Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan

H.  5 Jumada I 1447 Na: 13 / 1447
M.  Jumatatu, 27 Oktoba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Watawala wa Pakistan, Watu wa Trump, Wawateka nyara Mashababu wa Hizb ut Tahrir ili Kuhakikisha Kujisalimisha kwa Palestina

(Imetafsiriwa)

“Jenerali kipenzi cha Trump,” Asim Munir, amejibu kwa udhalimu kampeni yenye nguvu ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Pakistan, ambayo kwayo inataka uhamasishwaji wa haraka wa Vikosi vya Jeshi la Pakistan ili kuikomboa Palestina. Majambazi wa Asim Munir wamewateka nyara matetezi watano, kutoka Lahore, Karachi na Peshawar, na mahali walipo hapajulikani. Udhalimu wa Asim Munir unatarajiwa. Asim Munir hawezi kutenda, sembuse kufikiria, nje ya maagizo ya Trump katika suala lolote, iwe kuhusu Gaza, Kashmir, Afghanistan au rasilimali kubwa za madini za Pakistan. Maagizo ya sasa ya Trump kwa Gaza ni “amani kupitia nguvu,” ambayo inamaanisha kukandamiza kwa nguvu upinzani wowote dhidi ya kusalimishwa kwa sehemu kubwa ya Palestina Iliyobarikiwa kwa umbile la Kiyahudi, chini ya mpango wa Trump, Mkataba wa Abraham. Kwa hivyo, Asim Munir alihamasisha dhidi ya Hizb ut Tahrir, kama vile vibaraka wengine wa ukoloni katika Ulimwengu wa Kiislamu walivyofanya, ikiwemo Jordan na Lebanon hivi karibuni.

Enyi Waislamu wa Pakistan, Ardhi Safi! Sisi, Mashbabu (wanachama) wa Hizb ut Tahrir, tunawahakikishia kwamba hatutaacha Dawah ya Uislamu, kwa idhini ya Mwenyezi Mungu (swt). Kwa robo karne nchini Pakistan, tumekabiliana na madhalimu wengi, kuanzia Musharraf hadi Asim Munir, tukivumilia kampeni nyingi za unyanyasaji, kukamatwa, kuteswa na kutekwa nyara. Tunaendelea kwa subira kwa sababu tunafuata njia ya Mtume (saw) kwa ajili ya mabadiliko. Tunajitahidi kuiga subira ya Mtume (saw) ambaye alipigwa mawe na Abu Lahab, na kusababisha vifundo vya miguu na misuli yake kutokwa na damu mara tu baada ya kuwatangazia watu «يَا أَيُّهَا النَّاسُ، قُولُوا، لا إِلَهَ إِلَّا اللَّهُ تُفْلِحُوا» “Enyi watu, semeni hakuna mola wa haki isipokuwa Mwenyezi Mungu nanyi mtafaulu.” Tunajitahidi kuiga subira ya Yaasir (ra) ambaye alishuhudia kifo cha kishahidi cha wazazi wake, ambaye Mtume (saw) amesema kuhusiana nao, «صَبْراً آلَ ياسر فإنَّ مَوْعِدَكُم الجَنَّة» “Kuweni na subira enyi Jannah ni Jannah.”

Na tunaendelea kwa subira, tukihakikishiwa kwamba baada ya utawala wa dhulma na ukandamizaji, kuna Khilafah kwa Njia ya Utume. Ahmed amesimulia kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema, «ثُمَّ تَكُونُ مُلْكًا جَبْرِيَّةً فَتَكُونُ مَا شَاءَ اللَّهُ أَنْ تَكُونَ ثُمَّ يَرْفَعُهَا إِذَا شَاءَ أَنْ يَرْفَعَهَا ثُمَّ تَكُونُ خِلَافَةً عَلَى مِنْهَاجِ النُّبُوَّةِ»  “Kisha kutakuwa na utawala wa nguvu za kidhalimu, na utakuweko kwa muda anaotaka Mwenyezi Mungu uweko, kisha atauondoa atakapo Mwenyezi Mungu kuuondoa. Kisha itakuwepo Khilafah kwa Njia ya Utume.” Hakika, ni Sunnah ya Mwenyezi Mungu (swt) kuwajaribu Waislamu, kabla ya kuwapa nasr (ushindi). Kwa hivyo simameni nasi, ubavuni mwetu, nyuma yetu na mbele yetu, katika kuinua neno la haki mbele ya madhalimu!

Enyi Maafisa wa Vikosi vya Jeshi la Pakistan! Inajulikana vyema kwenu kwamba Hizb ut Tahrir haibebi silaha, licha ya udhalimu wote ambao imekabiliana nao kwa zaidi ya miongo saba, katika Ulimwengu wote wa Kiislamu. Hivyo, Hizb ut Tahrir inafuata kikamilifu mfano wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) ambaye alijiwekea mipaka mjini Makka kwa Dawah, na hakufanya vitendo vyovyote vya kijeshi, hadi (saw) alipofanya Hijra. Pindi watu wa Ahadi ya Pili ya Aqabah (Bay’ah) walipomwomba (saw) ruhusa ya kupigana na watu wa Mina kwa mapanga, yeye (saw) aliwajibu kwa kusema, «لَمْ نُؤْمَرْ بـِذَلِكَ» “Hatujaamrishwa kufanya hivyo bado.”

Sasa, ingawa sisi, Mashababu wa Hizb ut Tahrir, hatubebi silaha, tunawataka nyinyi, watu wenye silaha, mamlaka na nguvu, mutoe nusrah yenu (msaada wa kijeshi) kwa ajili ya kusimamisha tena Khilafah kwa Njia ya Utume. Ombi letu ni kwa mujibu wa njia ya Mtume (saw). Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) alikutana na watu wa vita, moto na chuma, na akawataka nusrah (msaada wa kijeshi) kwa ajili ya kusimamisha Dini. Yeye (saw) alitafuta wenye nguvu, kuhusiana na uwezo wa kisilaha kwa kina, akiuliza, «فَهَلْ عِنْدَ قَوْمِكَ مِنْ مَنَعَةٍ؟» “Je, watu wenu wana nguvu za kijeshi?” Hivyo yeye (saw) alikutana na makabila mengi yakiwemo; Banu Kalb, Banu Hanifah, Banu Amr bin Sa’asah, Banu Kinda na Banu Shaiban. Yeye (saw) alidumu katika njia hii kwa subira hadi Mwenyezi Mungu (swt) alipompa mafanikio. Answar (ra) walimpa Nusrah, na Dola ya Kiislamu ya Madina ikaasisiwa. Kwa hivyo, licha ya udhalimu wote tunaokabiliana nao, tutaendelea kudai kwamba mutoe nusrah (msaada wa kijeshi) kwa ajili ya kusimamisha tena hukmu kwa yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu (swt). Ama nyinyi, jihadharini katika majibu yenu, tusije tukatoa ushahidi dhidi yenu mbele ya Mwenyezi Mungu (swt) Siku ya Kiyama!

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Pakistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Pakistan
Address & Website
Tel: +(92)333-561-3813
http://www.hizb-pakistan.com/
Fax: +(92)21-520-6479
E-Mail: htmediapak@gmail.com

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.