Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Denmark

H.  23 Jumada I 1441 Na: 01 / 1441 H
M.  Jumamosi, 18 Januari 2020

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Mipango Ijayo ya serikali ya Denmark inayo husu kuondolewa kwa lazima kwa Watoto kutoka kwa Wazazi wao ni ushahidi wa mtazamo wake mbovu juu ya wanadamu na ni chuki kwa Waislamu

Kituo cha Televisheni ya Denmark TV2 kilichapisha makala mnamo Januari 15 kwa kichwa: “Serikali inataka kuzilazimisha manispaa kuwaondoa watoto wanaokulia katika mazingira ya misimamo mikali.” Makala hayo yalielezea vipi serikali ya Denmark inavyo taka kuunda tume ya “kutunga kanuni ambazo zinalazimisha manispaa kumweka mtoto au kijana mdogo nje ya nyumba yao ikiwa itakadiriwa kuwa vyenginevyo watakua katika mazingira ya misimamo mikali.”

Hata ingawa mpango huu muovu unaanzishwa chini ya pazia ya upanuzi wa sheria ya sasa dhidi ya wapiganaji wa kigeni, huwasilishwa kwa misemo ya jumla kama vile “mazingira ya misimamo mikali”, ambayo inafungua mlango ili iweze kutumiwa dhidi ya familia yoyote ya Waislamu inayo pinga maadili huru ya kisekula. Maneno kama “misimamo mikali” na “uvukaji mipaka” yametumika kwa njia ya kupitiliza na wanasiasa pindi wanapo zungumza kuhusu Uislamu na Waislamu kwa jumla.

Hili linajiri wiki chache tu baada ya Waziri Mkuu, Mette Frederiksen, kutoa hotuba yake ya Mwaka Mpya ambayo ilifasiriwa na wachambuzi kadhaa kama mwito wa kulazimisha kuondolewa kwa watoto zaidi wa Kiislamu.

Lars Trier Mogensen, mchambuzi wa kisiasa, ametoa maoni kwa hotuba yake hiyo ya Mwaka Mpya akisema: “Haiwezekani kukosewa na maneno yake. Njia ngumu dhidi ya wazazi wa watoto waliowekwa kwa kweli itakuwa ni upanuzi wa ule unaoitwa Mswada Ghetto kwa sababu watoto wengi ambao katika siku za usoni watatolewa kilazima na kupeanwa kwa ulezi watakuwa ni watoto kutoka kwa familia za wageni na wakimbizi. Tayari amefungua vita vipya vya kijamii na utamaduni ambavyo Wasoshalisti wa kidemokrasia kwa mara ya kwanza wako katika nafasi ya mashambulizi.

Taarifa hizi ni ushahidi wa mtazamo mbovu kwa wanadamu na chuki kwa Waislamu. Kuiondoa haki ya mtoto kuwa na mzazi wake na kinyume chake kunaweza kulinganishwa na kumuua mtu inapokuja kumdhuru mwanadamu mwengine. Pia imeonekana hapo awali katika historia jinsi gani Denmark na nchi nyengine za Ulaya zimefanya hili kwa jina la kustaarabisha watu washamba kwa fikra tofauti. Mtazamo wao huu mbovu kwa wanadamu hakika bado hauja badilika.

Hata ingawa matatizo mkubwa kama vile unyanyasaji wa kijinsia, pombe na vurugu kupita kiasi zimeenea kati ya familia nyinyi za Kideni, serikali imechagua kutozingatia umakini wake hapa. Si katika familia hizi ambazo Waziri Mkuu huyu anaamini “uondoaji kwa kutumia nguvu chache mno” unafanywa. Mnamo mwaka wa 2018, manispaa zilitekeleza uondoaji wa watoto 3871 nje ya nyumba zao. Katika visa hivi, mamlaka hizo zilitoa mathibitisho 7354 kuelezea uondoaji huu. Asilimia 7 pekee ya mathibitisho haya yalikuwa juu ya unyanyasaji wa wazazi na asilimia 6 pekee yalikuwa juu ya unyanyasaji wa kimwili, unyanyasaji wa kijinsia au aina nyengine za unyanyasaji.

Pia inajulikana vizuri kuwa ushughulikiaji wa kesi wakati inapokuja kuondolewa kwa lazima kwa watoto zimenakiliwa zikiwa na dosari. Uchunguzi wa ndani uliofanywa na Manispaa ya Frederiksberg umebaini dosari katika visa vyote. Lakini, serikali haitaki kurekebisha hili kabla Manispaa kulazimika kuwaondowa watoto kutoka kwa “wazazi wao wenye misimamo mikali”.

Wanazungumza kuhusu kuondolewa kwa lazima kwa mtindo baridi kiasi kwamba mtu angelifikiria walikuwa wanazungumza kuhusu kuondolewa kwa watoto wa wanyama kutoka kwa mama zao katika mbuga ya wamyama. Waziri Mkuu huyo wa Denmark anaonekana kuota kuhusu kukamilisha hali kama ile ya nchini China ambapo mamlaka huko Xinjiang zinaweza kuwaondoa watoto wa Kiislamu endapo maafisa wa China watatathmini kuwa familia hiyo sio ya Kichina sawasawa na imeonyesha dalili za msimamo mkali.

Tunatoa wito kwa Waislamu wote kupinga mipango hii ya kibaguzi dhidi ya jamii ya Waislamu. Tumeshuhudia hapo awali jinsi gani sheria za kupinga Uislamu zinatoa njia kwa sheria kali zaidi za kupinga Uislamu. Kuna uwezekano mkubwa kwamba kondolewa huku kwa watoto kwa lazima kunaweza kutumika katika siku za usoni kama ala ya vitisho dhidi ya Waislamu ikiwa hawatakubali kuoanishwa. Kama tunavyoona sasa huko nchini China.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Denmark

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Denmark
Address & Website
Tel: 

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.