Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  10 Rabi' II 1443 Na: 1443/22
M.  Jumatatu, 15 Novemba 2021

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Sarafu ya Khilafah ya Dhahabu na Fedha Itamaliza Mfumko wa Bei, Unaosababishwa na Uchapishaji Pesa ili Kukidhi Matumizi ya Serikali

(Imetafsiriwa)

Nchini Pakistan, kuanzia Julai 2018 hadi Juni 2021, rasilimali iliyo katika mzunguko ilipanuka kwa bilioni 2,300, huku amana za benki ziliongezeka kwa bilioni 6,000. Rupia bilioni 8,300 zilifurika ndani ya mfumo katika miaka mitatu tu pekee, huku pato la taifa halikupanda kuendana na ongezeko hilo, kwa kiasi kikubwa likibaki palepale. Matokeo yasiyoepukika yalikuwa ni dhoruba ya mfumko wa bei, kwani nguvu ya ununuzi ya Rupia ilipungua. Bei za bidhaa zote zilipanda sana, na kuwanyima maskini uwezo wa kununua mahitaji ya kimsingi. Tabaka la kati sasa linazama kwenye deni, huku tabaka la chini likilazimika kuomba omba. Hata manufaa ya ongezeko la kawaida la Pato la Taifa yalikuwa kwa kipote maalum, kutokana na mkusanyiko mkubwa wa mali katika mfumo wa kirasilimali. Kwa hivyo, Enyi Watu wenye Nguvu, ni nani atakayejitokeza kuizika maiti hii iliyooza ya mfumo?

Katika Uislamu, hakuna dhana ya sarafu ya karatasi, isiyo na thamani ya ndani. Dinar ya dhahabu ya Khilafah na dirham ya fedha ndizo sarafu za dola. Katika Shariah dinar moja ni gramu 4.25 za dhahabu, huku dirham moja ni gramu 2.975 za fedha. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «وَالْوَزْنُ وَزْنُ أَهْلِ مَكَّةَ» “Na uzani ni uzani wa watu wa Makkah.” (An-Nisai). Sarafu inayotokana na msingi wa dhahabu na fedha huweka nidhamu katika matumizi ya serikali, kwani serikali haiwezi tu kuchapisha sarafu ya karatasi ili kufidia gharama. Kwa hivyo, sarafu thabiti ya dhahabu na fedha ya Khilafah inalinda watu dhidi ya mfumko wa bei wa jumla unaoonekana katika uchumi unaotegemea sarafu ya karatasi, isiyo na thamani ya kindani ambayo hupoteza nguvu yake ya kununua huku zaidi zikiendelea kuchapishwa. Kupungua tu kwa usambazaji au ongezeko la mahitaji ya bidhaa ya mtu binafsi kunaweza kuongeza bei peke yake, huku dola inaweza kuchukua hatua stahiki ili kurekebisha upungufu unaotabirika wa usambazaji, mapema kabisa, kama sehemu ya usimamizi wake wa watu.

Hadi leo, karibu dhahabu na fedha zote zinazozalishwa duniani ziko salama, imara na zinaimarika. Katika karne ya 18 na 19, licha ya kushuka kwa kasi kwa uzalishaji, sarafu ya dhahabu na fedha ilisaidia bei thabiti. Kwa kuwa sarafu ya dhahabu na fedha ni adimu na ya thamani sana, inabaki na uwezo wake wa kuleta utulivu leo. Pia ni sarafu hii ndiyo itakayomaliza utawala haramu ulioanzishwa wa dolari duniani. Amerik hununua kutoka kwa masoko ya dunia kwa pesa zake za karatasi, huku dunia nzima ikilazimika kupata dolari ili kuagiza bidhaa. Pakistan inakabiliwa na dhoruba ya mfumko wa bei, huku uchapishaji wa noti ili kukidhi matumizi ya serikali unadhoofisha sarafu mbele ya dolari. Kisha, kushuka kwa thamani ya Rupia dhidi ya dolari huongeza gharama ya kiasi cha kila uagizaji. Ili kukidhi upungufu wa akiba ya dolari, watawala wa Pakistan huigeukia IMF, ambayo inapanua udhibiti wake wa uchumi wa Pakistan, kupitia mikopo ya riba, iliyo na masharti ya kukandamiza. IMF kisha  huusakama uchumi wetu, na kuifanya Pakistan kuwa tegemezi kwa Magharibi na kujinyeyekesha kwake kiuchumi na kisiasa.

Kando na Khilafah kwa Njia ya Utume, ni mfumo upi mwengine unaoweza kumaliza janga la mfumko wa bei duniani? Ikiwa tajiri wa rasilimali kuu za nishati na madini duniani, Khilafah itatumia dinar za dhahabu na dirham za fedha katika biashara ya kimataifa, kurudisha uchumi wa dunia kwenye uwanja thabiti wa sarafu ya dhahabu na fedha. Ulimwengu umeteseka chini ya urasilimali kwa muda mrefu sana na unatazamia kurudi kwa Khilafah pamoja na Uislamu wake, kueneza ustawi. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «يَكونُ في آخِرِ الزَّمانِ خَلِيفَةٌ يَقْسِمُ المالَ ولا يَعُدُّهُ» “Katika zama za mwisho kutakuwepo na Khalifah itaigawanya mali wala haitaiihesabu.” (Muslim). Kando na Hizb ut Tahrir, ni uongozi gani mwengine unaoweza kutawalisha Uislamu kivitendo? Basi watu wenye nguvu nawatoe Nussrah yao kwa Hizb ut Tahrir ili kuiregesha dunia kwenye njia iliyo sawa.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: 
https://bit.ly/3hNz70q

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.