Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Malaysia

H.  5 Safar 1447 Na: HTM 1447 / 01
M.  Jumatano, 30 Julai 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Maafa Mawili Yanaukumba Ummah wa Kiislamu – Watawala Wafisadi na Mfumo Fisadi – Yote Lazima Yabadilishwe kwa Wakati Mmoja

(Imetafsiriwa)

Mnamo 26 Julai 2025, jiji la Kuala Lumpur lilishuhudia maandamano ya ajabu ya umma — maandamano makubwa ya kudai kujiuzulu kwa Waziri Mkuu wa Malaysia, Datuk Seri Anwar Ibrahim. Mkutano huu ulionyesha hasira kubwa na kuchanganyikiwa kwa watu kuelekea uongozi ambao haujashindwa tu kutekeleza ahadi zake za mageuzi, lakini pia umezidisha ugumu wa watu kupitia nyongeza za kodi, ongezeko la ushuru wa umeme, na kupanda kwa bei za bidhaa muhimu.

Hasira ya umma inazidi kuchochewa na kile kinachoonekana sana kama unafiki wa Anwar. Ahadi yake ya kutokomeza ufisadi inapingana kabisa na ulinzi wake unaoendelea na kuwanua watu mafisadi. Zaidi ya hayo, ziara zake za mara kwa mara na za gharama kubwa nje ya nchi, ambazo aghlabu huhalalishwa na ahadi za mabilioni ya uwekezaji wa kigeni, zimethibitika kuwa ni maneno matupu tu.

Ingawa upinzani umefanikiwa kutumia hisia hii ya umma kwa kuandaa maandamano, wameshindwa kuwasilisha mtawala badali anayefaa. Kwa kweli, hakuna mrithi wazi aliyewasilishwa endapo Anwar atajiuzulu kweli. Angazo linabaki kuwa dogo — katika tu kumwondoa Waziri Mkuu, si katika kuanzisha njia inayoaminika ya kusonga mbele. La kusikitisha, umma unaendelea kuhamasishwa kulingana na hisia badala ya fikra sahihi ya kisiasa na masuluhisho yenye maana. Ni simulizi hii duni – kwamba tatizo liko kwa mtu mmoja tu, Anwar Ibrahim – ndiyo inayowapotosha watu. Wameshindwa kuelewa kwamba suala halisi sio mtawala tu, bali mfumo mzima unaotekelezwa nchini tangu miaka hiyo.

Tangu uhuru mwaka wa 1957, Malaysia imeongozwa na Mawaziri Wakuu kumi na vyama mbalimbali vya kisiasa – Barisan Nasional, Pakatan Harapan, Perikatan Nasional, na sasa serikali ya “Madani”. Ingawa sehemu ndogo ya idadi ya watu inaweza kuishi kwa raha, wengi wanaendelea kupambana na changamoto za kiuchumi, na masuala ya kijamii yanazidi kuwa ya kutisha. Sekta ya elimu, vivyo hivyo, inabaki kuwa imejaa matatizo yanayoendelea. Viwango vya uhalifu havionyeshi dalili za kupungua na vimekuwa vya kutisha sana, ikiwa ni pamoja na kile kinachotokea ndani ya jeshi la polisi lenyewe. Mazingira ya kisiasa yanaendelea kuchafuliwa na kashfa, ufisadi, uvunjifu wa uaminifu, mivutano ya madaraka, na aina nyenginezo mbalimbali za utovu wa nidhamu – ambazo watu huwa waathiriwa kila wakati.

Kwa kifupi, ingawa watawala wamebadilika baada ya muda, watu hawajawahi kupata raha na faraja ya kweli. Katika kila enzi ya utawala, watu wameendelea “kuasi” dhidi ya dhulma za serikali na kudai haki zao. Tangu enzi ya Dkt. Mahathir Mohamad (wa kwanza), Mawaziri Wakuu wameshinikizwa kujiuzulu – kutoka ndani ya vyama vyao na kutoka nguvu za nje. Hata hivyo, kila wakati Waziri Mkuu mpya anapoteuliwa, mabadiliko yanayotarajiwa na watu hayajawahi kutokea. Kinachobaki bila kubadilika ni mfumo wa kidemokrasia wenyewe – mfumo uliolazimishwa na dola za kikoloni kama sharti la uhuru wa nchi.

Je, mfumo ulioundwa na makafiri kinyume na mafundisho ya Uislamu unawezaje kutoa suluhisho la kweli kwa Ummah wa Kiislamu? Ni muhimu Waislamu waelewe ukweli huu msingi: kumbadilisha Waziri Mkuu bila kubadilisha mfumo hakutatui matatizo ya msingi yanayousumbua Ummah huu.

Hili si jambo la kipekee kwa Malaysia pekee. Katika ulimwengu wa Kiislamu, tunaona mpangilio huo huo: Tunisia, Misri, Yemen, na Libya zote zilipata machafuko wakati wa Mapinduzi ya Kiarabu ambayo yaliwaondoa watawala wao — lakini mifumo yao ya utawala ilibaki thabiti na mateso ya watu wao yaliendelea. Vile vile nchini Sudan, Uturuki, Pakistan, Bangladesh, Indonesia, na nchi zengine nyingi za Kiislamu, mabadiliko ya watawala yametokea mara kwa mara, lakini mifumo ya kisekula iliyorithiwa kutoka kwa wakoloni bado haijaguswa. Matokeo yake, hali ya Ummah imebaki bila kubadilika kwa kiasi kikubwa.

Ummah lazima uamke kwenye uhalisia huu; haupaswi kujiruhusu kung’atwa kutoka kwenye tundu moja mara mbili. Nchini Malaysia, kwa masikitiko, Ummah umeng’atwa si mara moja au mbili, bali mara nyingi tena na tena. Mara kwa mara, imethibitishwa kwamba wale walio madarakani chini ya mfumo wa kidemokrasia sio tu kwamba wanashindwa kutabikisha Uislamu — suluhisho halisi la migogoro yetu — lakini hawataki kufanya hivyo. Pia imethibitishwa kwamba urithi wa kikoloni wa demokrasia si tu kwamba hauendani na Uislamu, bali uliundwa waziwazi kutenganisha dini (Uislamu) na maisha. Kwa maana nyengine, uliundwa kuzuia utabikishaji wa Uislamu wenyewe. Huu ndio msiba pacha unaoukumba Ummah wa Kiislamu leo: watawala mafisadi na mfumo fisadi — vyote vimethibitishwa bila shaka.

Hakika, mifumo fisadi huzalisha watawala mafisadi, na watawala mafisadi huhifadhi mifumo fisadi. Kama vile ukomunisti unavyozalisha watawala wa kikomunisti wanaoshikamana na ukomunisti, na ubepari huzaa watawala wa kibepari wanaoshikamana na ubepari, vivyo hivyo demokrasia huendeleza duara lake lenye dosari. Mtawala na mfumo ni pande mbili za sarafu moja – zisizotengana na zinazoimarishana.

Hivyo, njia pekee ya kutokea kwa Ummah kutokana na majanga haya ni kubadilisha watawala na mfumo kwa wakati mmoja. Katika Uislamu, mtawala halali ni Khalifa, na mfumo na dola halali ni Khilafah. Hili ndilo ambalo Hizb ut Tahrir inalifanyia kazi bila kuchoka ili kulitimiza kote ulimwenguni, na huu ndio ulinganizi wetu kwa Ummah mzima – kufanya kazi nasi bega kwa bega ili kuusimamisha tena.

Abdul Hakim Othman
Msemaji Rasmi wa Hizb ut Tahrir
Malaysia

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Malaysia
Address & Website
Khilafah Centre, 47-1, Jalan 7/7A, Seksyen 7, 43650 Bandar Baru Bangi, Selangor
Tel: 03-8920 1614
www.mykhilafah.com
Fax: 03-8920 1614
E-Mail: htm@mykhilafah.com

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.