Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  27 Dhu al-Qi'dah 1446 Na: 45 / 1446
M.  Jumapili, 25 Mei 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Katikati ya Tabasamu za Idd na Machozi ya Gaza:
Wito kwa Maafisa na Wanajeshi

(Imetafsiriwa)

Huku Waislamu wakijiandaa kukaribisha Idd al-Adha na kusherehekea pamoja na watoto wao na wenza wao katika siku hizi za sherehe, tunaelekeza ujumbe huu makhsusi kwa wanajeshi na maafisa wanyoofu wa jeshi la nyuklia la Pakistan, na majeshi mengine ya Ummah kwa jumla. Tunawakumbusha katika siku hizi kwamba wamewatelekeza watu wao wenyewe, wanawake, watoto, wazee, na wanaume katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina na Gaza, na hawakujitokeza kuwanusuru licha ya kuwa na uwezo wa kufanya hivyo.

Tunakukumbusha juu ya kamanda wa kweli wa kijeshi na shujaa mtukufu, Salahuddin al-Ayyubi, ambaye hakutabasamu kwa kuanguka kwa Al-Quds (583 H / 1187 M) na aliugua sana kutokana na huzuni. Wakati huo, alisema, ما أشدّ ألمي وأنا أرى مدن الإسلام تسقط واحدة تلو الأخرى “Uchungu wangu ni wa kina kiasi gani ninapoitazama miji ya Uislamu ikianguka mmoja baada ya mwingine.” Hata baada ya kuiregesha Al-Quds kutoka kwa Makruseda kufuatia Vita vya Hattin, aliingia katika mji huo "na uso wa huzuni" na hakufurahia ushindi huo mkubwa, bali alibaki na huzuni. Alipoulizwa sababu ya huzuni yake, alijibu, كيف أفرح وقد ارتُكبت في هذه المدينة مآسٍ عظيمة؟! كيف أضحك وقد دخلتها وفي قلبي ألمٌ على ما جرى للمسلمين هنا؟  "Nitawezaje kufurahi wakati maafa makubwa kama haya yametokea katika mji huu? Nitacheka vipi ninapoingia humu, nikiwa na uchungu moyoni, kwa yale ambayo Waislamu wameyapitia hapa?" Aliuona ukombozi (tahrir) wa Al-Quds kama faradhi ya Shariah, na sio kama neema au kazi ya kishujaa. Hamu yake kubwa ilikuwa kutetea matukufu na maeneo matakatifu ya Waislamu, sio kujivunia ushindi.

Huu ndio ulikuwa msimamo wa Salahuddin, hali yake kabla na baada ya kukombolewa (tahrir) ya Al-Quds. La ajabu ni kwamba idadi ya Waislamu waliouawa na Wanajeshi wa Msalaba walipoikalia kwa mabavu Al-Quds ilikuwa karibu elfu sabiini, idadi sawa na au hata pungufu ya wale waliouawa na Mayahudi mjini Gaza na Palestina katika kipindi cha miaka miwili tu iliyopita. Kwa hiyo tunauliza: Je, hali yenu, enyi maafisa na wanajeshi, ni sawa na ile ya kiigizo chenu Salahuddin? Au mnajitayarisha kuwatembelea watoto na wake zenu, mkifurahi na kufurahia sikukuu ya Idd pamoja nao, kana kwamba mauaji ambayo yametokea, na yanayoendelea kutokea, mjini Gaza yanatokea katika kichinjio fulani kisichojulikana cha wanyama jijini Lahore, Dhaka, au Cairo?

Ikiwa hali yenu ni kama ya Salahuddin, basi munawezaje kufurahia kukutana na wapenzi wenu, au kupumzika juu ya vitanda vya wake zenu, hali mumeshindwa kufanya hata sehemu ya yale aliyofanya Salahuddin kwa ajili ya Kibla cha Kwanza na Msikiti watatu kwa utukufu katika Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina? Na mukisema, “Tunawezaje kujilinganisha na watu watukufu kama hao?” basi nyinyi ni miongoni mwa waliofanya khiyana na kula njama dhidi ya Waislamu, ambao wameegemeana na Mayahudi na kuwaunga mkono? Kisha mtakuwa mithiri ya askari wa Firauni muovu, muwe pamoja na Firauni au Hamana kama alivyowaeleza Mwenyezi Mungu.

[إِنَّ فِرْعَوْنَ وَهَامَانَ وَجُنُودَهُمَا كَانُوا خَاطِئِينَ] “Hakika Firauni na Hamana na majeshi yao walikuwa wenye makosa.” [Surah Al-Qassas 28:8]. Je, mungeridhika kufufuliwa pamoja nao katika Jahannam? Mwenyezi Mungu (swt) akulindeni na hilo!

Ninyi, enyi ndugu wapendwa, ni wa aina moja na Salahuddin. Hakuwa miongoni mwa Mitume (as) wala mfalme. Alikuwa ni mtu kama nyinyi, aliyeamini kama mlivyo amini, na akataraji kutoka kwa Mwenyezi Mungu kama nyinyi. Basi musisikilize minong'ono ya watawala waoga walioiuza Akhera yao kwa maisha ya kidunia ya kupita na ya udanganyifu.

Huzuni na msukumo uliofuata wa Waislamu kulipiza kisasi cha mashahidi wao haukuwa tu kwa mujahidina miongoni mwa makamanda na askari. Ulienea kwa idadi ya watu wote. Wanahistoria wameandika kwamba Waislamu katika Afrika Kaskazini na As-Sham walijizuia kusherehekea siku nyingi, kwa kuomboleza kuanguka kwa Al-Andalus. Baada ya kuanguka kwa Al-Quds na mauaji ya Al-Masjid Al-Aqsa, huzuni ilienea katika ulimwengu wa Kiislamu, na Waislamu walikataa kufanya harusi au sherehe. Hata Masultani wa Khilafah Uthmani baada ya kupoteza miji fulani huko Ulaya, wangepiga marufuku sherehe kwenye majumba na kutangaza maombolezo rasmi. Imepokewa kwamba Sultan Salim I alikuwa akisema, "Hakuna ladha ya chakula, hakuna kulala, na hakuna furaha katika moyo maadamu ardhi za Uislamu ziko katika hatari!"

Mifano hii inaonyesha kwamba kuhuzunika kwa kupoteza ardhi za Waislamu, kukiukwa matukufu yao, na kuuliwa wanaume na wanawake wao ni sehemu ya Imani. Maulamaa na watawala wa zamani waliona kufurahi wakati wa shida ni kumsaliti Mwenyezi Mungu (swt), Mtume wake (saw) na waumini. Ni nini basi kinachoweza kusemwa juu ya usaliti na ukimya mbele ya yale ambayo viumbe viovu zaidi, Mayahudi wanayafanya katika Ardhi Iliyobarikiwa?

Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema kweli pindi aliposema:

«مَنْ لَا يَهْتَمُّ بِأَمْرِ الْمُسْلِمِينَ فَلَيْسَ مِنْهُمْ، وَمَنْ لَا يُصْبِحُ وَيُمْسِي نَاصِحًا لِلَّهِ وَلِرَسُولِهِ وَلِكِتَابِهِ وَلِإِمَامِهِ وَلِعَامَّةِ الْمُسْلِمِينَ فَلَيْسَ مِنْهُمْ»

“Yeyote asiyejali mambo ya Waislamu si katika wao. Na asiyeanza na akamaliza siku kwa kunasihi kwa ajili ya Mwenyezi Mungu (swt), Mtume wake (saw), Kitabu Chake, kiongozi wa Waislamu, na Waislamu jumla, basi si katika wao.” [Imepokewa na al-Tabarani]

Hakika mumesikia na kuona kisa cha Dkt. Alaa Al-Najjar, ambaye alihuzunishwa na kufiwa na watoto wake tisa na mume wake, katika shambulizi la anga la kioga la kihalifu la Kiyahudi. Kwa hivyo munawezaje kupata faraja katika chakula, au kupumzika kwenye vitanda vya wake zenu wakati wa Idd al-Adha, wakati Dkt. Alaa ametoa kafara vipande vya moyo wake? Je Hamjui kwamba kuna maelfu kama Dkt. Alaa huko Gaza, kila mama ambaye amevunjika moyo kwa kufiwa na watoto wake na wapendwa wake katika kipindi cha miaka miwili iliyopita?

Ilitosha kwa al-Mu’tasim kusikia kilio cha mwanamke mmoja kutoka Amuriyya akiita, “Ewe Mu’tasim!” naye akaandaa jeshi kwa ajili yake. Ilitosha kwa al-Hajjaj ibn Yusuf kupokea habari za dhiki za wanawake kutoka Sind, wakitafuta ulinzi kutoka kwa mfalme dhalimu Dahir Shah hivyo akatuma jeshi likiongozwa na Muhammad bin Qasim, akamuua mfalme huyo, na kulipiza kisasi kwa wanawake wasafi wa Kiislamu. Basi, Wallahi (swt), mutasema nini, kwa vile sasa maelfu ya vilio vimekufikieni kutoka kwa wanawake watukufu wa Palestina? Je, chakula, kinywaji, au usingizi vinawezaje kukuleteeni faraja yoyote?

Imepokewa katika Sera ya Mtume, na katika zama za Khulafaa Rashidun (Makhalifa walioongoka) kwamba wanawake walikuwa wakijizuia na waume zao, ima kuwahimiza kutoka na kupigana, au kama njia ya kupinga dhidi ya uoga wao. Wakati wa msafara wa Tabuk, baadhi ya wanawake walikataa ukaribu na waume zao kama wangesita kujiunga na Jihad, wakiwataka watoke nje. Mwanamke mmoja alimwambia mumewe, لا طعم للطعام، ولا فرح للقلب ما دامت أرض الإسلام تحت التهديد “Hakuna tamu ya chakula, wala furaha ya moyo maadamu ardhi ya Kiislamu iko katika tishio.”

Umar ibn al-Khattab (ra) alikuwa akiwaadhibu wale wanaojizuia, na akawahimiza wanawake kuwatia moyo waume zao. Kwa hakika, baadhi ya wanawake hufikia hatua ya kuwaambia waume zao, إن لم تخرج للجهاد، فأنت طالق “Ikiwa hutoki kwenda Jihad, lazima unitaliki!” Imepokewa kwamba Ummu Hakim binti al-Harith alimhimiza mumewe, Ikrimah ibn Abi Jahl, ambaye alikuwa amesilimu baada ya kuupinga vikali Uislamu, atoke na kupigana. Alikataa unyumba naye hadi alipokwenda, na kwa hivyo alijiunga na vita na akauawa shahidi huko Yarmouk.

Uzembe wa askari na maafisa katika majeshi ya Waislamu unabeba matokeo mabaya. Hao ndio wenye uwezo na nguvu, na ndio wanaotarajiwa kuwanusuru wanaodhulumiwa, na kulinda heshima ya Waislamu. Wao sio kama watu wa kawaida. Kufeli kwao kunawavua uanaume wao na hadhi. Umar ibn al-Khattab (ra) alikuwa anawaaibisha hadharani wale waliobaki nyuma kutoka Jihad na kusema, لا تُقبل شهادة من ترك الجهاد بغير عذر “Ushahidi wa mwenye kuacha Jihad bila ya udhuru halali wa Shariah hautakubaliwa.”

Wala hatukwambiini, "Rekebisheni mapungufu yenu kabla ya kuchelewa," kwani kwa hakika, tayari ni kuchelewa mno! Badala yake, tunabaki kufidia yale mliyoyapuuza, tubuni kwa Mwenyezi Mungu (swt) kwa kufeli na kusitasita kwenu, na nendeni mkiwa na vifaa vyepesi au vizito na muwanusuru ndugu zenu wanaofanya kazi ya kusimamisha dola ya Kiislamu kupitia Hizb ut Tahrir, inayotawala kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt) na kuyakusanya majeshi kuzikomboa ardhi za Waislamu, na muwasaidie wanaodhulumiwa nchini Palestina, Kashmir, miongoni mwa Warohingya wa Burma, na wengineo, wale ambao wamepoteza matumaini kwa makamanda na watawala wenu wasaliti, waoga, na sasa wamebaki tu wale wanyoofu miongoni mwenu.

Je, mutaitikia wito wa Dkt. Alaa Al-Najjar na wanawake wengine watukufu wa Ummah huu? Je, mutajiunga na safu za Salahuddin, Muhammad bin Qasim, na Khalid ibn al-Walid kwenye birika (hawdh) la Muhammad al-Mustafa (saw)? Au mutatosheka kusimama pamoja na watawala wabaya na makamanda wao wa kijeshi pamoja na Firauni na Haman huko Saqar (Moto wa Jahannam)?

Hizi ni siku za majaribio na mtihani kwa kila mtu mwenye akili na uzito wa chembe ya atomi ya Imani moyoni mwake, kuchagua kile anachostahiki kweli. Jueni kuwa mafanikio ya mwisho ni kwa wacha Mungu. Amesema Allah (swt):

[وَسَارِعُوا إِلَى مَغْفِرَةٍ مِنْ رَبِّكُمْ وَجَنَّةٍ عَرْضُهَا السَّمَاوَاتُ وَالْأَرْضُ أُعِدَّتْ لِلْمُتَّقِينَ]

“Na yakimbilieni maghfira ya Mola wenu Mlezi, na Pepo ambayo upana wake ni mbingu na ardhi, iliyo wekwa tayari kwa wachamngu.” [Surah Aali Imran 3:133].

Na, amesema Mwenyezi Mungu (swt),

[انْفِرُوا خِفَافًا وَثِقَالًا وَجَاهِدُوا بِأَمْوَالِكُمْ وَأَنْفُسِكُمْ فِي سَبِيلِ اللَّهِ ذَلِكُمْ خَيْرٌ لَكُمْ إِنْ كُنْتُمْ تَعْلَمُونَ]

“Nendeni mtoke, mkiwa wepesi na wazito, na piganeni Jihadi kwa mali yenu na nafsi zenu katika Njia ya Mwenyezi Mungu. Haya ni kheri kwenu mkiwa mnajua.” [Surah At-Tawbah 9:41]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.