aliyepotoka na mwenye kupotosha ambaye atakuja zama za mwisho, wakati mwingine akidai kuwa Mungu, na wakati mwingine akidai kuwa Masihi, kwa uwongo na kwa uzushi. Atawaonyesha watu kitu kinachofanana na Pepo na kitu kinachofanana na Moto. Kile ambacho watu wanaona kama Pepo kwa kweli ni Moto, na kile ambacho watu wanaona kama Moto kwa kweli ni maji baridi na safi... Atawaadhibu vikali wale wanaomuasi na kuwapa wale wanaomtii raha za kidunia kama vile chakula, nyama, na maji... huku akiwazuia wale wanaomuasi. Lakini kuwazuia Neema hii kwa muumini haimdhuru muumini, kwani Dajjal ni duni sana kwa Mwenyezi Mungu kuweza kumfitini muumini... Kwa vyovyote vile, yeye ni fitna na majaribu kwa watu, na muumini anajua kwamba yeye ni Dajjal muongo, kwa hivyo anabaki imara katika imani yake bila kujali jinsi majaribu ya Dajjal yanavyoweza kuwa makali... Na wakati wa majaribu haya ya Dajjal kwa watu, na dai lake la kuwa Masihi, wakati huo Masihi Isa, amani iwe juu yake, atashuka na kumuua Dajjal huyo:

- Muslim amesimulia kutoka kwa Uqbah ibn Amr Abu Masoud al-Ansari, ambaye alisema: Nilikwenda naye kwa Hudhayfah ibn al-Yaman, na Uqbah akamwambia: Niambie ulichosikia kutoka kwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), kuhusu Dajjal. Akasema:

«إِنَّ الدَّجَّالَ يَخْرُجُ، وَإِنَّ مَعَهُ مَاءً وَنَاراً، فَأَمَّا الَّذِي يَرَاهُ النَّاسُ مَاءً، فَنَارٌ تُحْرِقُ، وَأَمَّا الَّذِي يَرَاهُ النَّاسُ نَاراً، فَمَاءٌ بَارِدٌ عَذْبٌ، فَمَنْ أَدْرَكَ ذَلِكَ مِنْكُمْ، فَلْيَقَعْ فِي الَّذِي يَرَاهُ نَاراً، فَإِنَّهُ مَاءٌ عَذْبٌ طَيِّبٌ»

 “Hakika Dajjal atatokea, Na hakika, pamoja naye kuna maji na moto. Kile ambacho watu wanaona kama maji kwa kweli ni moto unaowaka, na kile ambacho watu wanaona kama moto ni maji baridi na matamu. Kwa hivyo yeyote kati yenu atakayeyakuta haya, na basi na azame kwenye kile anachokiona kama moto, kwani ni maji matamu, safi.” Kisha Uqbah akasema, “Nami nilisikia hili likithibitisha alichosema Hudhayfah.”

- Muslim aliripoti kwamba Anas ibn Malik alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«مَا مِنْ نَبِيٍّ إِلَّا وَقَدْ أَنْذَرَ أُمَّتَهُ الْأَعْوَرَ الْكَذَّابَ، أَلَا إِنَّهُ أَعْوَرُ، وَإِنَّ رَبَّكُمْ لَيْسَ بِأَعْوَرَ، وَمَكْتُوبٌ بَيْنَ عَيْنَيْهِ ك ف ر»

“Hakuna nabii ambaye hakuuonya Umma wake kuhusu mwongo mwenye jicho moja. Hakika, yeye ni mwenye jicho moja, na Mola wenu si mwenye jicho moja. Na imeandikwa kati ya macho yake ni K-F-R.” Katika riwaya nyengine ya Muslim:

- Muslim aliripoti kwamba Anas ibn Malik alisema: Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«مَا مِنْ نَبِيٍّ إِلَّا وَقَدْ أَنْذَرَ أُمَّتَهُ الْأَعْوَرَ الْكَذَّابَ، أَلَا إِنَّهُ أَعْوَرُ، وَإِنَّ رَبَّكُمْ لَيْسَ بِأَعْوَرَ، وَمَكْتُوبٌ بَيْنَ عَيْنَيْهِ ك ف ر»

“Hakuna nabii ambaye hakuuonya Umma wake kuhusu mwongo mwenye jicho moja. Hakika, yeye ni mwenye jicho moja, na Mola wenu si mwenye jicho moja. Na imeandikwa kati ya macho yake ni K-F-R.” Katika riwaya nyengine ya Muslim:

مَكْتُوبٌ بَيْنَ عَيْنَيْهِ كَافِرٌ، يَقْرَؤُهُ كُلُّ مُؤْمِنٍ، كَاتِبٍ وَغَيْرِ كَاتِبٍ».

“Imeandikwa kati ya macho yake ni Kafir (kafiri), ambayo kila muumini, awe anajua kusoma au asiyejua kusoma, anaweza kusoma.”

- Na katika riwaya ya Muslim kuhusu mahali ambapo Isa, amani iwe juu yake, atashuka, na kuhusu mahali ambapo atamuua Dajjal:

«فَبَيْنَمَا هُوَ كَذَلِكَ إِذْ بَعَثَ اللهُ الْمَسِيحَ ابْنَ مَرْيَمَ، فَيَنْزِلُ عِنْدَ الْمَنَارَةِ الْبَيْضَاءِ شَرْقِيَّ دِمَشْقَ، بَيْنَ مَهْرُودَتَيْنِ، وَاضِعاً كَفَّيْهِ عَلَى أَجْنِحَةِ مَلَكَيْنِ، إِذَا طَأْطَأَ رَأْسَهُ قَطَرَ، وَإِذَا رَفَعَهُ تَحَدَّرَ مِنْهُ جُمَانٌ كَاللُّؤْلُؤِ، فَلَا يَحِلُّ لِكَافِرٍ يَجِدُ رِيحَ نَفَسِهِ إِلَّا مَاتَ، وَنَفَسُهُ يَنْتَهِي حَيْثُ يَنْتَهِي طَرْفُهُ، فَيَطْلُبُهُ حَتَّى يُدْرِكَهُ بِبَابِ لُدٍّ، فَيَقْتُلُهُ...»].

“Akiwa katika hali hiyo, Mwenyezi Mungu atamtuma Masihi, mwana wa Mariam, naye atashuka kwenye Mnara Mweupe mashariki mwa Damascus, kati ya miamba miwili, akiweka mikono yake juu ya mabawa ya malaika wawili. Anapoinamisha kichwa chake, kinadondoka, na anapokiinua, lulu kama vito vitashuka kutoka humo. Hakuna kafiri atayesikia harufu ya pumzi yake isipokuwa atakufa.” Pumzi yake inaishia pale ambapo macho yake yanaishia kuona, kwa hivyo anamtafuta hadi atamkamata kwenye lango la Lud, na kumuua...”]

C. Kuhusu ushawishi wa Dajjal kwenye matendo yetu atakapoonekana zama za mwisho, hautamuathiri muumini, kwa sababu:

- Uongo wake uko wazi kwa kila mtu mwenye utambuzi na ufahamu. Dai lake la kuwa Mungu ni dai la uongo ambalo hakuna mtu mwenye akili timamu angeamini. Yeye ni kiumbe mwenye kikomo, asiye mkamilifu, asiye mkamilifu kabisa. Ana jicho moja, na kwa hivyo yeye ni kiumbe aliyeumbwa, na hili liko wazi kwa kila mtu mwenye akili timamu.

Madai yake kwamba yeye ni Masihi, Isa mwana wa Mariam, pia ni ya uongo, kwani ana jicho moja, na kile kilichosimuliwa kuhusu sifa za Isa, amani iwe juu yake, ni kwamba yuko katika umbo kamili na mwenye tabia njema... Al-Bukhari amesimulia katika Sahih yake kutoka kwa Abdullah ibn Umar, Mwenyezi Mungu awe radhi na wote wa wawili, kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), amesema:

«أُرَانِي اللَّيْلَةَ عِنْدَ الكَعْبَةِ، فَرَأَيْتُ رَجُلاً آدَمَ، كَأَحْسَنِ مَا أَنْتَ رَاءٍ مِنْ أُدْمِ الرِّجَالِ، لَهُ لِمَّةٌ كَأَحْسَنِ مَا أَنْتَ رَاءٍ مِنَ اللِّمَمِ قَدْ رَجَّلَهَا، فَهِيَ تَقْطُرُ مَاءً، مُتَّكِئاً عَلَى رَجُلَيْنِ، أَوْ عَلَى عَوَاتِقِ رَجُلَيْنِ، يَطُوفُ بِالْبَيْتِ، فَسَأَلْتُ: مَنْ هَذَا؟ فَقِيلَ: المَسِيحُ ابْنُ مَرْيَمَ.. وَإِذَا أَنَا بِرَجُلٍ جَعْدٍ قَطَطٍ، أَعْوَرِ العَيْنِ اليُمْنَى، كَأَنَّهَا عِنَبَةٌ طَافِيَةٌ، فَسَأَلْتُ: مَنْ هَذَا؟ فَقِيلَ: المَسِيحُ الدَّجَّالُ».

“Nilijiona usiku kwenye Kaaba, na nikamwona mtu mwenye ngozi nyeusi, mrembo zaidi kati ya watu wenye ngozi nyeusi ambao ungeweza kuwaona, mwenye nywele nzuri zaidi ungeweza kuziona, ambazo alikuwa amezichana, na zilikuwa zikidondoka maji, akiwa ameegemea watu wawili, au kwenye au kwenye mabega ya watu wawili wakizunguka Kaaba, nikauliza, “Huyu ni nani?” ikajibiwa, “Masihi, mwana wa Mariam.” Kisha nikamwona mtu mwenye nywele zilizopinda, chongo katika jicho lake la kulia, ambalo lilionekana kama zabibu inayoelea. Nikauliza, “Huyu ni nani?” ikajibiwa, “Masihi Dajjal.”

- Vivyo hivyo, neno “kafiri” limeandikwa kati ya macho ya Dajjal, na kama ilivyotajwa katika hadith, atalisoma muumini asiyejua kusoma na kuandika na msomi. Kwa hivyo, anabeba ukanushaji wake mwenyewe. Mtume (saw) alitufahamisha katika hadith zake kuhusu Dajjal, akisema kwamba hatawaathiri waumini. Akatufafanulia uhalisia wake na uhakika wake, na kwamba yeye ni fitna na majaribu ambayo waumini wataokolewa nayo kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt).

Haya ndiyo ninayoyaamini kuwa nguvu zaidi, na Mwenyezi Mungu ni mjuzi zaidi mwingi wa hekima.

Hakuna haja ya kuchunguza kwa undani zaidi katika maudhui ya Dajjal, kwani tuliyotaja yanatosha, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu.

Ndugu Yenu,

Ata bin Khalil Abu Al-Rashtah

18 Sha’ban 1447 H

06/02/2026 M 

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.