Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Tanzania

H.  30 Dhu al-Qi'dah 1441 Na: 1441 / 04
M.  Jumanne, 21 Julai 2020

 Taarifa Kwa Vyombo vya Habari

Sikilizeni Kesi za Mahabusu, Wapeni Dhamana au Waachieni Huru Mara Moja

Ni karibu miaka mitatu sasa tangu wanachama watatu wa Hizb ut Tahrir Tanzania: Ustadh Ramadhan Moshi (41), Waziri Suleiman (33) na Omar Salum Bumbo (51) kunyakuliwa kisha kubambikiziwa mashtaka ya uongo ya ‘kula njama ya kutenda ugaidi’ na ‘kutenda matendo ya ugaidi’. Kwa maelezo zaidi soma taarifa yetu kwa vyombo vya habari ya tarehe 14 Disemba 2017:

http://www.hizb-ut-tahrir.info/en/index.php/press-releases/tanzania/14417.html

Kwa kipindi chote cha wanachama wetu hao kuwa mahabusu, licha ya kuwa mbali na familia zao, ndugu, marafiki na kusita kwa shughuli zao za uzalishaji, pia wamerundikwa katika mahabusu zenye mazingira duni kibinadamu, yakikosa usalama wa kiafya na huduma stahiki kwa jumla.

Baya na la kusikitisha zaidi, kesi yao imekuwa ikitajwa tu kila wiki mbili, bila ya kuanza kusikilizwa, kwa kisingizio cha kutokamilika ukusanyaji wa ushahidi ati kwa karibu miaka mitatu sasa!

Sisi Hizb ut Tahrir Tanzania tunasisitiza kwa kinywa kipana kwamba wanachama wetu hao hawana tembe ya hatia, na ndio maana mpaka sasa kumekosekana hali ya kujiamini na ujasiri wa kuanza kusikilizwa kesi yao. Wanachama wetu hao na wengi wengineo waliotajwa katika waraka wa karibuni wa Shura ya Maimamu (uk 17-25) si zaidi, bali ni wahanga wa sheria ya kibaguzi ya Kupambana na Ugaidi iliyolazimishwa na madola makubwa (kwa nchi changa) inayotumika kudhulumu, kukhofisha, kutesa, kuteka nk.

Pia tunasisitiza kwamba tangu kuasisiwa Hizb ut Tahrir mnamo mwaka 1953 imekuwa ikilingania Uislamu kwa kushikamana kwa umakini wa hali ya juu na njia ya Mtume SAAW kwa kujifunga kikamilifu na njia ya kifikra na kisiasa ikijiepusha kwa hali zote na utumiaji nguvu na mabavu.

Kwa mara nyengine tena, sisi Hizb ut Tahrir / Tanzania tunatoa mwito wa kuzitaka taasisi zote husika na utoaji wa haki ndani ya Tanzania kushikamana ipasavyo na mchakato wa kimahkama, amma kwa kuwasilisha ushahidi dhidi ya mahabusu hao mahkamani tayari kuanza kusikiliza kesi zao, lau kama wanao huo ushahidi, amma kuwapatia wanachama wetu hao dhamana, au kuwaachia huru mara moja.

Masoud Msellem
Mwakilishi kwa Vyombo vya Habari Hizb ut Tahrir Tanzania

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Tanzania
Address & Website
Tel: +255778 870609
E-Mail: mediarep@hizb.or.tz

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.