Afisi ya Habari
Australia
| H. 3 Rajab 1447 | Na: 07 / 1447 H |
| M. Jumanne, 23 Disemba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Tishio la Kupiga Marufuku Hizb ut Tahrir nchini Australia
(Imetafsiriwa)
Kabla ya waathiriwa wa janga la Bondi hata kuzikwa, watetezi wanaounga mkono Uzayuni katika nchi hii walikuwa tayari wamekubaliana kuhusu simulizi yao na kuchochea orodha yao ya madai ya umma. Uchunguzi ndio umeanza tu, lakini watetezi wanaounga mkono Uzayuni katika nchi hii, wakichukua maelekezo kutoka kwa mhalifu wa kivita Netanyahu, wanasisitiza kwamba kipindi hiki chote kinaweza kuelezewa pekee kupitia jicho la chuki dhidi ya Mayahudi.
Watetezi wanaounga mkono Uzayuni walikwenda mbali zaidi. Tatizo si chuki yoyote tu kwa Mayahudi, bali aina yake mbaya inayoonekana kuwa imejikita katika Uislamu ‘wenye msimamo mkali’. Upanuzi wa mantiki hii ya uongo ni kugawanya lawama ya Bondi sio tu kwa washambuliaji, bali jamii nzima ya Waislamu kama msingi wa kimaumbile wa hii ‘misimamo mikali’ unayodaiwa. Sote sasa ni washukiwa isipokuwa tu tukikataa waziwazi ‘misimamo mikali’ kama hiyo, ambapo kwa watetezi wanaounga mkono Uzayuni, ni ishara tu ya kukubali mauaji ya halaiki na haki ya umbile vamizi ya kuyatekeleza.
Kama tulivyoona katika ‘wimbi’ bandia la mashambulizi ya chuki dhidi ya Mayahudi la msimu wa joto uliopita, watetezi wanaounga mkono Uzayuni katika nchi hii wanaitaka Australia ibadilishe mifumo yake ya kisiasa na kisheria ili kuutenga uhalifu wa Kizayuni. Lengo ni kunyamazisha uanaharakati unaounga mkono Palestina kwa jumla, na hasa uanaharakati unaozingatia Ummah. Ndoto ya Wazayuni ni kuua upinzani wowote dhidi yake Mashariki pamoja na Magharibi.
Juhudi za kupiga marufuku maandamano, nembo na hata kauli mbiu tayari zimeanza. Waziri Mkuu, chini ya shinikizo kubwa kutoka kwa umbile la Kizayuni na watu wake wa chini katika nchi hii, alihisi kulazimika kujibu kwa kiasi fulani. Kwa njia ambayo jamii ya Kiislamu imezoea, Waziri Mkuu aliitoa jamii hiyo kama kondoo wa kafara. Akikusudia Uislamu ‘wenye msimamo mkali’, wahubiri ‘wenye msimamo mkali’, kauli za chuki na viwanda vya kutengeneza chuki vilianza kupamba kauli na taarifa zake.
Mnamo tarehe 18 Disemba 2025, Waziri Mkuu alitangaza kwamba uhai wake wa kisiasa utakuwa gharama ya ubwana wa Australia, akikubali matakwa ya Wazayuni na kutangaza mpango wake wa mambo matano wa kupambana na chuki dhidi ya Mayahudi. Mojawapo ya mambo hayo ilikuwa ni kuharamisha harakati za Kiislamu nchini Palestina, kutangaza nia ya kuunda “utaratibu wa kuorodhesha mashirika ambayo viongozi wake wanashiriki katika hotuba za chuki zinazochochea vurugu au chuki za ubaguzi wa rangi.”
Mnamo tarehe 22 Disemba 2025, Waziri wa Mambo ya Ndani alipanua tangazo hili kwa kutangaza nia ya Australia ya kuunda mfumo mpya wa kisheria ambao ungetimiza kusudi la kuharamisha upinzani wa Waislamu, ukianzia na Hizb ut Tahrir. Alisema: “Mashirika (haya) kwa muda mrefu yameweza kuchukua chuki moja kwa moja bila kutumia maneno vurugu na kuepuka orodha yoyote ya kigaidi. Tutaanzisha aina mpya ya uorodheshaji kwa wale ambao hawafikii mashirika ya kigaidi – ya kuweza kupendekeza mashirika ... Tabia zao zinahitaji kuwa zisizokubalika, tabia zao zinahitaji kuwa kinyume cha sheria, tabia zao zinahitaji kuwa za kutosha ili tuweze kupendekeza shirika hilo na kupiga marufuku shughuli zao nchini Australia.”
Kwa maana nyengine, mithili ya juhudi zote za wanaharakati, kila kitu Hizb ut Tahrir inachosema au kufanya ni halali kabisa nchini humu. Lakini Wazayuni hawatupendi, na wamefanikiwa kuzishawishi dola za serikali za kifederali kwa miaka mingi kutupiga marufuku, na sasa wanaona katika Bondi fursa ya kipekee ya kuzima harakati za kuunga mkono Wapalestina katika jamii ya Waislamu.
Kuna mengi yanayohitaji kusemwa kuhusu pendekezo la serikali, na mengi yatasemwa katika siku zijazo, lakini mara moja, tunataka kusisitiza mambo yafuatayo:
1. Mpango wa kupiga marufuku Hizb ut Tahrir nchini Australia unaweza kutokea tu kupitia kuanzishwa kwa mfumo wa kisheria wa ngazi mbili. Waziri Mkuu ameutaja, na Waziri wake wa Mambo ya Ndani alisema waziwazi, kwamba licha ya kutokuwa na msingi wa kisheria wa kupiga marufuku Hizb ut Tahrir, Australia sasa itatafuta kuunda mfumo mpya kabisa wa kisheria unaolenga jamii ya Waislamu waziwazi.
2. Juhudi za kuipiga marufuku Hizb ut Tahrir ni sehemu ya madai mapana ya Wazayuni ya kuharamisha harakati zote za kuunga mkono Wapalestina. Kila mtu ni mlengwa.
3. Kesi ya serikali ya kupiga marufuku Hizb ut Tahrir nchini Australia inategemea uongo na mila za ubaguzi wa rangi na chuki dhidi ya Uislamu ambazo zinapaswa kuwakera watu wote wenye dhamiri.
Tutakuwa na mengi zaidi ya kusema kuhusu haya yote katika taarifa zijazo.
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Australia
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Australia |
Address & Website Tel: 0438 000 465 www.hizb-australia.org |
E-Mail: media@hizb-australia.org |