Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Denmark

H.  4 Jumada II 1441 Na: 02 / 1441 H
M.  Jumatano, 29 Januari 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Maoni ya Waziri Mkuu wa Denmark Juu ya Kupinga Uyahudi Yanaonyesha Chuki Dhidi ya Uislamu

Siku chache zilizopita, Waziri Mkuu wa Denmark, Mette Frederiksen, alikuwa kwenye ziara rasmi katika Palestina iliyo vamiwa. Alikutana na Rais wa umbile la Kiyahudi Reuven Rivlin katika Jerusalem iliyo vamiwa na zaidi ya hayo akashiriki katika ukumbusho wa miaka 75 ya ukombozi wa Auschwitz.

Kuwakumbuka wahasiriwa wa mauwaji ya halaiki katika dola, ambayo ilijengwa juu ya mauwaji ya halaiki yaliyo tekelezwa dhidi ya wenyeji wa Palestina, sio unafiki tu. Ni kuwakejeli wahasiriwa. Ubaya wa fedheha hiyo unazidishwa na ukweli kuwa wahalifu wa kivita kama Benjamin Netanyahu, ambaye anahusika na mauaji ya maelfu ya wanawake wasio na hatia, wazee na watoto ndani ya Gaza, alitoa hotuba katika ukumbusho huo.

Mette Frederiksen alichagua kabla ya kuondoka kwake kuwatuhumu Waislamu nchini Denmark kwa kuwa wanawapinga Mayahudi. Alidai kuwa “Uhamiaji” kutoka nchi fulani umechangia kuongezeka kwa kupinga mayahudi nchini Denmark. Akimaanisha wazi nchi za Waislamu. Ni upuuzi kuwa kitu kama chuki dhidi ya mayahudi, ambacho kina mizizi ya kina barani Uropa, kuonyeshwa kama ndio hali ya Waislamu. Haswa ukizingatia kuwa Neo-Nazis ambao waliharibu mawe ya kaburi la Mayahudi katika mji wa Randers walikuwa wa kabila la Danes. Hii pia ilikuwa ndio hali kwa wale ambao hivi karibuni waliweka vibandiko vya nyota za manjano kwenye masanduku ya barua za Mayahudi wa Denmark.

Nchi hizo, ambazo Waislamu wamehamia zina historia tofauti kabisa linapokuja suala la kupinga Uyahudi. Wakati Wayahudi walipo kimbia mateso mabaya ya Ulaya, kama vile Uchunguzi wa Kihispania, hawakupata sehemu ya kuwakaribisha na kuwapokea isipokuwa katika ardhi za Waislamu, ambazo zilitawaliwa na Uislamu wakati huo.

Chuki dhidi ya Mayahudi imekuwepo nchini Denmark kwa karne nyingi. Katika mwaka wa 1819, mateso ya Mayahudi yalikuwa makubwa sana hadi wanajeshi waliitwa huko Copenhagen na mji huo uliwekwa katika hali ya hatari. Magazeti makubwa ya Kidenmark kama Politiken, Jyllands Posten, na Berlingske yalikuwa na bidii sana ya kueneza hisia ya kupinga Uyahudi katika karne ya 20. Kupinga Uyahudi ilikuwa kawaida. Kama chuki dhidi ya Uislamu ni kawaida leo hii. Pindi historia nyeusi ya Ulaya ya kupinga Uyahudi inapo onyeshwa Waislamu huwa sio kwamba ni mambo yasiyo kuwa ya kweli na Ujinga wa kihistoria. Ni hadaifu.

Kama sehemu ya propaganda hii, Waziri Mkuu anataka kuwaonyesha Waislamu wanao ukashifu uvamizi wa Wazayuni kama watu walio dhidi ya Uyahudi kwa kutumia ufafanuzi maalum, ambao utamnyanyapaa yeyote ambaye anaye ikashifu dola itwayo “Israeli”. Mwito wa Waislamu wa kukombolewa Palestina, hata hivyo, sio mwito wa kuwapiga vita Mayahudi wote. Ni mwito wa kukomesha uvamizi haramu wa “Israeli”. Haki ya Waislamu ya kupinga Uvamizi katika Palestina yote kwa nguvu za kijeshi sio dhaifu zaidi ya ule upinzani wa Denmark wakati walipo pigana na Wajerumani katika miaka ya 1940.

Katika muangaza huu uamuzi wa Mahakama ya kitaifa dhidi ya Monzer Abdullah lazima uzingatiwe kama uamuzi wa kisiasa, ambao unaitia hatiani taarifa yoyote muhimu dhidi ya “Israeli”. Alihukumiwa kwa sababu ya hotuba ya Ijumaa, ambayo ilikuwa inahusu ukatili wa wa uvamizi “Israeli” kwa Palestina. Hotuba hiyo haikuhusu Mayahudi kwa ujumla. Katika mazungumzo hayo ilitajwa kuwa kuuondoa uvamizi huo inaweza kutokea pekee kupitia shambulio la kijeshi dhidi ya uvamizi huo. Huku sio kutangaza vita dhidi ya Mayahudi. Ni, kwa upande mwengine, mtazamo sahihi wa Kiislamu dhidi ya uvamizi wowote wa kijeshi, iwe ni Palestina, Kashmir au Afghanistan. Kupinga Uyahudi kwa muda mrefu kumekuwa ni chombo cha kisiasa cha kunyamazisha sauti zenye kukosoa dhidi ya uvamizi wa Palestina. Waislamu hawakubali na hawatokubali hili. Haijalishi ni maamuzi mangapi ya kisiasa yatapitishwa.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
Denmark

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Denmark
Address & Website
Tel: 

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.