Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Ni Dhambi Kubwa Kwa Ndege za Mayahudi Kuvuka Anga ya Tawala, Kuipiga Mabomu Iran na Kurudi Salama Bila Kutunguliwa na Tawala hizi Hata kwa Risasi Moja!
(Imetafsiriwa)

Trump alisema katika chapisho kwenye jukwaa la Kijamii la ‘Truth’: ["Iran na Israel wanapaswa kufanya makubaliano, na watafanya makubaliano, kama vile nilivyozifanya India na Pakistan kufanya." Aliendelea: "Vivyo hivyo, tutakuwa na AMANI, hivi karibuni, kati ya Israel na Iran! Miito mingi na mikutano inafanyika hivi sasa."(Sky News,15/6/2025). Mnamo Jumapili, msemaji wa jeshi la umbile la Kiyahudi alisema kupitia jukwaa la X kwamba "Israel ilitoa onyo kwa Wairan wanaoishi karibu na vinu vya nyuklia nchini Iran kuhama makaazi yao." Wakati huo huo, msemaji wa jeshi la 'Israel' alisema kuwa jeshi lilishambulia kituo cha nyuklia katika mji wa Isfahan, katikati mwa Iran. Tangu alfajiri ya Jumapili, Iran ilianza kurusha raundi mpya za makombora kwenye shabaha ndani ya 'Israel', na kusababisha vifo na makumi ya majeruhi, na kusababisha uharibifu mkubwa kwa nyumba na majengo. Kwa kujibu, Tehran imekuwa chini ya mashambulizi ya 'Israeli'. (Al Jazeera,15/6/2025).

Umbile la Kiyahudi lilitangaza mnamo Jumamosi, 14/6/2025, kwamba wanasayansi 9 na wataalamu katika mpango wa nyuklia wa Iran waliuawa wakati wa uvamizi wake nchini, na hivyo kuongeza idadi ya vifo iliyotangazwa hapo awali, nao ni: Ali Bakhoy Karimi, Mansour Askari, na Saeed Borji, ambao ni wataalamu wa mekaniki, fizikia, na vifaa vya uhandisi, mtawaliwa, katika uvamizi mnamo Ijumaa, kwa mujibu wa jeshi. Hili lilikuja katika tangazo lililothibitishwa na Shirika la Habari la Tasnim la Iran. Umbile la Kiyahudi lilikuwa limeanzisha "shambulizi ambalo halijawahi kushuhudiwa nchini Iran alfajiri ya Ijumaa, 13/6/2025, likilenga kitovu cha mpango wa nyuklia wa Iran na viongozi wakuu wa kijeshi. Huku Iran ikithibitisha kwamba ilirusha mamia ya makombora mnamo Ijumaa jioni mwanzoni mwa jibu lake kwa Israel." (CNN, 14/6/2025)

Mara tu baada ya shambulizi la Kiyahudi, Rais wa Marekani Donald Trump alitangaza mnamo Ijumaa, 13/6/2025: [“Shambulizi la Israel dhidi ya Iran limekuwa bora kabisa,” akiitaka ikamilishe makubaliano kuhusu mpango wake wa nyuklia. Akijibu swali kutoka kwa ABC: "Je, kuna dori ya Marekani katika shambulizi la Iran?" alisema, “Sitaki kujibu hilo.” Alisema kwenye jukwaa la Kijamii la ‘Truth’, "Iran lazima ifanye mapatano, kabla haijapoteza kila kitu, na kuokoa kile ambacho hapo awali kilijulikana kama Himaya ya Iran." Aliongeza kuwa aliionya Tehran kwamba "Marekani inatengeneza zana bora zaidi za kijeshi zenye hatari zaidi popote duniani ... Israel inazo nyingi, na nyingi zaidi zinakuja - na wanajua jinsi ya kuzitumia." Katika taarifa mithili ya hizo, Trump alisema: "Leo ni siku ya 61. Niliwaambia la kufanya, lakini hawakuweza kufika huko. Sasa wamefika, labda, ni nafasi ya pili!" (Al Jazeera, 13/6/2025)]

Kwa kutafakari matukio haya, yafuatayo yanadhihirika:

1- Ni wazi kutokana na matukio haya kwamba Mayahudi hawakuishambulia Iran isipokuwa kwa amri ya Marekani ya Trump, kwani kauli zake zinaeleza haya kwa uwazi. Hili ni hakika na linatarajiwa, kwa kuwa Mayahudi hawana uwezo wao wenyewe, wala hawana uwezo wa kupigana. Mwenyezi Mungu Mtukufu, Aliyetukuka, ni Mkweli zaidi:

[لَنْ يَضُرُّوكُمْ إِلَّا أَذًى وَإِنْ يُقَاتِلُوكُمْ يُوَلُّوكُمُ الْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يُنْصَرُونَ * ضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الذِّلَّةُ أَيْنَ مَا ثُقِفُوا إِلَّا بِحَبْلٍ مِنَ اللهِ وَحَبْلٍ مِنَ النَّاسِ وَبَاءُوا بِغَضَبٍ مِنَ اللهِ وَضُرِبَتْ عَلَيْهِمُ الْمَسْكَنَةُ]

“Maadui hawatakudhuruni ila ni maudhi tu. Na wakipigana nanyi watakupeni mgongo, na tena hawatanusuriwa. * Wamepigwa na udhalili popote wanapo kutikana, isipo kuwa wakishika kamba ya Mwenyezi Mungu na kamba ya watu. Na wakastahiki ghadhabu ya Mwenyezi Mungu, na wamepigwa na unyonge.” [Aal-i-Imran: 111-2]. Hivyo, tangu zama zao za mwanzo, wameikata kamba ya Mwenyezi Mungu baada ya zama za Mitume wao. Na ni vivyo hivyo katika zama za kisasa, kama vile Uingereza iliwatabanni tangu Vita vya Kwanza vya Dunia, kisha wakahamia kukumbatia Amerika baada ya Vita vya Pili vya Dunia. Vita vyao vyote vinazungumza juu ya hilo, kwa kuwa wako kwenye kamba ya watu…Usaidizi wa Trump kwao katika shambulizi lao dhidi ya Iran uko wazi kutokana na kauli za Trump hapo juu kwa yeyote aliye na moyo au anayesikiliza kwa makini.

2- Kisha lililo kubwa zaidi kuliko hili na la maafa na machungu zaidi ni kwamba ndege za Mayahudi zilivuka anga za tawala zinazotawala katika nchi za Kiislamu zinazozunguka umbile la Kiyahudi, ambazo ziliharibu na kuua huku zikiwa Iran na kisha zikaregea katika ardhi inayokaliwa kwa mabavu kwa usalama na amani. Hakuna hata risasi moja iliyorushwa kwa ndege hizi na watawala waliowazunguka huko Ash-Sham, Iraq, Misri, Uturuki na kutoka kila mahali… Hivyo, wanavuka mipaka na kushambulia wakiwa salama, wakienda na kurudi, na watawala katika nchi za Kiislamu wakitazama yale yaliyokuwa yakitendeka bila kuchukua hatua. Walisahau au kujifanya kusahau matokeo ya uhalifu wa kimya chao.

[سَيُصِيبُ الَّذِينَ أَجْرَمُوا صَغَارٌ عِنْدَ اللهِ وَعَذَابٌ شَدِيدٌ بِمَا كَانُوا يَمْكُرُونَ]

“Itawafikia hao walio kosa udhalili na adhabu kali kutoka kwa Mwenyezi Mungu kwa sababu ya vitimbi walivyo kuwa wakivifanya.” [Al-An’am: 124]. Ni dhambi kubwa kwamba ndege za Kiyahudi huvuka anga ya watawala vibaraka, kutekeleza mashambulizi yao na kurudi bila ya kutunguliwa na yeyote kati ya watawala hao.

3- Kila mwenye akili timamu anatambua kuwa njia bora ya kujilinda dhidi ya Mayahudi ni mashambulizi. Mayahudi wamekuwa wakitishia Iran kwa muda mrefu, haswa katika siku za hivi karibuni. Trump hata alidokeza na hata kutangaza kwamba Mayahudi watashambulia vituo vya nyuklia vya Iran. Hata hivyo, Iran haikuanzisha jibu la mashambulizi dhidi ya Mayahudi, katika kuilinda Iran, na kuepusha vitisho hivi kutoka kwa Marekani na Mayahudi. Hii inashangaza kwa kweli!! Iran ilikaa kimya hadi mitambo yake iliposhambuliwa na wanasayansi wake kuuawa, na ndipo ikaanza kujibu. Licha ya mashambulizi yote mfululizo, Trump anaendelea kutangaza, "Vivyo hivyo, tutakuwa na AMANI, hivi karibuni, kati ya Israel na Iran! Miito mingi na mikutano inafanyika sasa." (Sky News, 15/6/2025)! Tunatahadharisha dhidi ya vita hivi kuleta amani na umbile la Kiyahudi, bali, kama Mwenyezi Mungu alivyosema:

[فَإِمَّا تَثْقَفَنَّهُمْ فِي الْحَرْبِ فَشَرِّدْ بِهِمْ مَنْ خَلْفَهُمْ]

“Basi ukiwakuta vitani wakimbize walio nyuma yao ili wapate kukumbuka.” [Al-Anfal:57].

4- Lakini kinachovunja moyo kweli ni watawala Ruwaibidha (wajinga wasio na maana) katika nchi za Waislamu, hususan zile zinazolizunguka umbile la Kiyahudi linaloikalia kimabavu Palestina. Wanawazunguka, basi iweje wasione ndege za Kiyahudi zikipita juu ya vichwa vyao, zikipiga mabomu nchi za Kiislamu na kurudi salama bila hata risasi moja kufyatuliwa?! Badala yake, wao kana kwamba ni watu wasioegemea upande wowote wanaotazama yanayoendelea, kana kwamba wako katika nchi fulani ya mbali, si katika ardhi za Waislamu! Watawala hawa wako katika hali ya kuangamia na hilo halishangazi, kwani wako kwenye mvuto na wito wa nchi za kikoloni za makafiri hususan Amerika.

Wanasema wanachosema na kufanya wanachotaka. Wanahalalisha kutochukua hatua na kutukuza mipaka, na wakasahau au wanajifanya kusahau kuwa ardhi za Waislamu ni moja, sawa iwe ziko katika sehemu ya mbali zaidi ya dunia au iliyo karibu zaidi! Na kwamba amani ya Waumini ni moja, na vita vyao ni vimoja. Sio sawa zigawanyike kwa madhehebu yao ya Kiislamu, maadamu wao ni Waislamu, kwani wao ni Ummah mmoja:

[إِنَّ هَذِهِ أُمَّتُكُمْ أُمَّةً وَاحِدَةً وَأَنَا رَبُّكُمْ فَاعْبُدُونِ]

“Kwa hakika huu umma wenu ni umma mmoja, na Mimi ni Mola wenu Mlezi. Kwa hivyo niabuduni Mimi.” [Al-Anbya: 92].

Iweje ndege za adui ziruke juu ya anga ya watawala katika nchi za Waislamu na kuipiga mabomu nchi nyingine ya Kiislamu huku wao wakinyamaza kimya?! Mfano zaidi wa haya ni njia ya wale wanaotazama ndege za adui zikija na kuondoka kana kwamba haziegemei upande wowote au wako karibu na Mayahudi! Aidha, ijapokuwa watawala hawa wanasikia kauli ya Trump, sio vidokezo vyake, kwamba umbile la Kiyahudi linapigana kwa kamba (msaada) ya Amerika, amri zake, na silaha zake, lakini hakuna hata mmoja wao anayesubutu angalau kukata mahusiano na Amerika.

[أَلَا سَاءَ مَا يَحْكُمُونَ]

“Tazama uovu wa wanavyohukumu!” [An-Nahl: 59]

5- Pamoja na hayo yote, Ruwaibidha (watawala wasio na maana) hawa watatoweka na Dola ya Kiislamu, Khilafah Rashida, itaregea kuwa dola ya kwanza duniani, ikieneza kheri ndani yake, Mwenyezi Mungu akipenda. Kupigana na Mayahudi na kuondoa uvamizi wao kutatokea, Mwenyezi Mungu akipenda. Mkweli na Mwaminifu (saw) amesema katika Musnad Ahmad kutoka kwa Hudhayfah:

«...ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»

"...kisha kutakuwa na Khilafah kwa njia ya Utume." Kadhalika, Al-Bukhari amepokea kutoka kwa Abdullah ibn Umar, Mwenyezi Mungu awe radhi nao wote wawili, ambaye amesema: Nimemsikia Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) akisema: «تُقَاتِلُكُمْ الْيَهُودُ فَتُسَلَّطُونَ عَلَيْهِمْ..» Mayahudi watapigana nanyi. Basi mtawadhibiti juu yao” Imepokewa pia na Muslim kutoka kwa Ibn Umar, kutoka kwa Mtume (saw) ambaye amesema: «لَتُقَاتِلُنَّ الْيَهُودَ فَلَتَقْتُلُنَّهُمْ..» "Kwa yakini mtapigana na Mayahudi, na mutawaua." Kisha dunia itang'aa kwa ushindi wa Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hekima.

[إِنَّ فِي ذَلِكَ لَذِكْرَى لِمَنْ كَانَ لَهُ قَلْبٌ أَوْ أَلْقَى السَّمْعَ وَهُوَ شَهِيدٌ]

“Hakika katika hayo upo ukumbusho kwa mwenye moyo au akatega sikio naye yupo anashuhudia.” [Qaf: 37]

Kwa kumalizia, Hizb ut Tahrir, kiongozi asiyewadanganya watu wake, inakuombeni muiunge mkono na mufanye kazi nayo kuiregesha Khilafah Rashida kwa mara nyengine tena, ili Uislamu na watu wake uheshimiwe na ukafiri na watu wake wadhalilike, na huo ndio utakuwa ushindi mkubwa.

[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]

“Na siku hiyo Waumini watafurahi. Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum: 4-5]

H. 20 Dhu al-Hijjah 1446
M. : Jumatatu, 16 Juni 2025

Hizb-ut-Tahrir

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.