Afisi ya Habari
Wilayah Uturuki
| H. 29 Rabi' II 1447 | Na: 1447/05 |
| M. Jumanne, 21 Oktoba 2025 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mjini Gabes: Janga la Mazingira na la Kibinadamu... Na Adhabu ya Jumla Dhidi ya Vizazi
(Imetafsiriwa)
Mji wa Gabes umekumbwa na janga kubwa, pumzi yake imenyongwa kwa kifo cha polepole kutokana na mgogoro wa mazingira unaosababishwa na uzalishaji wa hewa chafu kutoka kwa kiwanda cha kemikali.
Wakati huo huo, wakaazi wanaendelea kumsubiri gavana ambaye hajafika kukomesha uharibifu mkubwa kwa maisha yao. Badala yake, msafara wa vitengo vya usalama ulifika, ukikandamiza maandamano ya amani ya watoto, wanawake, na wazee, wakiwakabili kwa gesi ya machozi!
Polisi pia walikamata zaidi ya watu 70 wakati wa saa za usiku za Ijumaa, na idadi hiyo iliongezeka kufikia alfajiri. Baadhi walichukuliwa kutoka majumbani mwao, kulingana na Khair Eddine Dabiya, mwanachama wa kampeni ya “Komesha Uchafuzi wa Mazingira”. Baadhi walipelekwa kushtakiwa, huku wengine wakifungwa. Matakwa ya waandamanaji yalibadilika kutoka kuzuia uchafuzi wa mazingira hadi kuwaachilia huru wafungwa!
Kwa kuzingatia maendeleo haya, sisi, katika Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia, tunasisitiza yafuatayo:
1- Matakwa ya waandamanaji ya kuvunjwa na kufungwa viwanda vinavyochafua mazingira ni matakwa halali ambayo mamlaka lazima ziyatii mara moja. Uamuzi wa kuvunjwa viwanda hivyo ulitolewa mwaka wa 2017, na baraza la mji wa Gabes hapo awali lilikuwa limeonya kwamba viwanda hivi vinahatarisha maisha moja kwa moja.
2- Matumizi ya vurugu na ukamataji yatazidisha hali hiyo na kufichua tena ulemavu wa watawala wetu na unyakuzi wao wa ubwana linapokuja suala la majukumu msingi kabisa ya utunzaji. Wako haraka kutumia fimbo ya mamlaka na kuwanyima watu haki zao halali za maisha yenye staha.
Enyi Watu Wetu wa Tunisia ya Kijani: Uchafu unaojaza mazingira yetu ni matokeo ya kimaumbile ya mfumo wa kibepari wenye tamaa ambao hamu yake pekee ni faida na kuongezeka kwa uzalishaji. Yanayotokea leo mjini Gabes si tofauti, ni mfano wa uchafuzi wa mazingira unaosababishwa na gesi ya visukuku huko Kairouan, taka za nyuklia huko Douz, tatizo la takataka huko Sfax, na miradi ya hidrojeni ya kijani katika mustakbali wa hivi karibuni.
Tatizo la mazingira linaweza kutatuliwa kwa kiasi kikubwa tu chini ya uongozi wa Khilafah Rashida kwa njia ya Utume. Dola hii ina maamuzi yake yenyewe, inadhibiti vitendo vyake kulingana na hukmu za sheria ya Kiislamu, inamwogopa Mwenyezi Mungu katika kuamiliana na watu wake na ardhi yake, na inakata mkono wa ukoloni kwa kufutilia mbali mikataba ya kimataifa inayoendeleza utegemezi, kupora utajiri, na kunyonya rasilimali kwa gharama ya watoto wetu na mazingira yetu. Imepokewa kutoka kwa Abu Dhar kwamba Mtume (saw) amesema: «عُرِضَتْ عَلَيَّ أُمَّتِي بِأَعْمَالِهَا حَسَنِهَا وَسَيِّئِهَا فَرَأَيْتُ فِي مَحَاسِنِ أَعْمَالِهَا الأَذَى يُنَحَّى عَنِ الطَّرِيقِ وَرَأَيْتُ فِي سَيِّئِ أَعْمَالِهَا النُّخَاعَةَ فِي الْمَسْجِدِ لاَ تُدْفَنُ» “Umma wangu ulionyeshwa kwangu pamoja na amali zao nzuri na mbaya. Miongoni mwa amali zao njema niliona kitu chenye madhara kikiondolewa barabarani. Na miongoni mwa amali zao mbaya niliona makohozi msikitini ambayo hayakuwa yameondolewa.”
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Tunisia
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Uturuki |
Address & Website Tel: http://www.hizb-turkiye.org |
E-Mail: bilgi@hizb-turkiye.org |