Ualishi jumla kutoka kwa dada mheshimiwa Dkt Nasreen Nawaz / Mkurugenzi wa Kitengo cha Wanawake katika Afisi ya Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir kuhudhuria kongamano la Wanawake nchini Denmark, ambalo litafanyika mnamo siku ya Jumapili 19/09/2021 M chini ya anwani:
Kwa Mnasaba wa Kumbukumbu ya Miaka Ishirini ya Matukio ya 11 Septemba na Amerika Kinara wa Ukafiri kuanzisha Vita dhidi ya kuchomoza kwa Uislamu chini ya lakabu (Vita dhidi ya Ugaidi).
Miaka ishirini imepita tangu Amerika itangaze kile ilichokiita "Vita dhidi ya Ugaidi" kufuatia mashambulizi ya Septemba 11 kwenye minara ya jumba la Kituo cha Biashara cha Ulimwengu jijini New York mnamo 2001, baada ya hapo Amerika iliivamia Afghanistan na Iraq.
Taliban wametangaza kuwa wanajaribu kuunda serikali mpya nchini Afghanistan – serikali ambayo inataka mahusiano mazuri ya kidiplomasia yaliojengwa juu ya ‘kuheshimiana’ na Amerika na sehemu nyengine za dunia.
Je, mwaweza kutuwekea wazi kuhusu rai ya Abu Hanifah na Sufyan al-Thawri na wengineo, kwamba hapana Riba katika Dar ul-Kufr. wakitolea dalili hadith isemayo: “Hapana Riba katika Dar ul-Kufr”.