Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Trump, Msaidizi Mkuu wa Umbile la Kiyahudi katika Uhalifu wake wa Kinyama mjini Gaza na Palestina Yote, Anatoa Suluhisho la Maangamivu kwa Gaza, Hata Kulilazimisha, Juu ya Kundi la Watawala katika Nchi za Waislamu!!
(Imetafsiriwa)

Trump alisema katika chapisho kwenye jukwaa lake la Kijamii la Ukweli: “Ninafuraha kuripoti kwamba tuna mazungumzo yenye msukumo na yenye natija na Jumuiya ya Mashariki ya Kati kuhusu Gaza,” na kuongeza kuwa, “mazungumzo makali yamekuwa yakiendelea kwa siku nne, na yataendelea kwa muda mrefu iwezekanavyo ili kupata Makubaliano Yanayokamilishwa kwa Mafanikio.” (Truth Social; TRT Kiarabu, 27/9/2025)

Trump aliongoza mkutano uliojumuisha Saudi Arabia, Imarati, Qatar, Misri, Jordan, Uturuki, Indonesia na Pakistan kando ya mikutano ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, Jumanne, 23/9/2025, akiutaja kama: “moja ya mikutano muhimu zaidi”... kisha akawasilisha, au akalazimisha, kwao mpango wa nukta 21, maarufu zaidi kati yazo ni, “kuachiliwa huru kwa wafungwa wote wa Kiyahudi na Hamas, makubaliano ya kudumu ya kusitisha vita, kuondoka hatua kwa hatua kwa jeshi la Kiyahudi...” (Al Arabiya Net, 25/9/2025). Trump aliweka wazi lengo lake la kuwakusanya, ambalo lilikuwa ni kuwaachilia huru wafungwa wa Kiyahudi. Aliwahutubia, akisema: “serikali yake inataka kuregesha mateka 20 na miili 38 kutoka Gaza...” kisha akatoa masharti ya uondokaji wa hatua kwa hatua, neno lililosheheni kukomesha uondokaji huo, na hivyo umbile la Kiyahudi lingeendelea kudhibiti usitishaji mapigano! Pamoja na hayo yote, watawala wa ruwaibidha (wajinga wasio na maana) waliokusanyika walifurahishwa na Trump na mpango wake! Amiri wa Qatar, ambaye alishambuliwa na umbile la Kiyahudi, na bila shaka Mayahudi hawangefanya hivyo bila ya idhini kutoka kwa Trump, hata hivyo alisema: “Tunakutegemea wewe [Trump] na uongozi wako ... kumaliza vita hivi na kuwasaidia watu wa Gaza.” (Al Jazeera, 23/9/2025) Rais wa Uturuki Recep Tayyip Erdogan, ambaye alishiriki katika mkutano huo, pia alisema: “Mkutano ulikuwa ‘wenye matunda mengi’” (BBC News Arabic, 23/9/2025). Kauli hizi ndizo kauli sawia za watawala wengine.

[قَاتَلَهُمُ اللَّهُ أَنَّى يُؤْفَكُونَ]

“Mwenyezi Mungu awaangamize! Wanageuzwa namna gani hawa!” [At-Tawbah: 30]

Enyi Waislamu... Enyi Majeshi ya Waislamu:

Je, sio kilele cha usaliti na udhalilifu wa mwisho kumtegemea Trump kuiokoa Gaza kwa kukomesha vita huko, wakati yeye ndiye muungaji mkono mkuu wa hujma ya kikatili ya Kiyahudi dhidi ya Gaza!!?

[وَلَا تَرْكَنُوا إِلَى الَّذِينَ ظَلَمُوا فَتَمَسَّكُمُ النَّارُ وَمَا لَكُمْ مِنْ دُونِ اللَّهِ مِنْ أَوْلِيَاءَ ثُمَّ لَا تُنْصَرُونَ]

“Wala msiwategemee wanao dhulumu, usije ukakuguseni Moto. Wala nyinyi hamna walinzi badala ya Mwenyezi Mungu, wala tena hamtasaidiwa.” [Hud: 113]

Je, ushindi wa Gaza hauko katika majeshi ya Kiislamu kusonga na kupigana na wavamizi wa Kiyahudi wa Ardhi Iliyobarikiwa ambao hawawezi kupata ushindi na hawaongozwi kwenye njia?

[وَإِنْ يُقَاتِلُوكُمْ يُوَلُّوكُمُ الْأَدْبَارَ ثُمَّ لَا يُنْصَرُونَ]

“Na wakipigana nanyi watakupeni mgongo, na tena hawatanusuriwa.” [Aal-i-Imran: 111]

Je, majeshi ya watawala ambayo Trump amewakusanya katika baraza lake la mawaziri, au hata baadhi yao, hayatoshi kulisaga saga umbile la Kiyahudi na kuiregesha Palestina yote kwenye ardhi za Uislamu?

[قَاتِلُوهُمْ يُعَذِّبْهُمُ اللَّهُ بِأَيْدِيكُمْ وَيُخْزِهِمْ وَيَنْصُرْكُمْ عَلَيْهِمْ وَيَشْفِ صُدُورَ قَوْمٍ مُؤْمِنِينَ]

“Piganeni nao, Mwenyezi Mungu awaadhibu kwa mikono yenu, na awahizi na akunusuruni muwashinde, na avipoze vifua vya kaumu ya Waumini” [At-Tawbah: 14]

Enyi Waislamu:

Msiba wa Ummah uko kwa watawala wake. Tangu Khilafah ilipofutwa karibu miaka mia moja iliyopita, Waislamu wamekuwa hawana Khalifa wa kumgeukia na kupigana nyuma yake.  «وَإِنَّمَا الْإِمَامُ جُنَّةٌ يُقَاتَلُ مِنْ وَرَائِهِ وَيُتَّقَى بِهِ» “Hakika Imam ni ngao watu hupigana nyuma yake hujihami kwaye” (Imepokewa na Al-Muslim). Matukufu ya Waislamu yamekiukwa, ardhi zao zikatawaliwa na ukoloni, na Ruwaibidha (wasio na maana na wajinga) wakawatawala, bila kumfukuza adui wala kulinda hadhi ya Uislamu, mpaka hali ikafika mahali ambapo Ardhi Iliyobarikiwa ikakaliwa kimabavu na wale waliopata fedheha na taabu, na wakapata ghadhabu ya Mwenyezi Mungu!

Enyi Majeshi ya Ardhi za Waislamu:

Je, hakuna mwanamume mwenye busara miongoni mwenu ambaye damu yake inachemka katika mishipa yake anaposhuhudia jinai za umbile la Kiyahudi zilizoenea kote Gaza, likibomoa nyumba na kumwaga damu katika mauaji ya kikatili yanayowalenga wazee, watoto na wanawake? Je, hakuna mtu miongoni mwenu mwenye busara ambaye damu yake inachemka katika mishipa yake anapowaona watu wakihama kutoka sehemu moja hadi nyingine na ndege za Kiyahudi zikiwashambulia kwa mabomu katika harakati zao na kuhama kwao?

Je, hakuna mtu miongoni mwenu mwenye akili anayetambua kwamba kuwatii watawala kwa kunyenyekea uvamizi wa Kiyahudi na kutoujibu ni fedheha katika maisha haya ya dunia na adhabu chungu ya Akhera? Hata wale wanaowatii katika kumuasi Mwenyezi Mungu watawakana Siku ya Kiyama, na atajuta kuwafuata katika kumuasi Mwenyezi Mungu, lakini hakuna wakati wa majuto.

[إِذْ تَبَرَّأَ الَّذِينَ اتُّبِعُوا مِنَ الَّذِينَ اتَّبَعُوا وَرَأَوُا الْعَذَابَ وَتَقَطَّعَتْ بِهِمُ الْأَسْبَابُ * وَقَالَ الَّذِينَ اتَّبَعُوا لَوْ أَنَّ لَنَا كَرَّةً فَنَتَبَرَّأَ مِنْهُمْ كَمَا تَبَرَّءُوا مِنَّا كَذَلِكَ يُرِيهِمُ اللَّهُ أَعْمَالَهُمْ حَسَرَاتٍ عَلَيْهِمْ وَمَا هُمْ بِخَارِجِينَ مِنَ النَّارِ]

“Walio fuatwa watakapo wakataa wale walio wafuata, na hali ya kuwa wamekwisha iona adhabu; na yatakatika mafungamano yao * Na watasema wale walio fuata: Laiti tungeweza kurudi tukawakataa wao kama wanavyo tukataa sisi! Hivi ndivyo Mwenyezi Mungu atakavyo waonyesha vitendo vyao kuwa majuto yao; wala hawatakuwa wenye kutoka Motoni.” [Al-Baqarah: 166-167]

Je, hakuna mtu miongoni mwenu mwenye hekima ambaye anatamani mojawapo ya mambo mawili ya kheri, kuwaongoza askari wa Uislamu na kuikomboa Gaza, Kibla cha kwanza kati ya Viblah viwili na msikiti wa tatu mtakatifu kati ya miwili mitakatifu, na kupiga Takbira za ushindi zisikike pembeni mwake kama alivyofanya al-Faruq wakati wa ufunguzi, na Swalahudin wakati wa kukombolewa kwa Bait al-Maqdis na Abdul Hamid wakati wa ulinzi wake wa Ardhi Iliyobarikiwa kutokana na uovu wa Mayahudi... na hivyo kutimiza bishara njema ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw): «لَتُقَاتِلُنَّ الْيَهُودَ فَلَتَقْتُلُنَّهُمْ...» “Kwa yakini mtapigana na Mayahudi na kwa yakini mtawauwa...” (Imesimuliwa na Muslim katika Sahih yake)?

Enyi Waislamu:

Tumehakikishiwa ushindi (nasr) wa Mwenyezi Mungu, izza ya Uislamu na Waislamu, kuregea kwa Khilafah Rashida, kupigana na kuwauwa Mayahudi, na kufunguliwa kwa Roma sawa na Konstantinopoli ilivyokombolewa, na kuifanya Istanbul kuwa makaazi ya Uislamu. Haya yote ni kwa mujibu wa ahadi ya Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, na bishara njema ya Mtume wake (saw) na yatatokea, Mwenyezi Mungu akipenda. Hata hivyo, sheria ya Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Mwenye hekima, haitaki Malaika washuke kutoka mbinguni ili kutusimamishia Khilafah na kutimiza ahadi ya Mwenyezi Mungu, Mwenye nguvu, Aliyetukuka, na bishara njema ya Mtume Wake (saw) huku tukiwa tumekaa bila kutetereka. Badala yake, malaika hushuka juu yetu ili kutusaidia tunapofanya kazi kwa umakini, bidii, ukweli na ikhlasi. Hapo ndipo Mwenyezi Mungu atatupa nusra na ushindi katika ulimwengu huu pamoja na akhera, na huko ndiko kufuzu kukubwa.

[وَيَوْمَئِذٍ يَفْرَحُ الْمُؤْمِنُونَ * بِنَصْرِ اللَّهِ يَنْصُرُ مَنْ يَشَاءُ وَهُوَ الْعَزِيزُ الرَّحِيمُ]

“Na siku hiyo Waumini watafurahi * Kwa nusura ya Mwenyezi Mungu humnusuru amtakaye. Naye ndiye Mwenye nguvu Mwenye kurehemu.” [Ar-Rum: 4-5]

Enyi Waislamu... Enyi Majeshi katika Ardhi za Waislamu:

Hizb ut Tahrir, kiongozi asiyewadanganya watu wake, inakuhutubieni na kukulinganieni kwa maneno ya Mwenyezi Mungu (swt):

[هَذَا بَلَاغٌ لِلنَّاسِ وَلِيُنْذَرُوا بِهِ وَلِيَعْلَمُوا أَنَّمَا هُوَ إِلَهٌ وَاحِدٌ وَلِيَذَّكَّرَ أُولُو الْأَلْبَابِ]

“Hili ni Tangazo liwafikie watu, liwaonye, na wapate kujua kuwa hakika Yeye ni Mungu Mmoja, na wapate kukumbuka wenye akili.” [Ibrahim: 52].

H. 5 Rabi' II 1447
M. : Jumamosi, 27 Septemba 2025

Hizb-ut-Tahrir

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.