Afisi ya Habari
Malaysia
| H. 3 Jumada I 1447 | Na: HTM 1447 / 02 |
| M. Jumamosi, 25 Oktoba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Kumwalika Adui wa Mwenyezi Mungu, Mtume Wake, na Waumini Ni Sawa na Kualika Ghadhabu ya Mwenyezi Mungu na Msiba: Mche Mwenyezi Mungu, Ewe Waziri Mkuu wa Malaysia!
(Imetafsiriwa)
Hizb ut Tahrir / Malaysia inalaani vikali mwaliko uliotolewa na Waziri Mkuu wa Malaysia, Dato’ Seri Anwar Ibrahim, kwa Rais wa Marekani, Donald Trump — ambaye mikono yake imejaa damu ya Waislamu wa Gaza — kuja nchini Malaysia kuhudhuria Mkutano wa 47 wa ASEAN jijini Kuala Lumpur. Mwaliko huu si tu ishara ya aibu ya kidiplomasia isiyo na msimamo wa kimaadili; ni aibu kubwa kwa hadhi ya Ummah huu, usaliti unaojeruhi dhamiri ya kila Muislamu ambaye bado ana heshima karibu na moyo wake, hasa zaidi watu wa Palestina.
Mtu anayedai kutetea kadhia ya Palestina anawezaje kumwalika muuaji wa Wapalestina na mharibifu wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina katika nchi ya Waislamu? Hadhi ya Muislamu iko wapi wakati adui wa Mwenyezi Mungu (swt), adui wa Mtume Wake (saw) na adui wa Waumini anakaribishwa nchini mwetu kwa heshima za sherehe zinazotolewa kwa mgeni wa serikali? Ni chembe gani ya thamani ambayo adui wa Uislamu asiye na ubinadamu anayo ambayo inastahili zulia jekundu na fahari rasmi? Ni nani, miongoni mwa adui aliye hai wa Mwenyezi Mungu leo, anayeweza kuchukiza zaidi machoni pa Mwenyezi Mungu kuliko yule aliyehusika na vifo vya Waislamu zaidi ya 67,000 na uharibifu wa ardhi takatifu ya Palestina?
Trump sio tu Kafiri mwenye kiburi; kupitia mikono yake, damu ya Waislamu wasio na hatia imemwagika kwenye ardhi ya Gaza, na anajivunia sana hilo. Kupitia maneno yake, al-Quds – Kibla cha kwanza cha Ummah huu – imetambuliwa kama mji mkuu wa umbile haramu la Kiyahudi. Kupitia saini yake, alipitisha kile kinachoitwa “Dili ya Karne,” mpango ulionyima haki za watu wa Palestina na kwa ufanisi akatafuta kuifuta Palestina kwenye ramani ya dunia. Na sasa, kwa mara nyengine tena, anatangaza kile kinachoitwa “Mpango wa Amani” juu ya ardhi ambayo hana madai halali kabisa. Je, inafaa mtu kama huyo aalikwe na kuheshimiwa katika nchi ambayo watu wake wanashuhudia kwamba hakuna mola wa haki ila Mwenyezi Mungu na kwamba Muhammad ni Mtume Wake?
Waziri Mkuu wa Malaysia anatafuta kuficha fedheha hii ndani ya vazi la uenyekiti wa ASEAN. Tunauliza waziwazi: je, kuna wajibu ulio ndani ya dori ya mwenyekiti wa ASEAN kutoa mwaliko kama huo? Kinyume chake, kukataa kumwalika mhalifu Trump kungeonyesha masalio ya heshima na ujasiri. Vyovyote vile nyudhuru zinazotolewa, haziwezi kuficha ukweli kwamba kitendo hiki kinatokana na utumwa na hofu ya Amerika. Ilhali, unyenyekevu na heshima ya kweli ni ya Mwenyezi Mungu (swt) pekee, sio kwa maadui zake.
Cha aibu zaidi ni hoja kwamba kwa uwepo wa Trump, ujumbe kuhusu Palestina unaweza kufikishwa moja kwa moja kwake. Pendekezo hilo ni la kejeli sana: je, mbwa mwitu anayekula kundi la kondoo atatii ushauri kuhusu huruma kwa kondoo? Ni upuuzi ulioje! Tunawezaje kutafuta azimio kutoka kwa mtendaji yule yule ambaye ameiangamiza Palestina? Tunawezaje kutoa sauti, au hata kukubali suluhisho la tatizo letu, kutoka kwa adui yetu mwenyewe? Jua hili, ewe Waziri Mkuu wa Malaysia, azimio la kadhia ya Palestina halitatoka kwa Donald Trump, na kamwe halitatoka. Azimio liko mikononi mwako, na mikononi mwa watawala wote wa Waislamu – kwamba wewe na wenzako wote muhamasishe majeshi yenu ili kuliangamiza umbile la Kiyahudi kutoka kwenye mzizi wake. La kusikitisha, hamfanyi hivyo, na “mnasalimisha” shingo za Wapalestina ili wachinjwe na Trump badala yake!
Hakika, kumwalika Trump nchini humu hakuhatarishi tu kukaribisha ghadhabu ya Mwenyezi Mungu (swt), bali pia kunahatarisha ubwana wa taifa wenyewe. Mara tu atakapowasili, hatutatekeleza tena mamlaka kamili juu ya vipengee vya vyombo vyetu wenyewe vya usalama vya serikali: polisi, jeshi, mamlaka ya uhamiaji na taasisi nzima ya usalama itahamishwa ili kuhakikisha ulinzi wa mtu anayehusika na vifo vya zaidi ya Waislamu 67,000 – ili kuzuia hata chembe ndogo ya vumbi isimguse. Hii, ni fedheha kubwa: muuaji wa watoto wachanga, watoto wadogo, wanawake na wazee anatendewa zaidi ya yale yanayotendewa hata mfalme. Yeye (swt) asema:
[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُوا لَا تَتَّخِذُوا عَدُوِّي وَعَدُوَّكُمْ أَوْلِيَاءَ]
“Enyi mlio amini! Msiwafanye adui zangu na adui zenu kuwa marafiki.” [Al-Mumtahanah (60):1].
Ewe Waziri Mkuu wa Malaysia! Fahamu kwamba kwa kumwalika Trump; kwa kukaa katika baraza na kupiga picha naye, hutapata heshima yoyote, hata ya uzito wa chembe ya atomu! Heshima yote ni ya Mwenyezi Mungu pekee. Maadui zake na wale wanaotafuta upendeleo wao watapata fedheha tu. Yeyote anayetaka kuongeza sifa yake machoni pa maadui wa Mwenyezi Mungu anapaswa kujua kwamba Waumini wa kweli watawaona kuwa wa kudharauliwa, na mbele ya Mwenyezi Mungu, fedheha yao ni kubwa zaidi.
[أَيَبْتَغُونَ عِنْدَهُمُ الْعِزَّةَ فَإِنَّ الْعِزَّةَ لِلَّهِ جَمِيعًا]
“Je! Wanataka wapate kwao utukufu? Basi hakika utukufu wote ni wa Mwenyezi Mungu.” [An-Nisa' (4): 139].
Zaidi ya hayo, hakuna tofauti ya kivitendo kati ya kumwalika Trump na kumwalika Netanyahu nchini humu kwani wote wawili ni Kafir Harbī Fi‘lan (Makafiri wa kivita kivitendo), adui wa Uislamu, wa Mwenyezi Mungu, wa Mtume Wake, na wa Waumini. Wote wawili ni wahalifu wachafu, lakini Trump anajiona ametukuka kwa sababu watawala wa Waislamu wamechagua kumtukuza; watawala wa Waislamu wanaomtukuza hivyo ni wapumbavu kiasi gani. Hizb ut Tahrir inafanya kazi ya kusimamisha tena Khilafah, nchi itakayoifundisha Amerika na umbile la Kiyahudi maana halisi ya urafiki na uadui. Wakati huo, maadui wa Mwenyezi Mungu (swt) watapata fedheha yao katika ulimwengu huu, kabla ya “kupelekwa” Kwake (swt), Ambaye atawahukumu kwa udhalilifu wa mwisho kesho Akhera.
Abdul Hakim Othman
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
Malaysia
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Malaysia |
Address & Website Khilafah Centre, 47-1, Jalan 7/7A, Seksyen 7, 43650 Bandar Baru Bangi, Selangor Tel: 03-8920 1614 www.mykhilafah.com |
Fax: 03-8920 1614 E-Mail: htm@mykhilafah.com |