Afisi ya Habari
Wilayah Jordan
| H. 21 Jumada II 1447 | Na: 1447 / 12 |
| M. Ijumaa, 12 Disemba 2025 |
Tanzia ya Mbebaji Ulinganizi Miongoni mwa Mashababu wa Hizb ut Tahrir
Mwalimu Ustadh Ahmad Muhammad Al-Saharin (Abu Khalid)
﴿مِّنَ الْمُؤْمِنِينَ رِجَالٌ صَدَقُواْ مَا عَاهَدُواْ اللَّهَ عَلَيْهِ فَمِنْهُم مَّن قَضَى نَحْبَهُ
وَمِنْهُم مَّن يَنتَظِرُ وَمَا بَدَّلُواْ تَبْدِيلاً﴾
“Miongoni mwa Waumini wapo watu walio timiza waliyo ahidiana na Mwenyezi Mungu. Baadhi yao wamekwisha kufa, na baadhi wanangojea, wala hawakubadilisha (ahadi) hata kidogo.” [Al-Ahzab: 23]
(Imetafsiriwa)
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir/Wilayah Jordan inaomboleza kifo cha mwalimu mtukufu, Ustadh Ahmad Muhammad Al-Saharin (Abu Khalid), mwanachama wa Hizb ut Tahrir, aliyefariki Jumatano, 10 Disemba 2025, akiwa na umri wa miaka 79. Alikuwa miongoni mwa wabebaji da’wah wa muda mrefu na anayejulikana sana huko Tafila.
Ustadh Ahmad Al-Saharin alijitolea maisha yake kubeba ulinganizi wa Uislamu, msema kweli, mlezi, msimamizi, na mfano wa kuigwa. Alikuwa mbebabji jasiri na asiyeyumba wa da’wah, asiyezuiwa na kikwazo chochote. Alikuwa na nafasi maalum katika nyoyo za watu na alitajwa kwa uzuri katika ndimi zao, akitimiza majukumu yake kwa uaminifu na ikhlasi. Tunamhisabu, na Mwenyezi Mungu ndiye bora wa kuhisabu, kwamba alijitolea kwa Uislamu katika aqida yake, hukmu zake, na da’wah yake kwa Mwenyezi Mungu kwa njia inayomridhisha, Mwenyezi Mungu Aliyetukuka.
Aliteseka kutokana na ugonjwa mwishoni mwa maisha yake, lakini alikuwa ameridhika, mvumilivu, na imara hadi Mwenyezi Mungu alipomchukua. Tunamuomba Mwenyezi Mungu amsamehe, amrehemu, na amfanye mmoja wa wakaazi wa Pepo ya Juu Zaidi pamoja na manabii, wakweli, mashahidi, na wema, na hao ni maswahaba wazuri walioje. Tunamuomba Mwenyezi Mungu awape familia yake uvumilivu na uthabiti na awalipe ujira mkubwa kwa msiba wao. Na hatusemi ila tu yale yanayomridhisha Mwenyezi Mungu:
﴿إِنَّا للهِ وَإِنَّا إِلَيْهِ رَاجِعُونَ﴾
“Hakika sisi ni wa Mwenyezi Mungu, na kwake Yeye hakika tutarejea.” [Baqara: 156]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Jordan

Kalima ya Ujumbe wa Hizb ut Tahrir Iliyowasilishwa na Ustadh Bilal Al-Qasrawi (Abu Ibrahim)
Katika Kikao cha Kutoa Rambirambi za Marehemu Mwalimu Ahmed Mohammed Al-Saharin (Abu Khalid), Mwenyezi Mungu amrehemu
Ijumaa, 21 Jumada al-Awwal 1447 H sawia na 12 Disemba 2025

| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Jordan |
Address & Website Tel: http://www.hizb-jordan.org/ |
E-Mail: info@hizb-jordan.org |