Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Uzbekistan

H.  26 Dhu al-Qi'dah 1446 Na: 1446 / 14
M.  Jumamosi, 24 Mei 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Enyi Madhalimu! Fungueni Macho yenu!
(Imetafsiriwa)

Mnamo 19 Mei 2025, kesi ya wanachama 33 wa Hizb ut Tahrir, iliyodumu kwa karibu miezi minane, ilifikia kikomo. Kwa mujibu wa uamuzi wa mahakama, Musayev Shukrullah alihukumiwa kifungo cha miaka 17 katika jela maalum ya utawala; Selimov Dilshod alihukumiwa miaka 16 katika gereza maalum la utawala; Watu 20 walihukumiwa kifungo cha miaka 12 katika gereza maalum la utawala; Watu 8 walihukumiwa kifungo cha kati ya miaka 8 na 10, 4 kati yao katika hali maalum na wengine 4 katika hali kali; na watatu waliosalia walihukumiwa kati ya miaka 4 na 5 chini ya kifungo cha nyumbani. Baada ya uamuzi huo kutangazwa, hakimu aliondoka haraka kwenye chumba cha mahakama chini ya dhoruba ya kulaaniwa na dua dhidi yake, licha ya ukweli kwamba, tofauti na kesi za awali, kikao hiki cha mwisho kilihudhuriwa na idadi kubwa ya wafanyikazi wa Usalama wa Serikali, vitengo vya kukabiliana na ugaidi, na walinzi wa kijeshi. Vyombo vya habari, ikiwemo chaneli ya TV ya Uzbekistan 24, wanablogu, na afisa wa usalama wa kibinafsi, walirekodi kikao kwenye video.

Katika kauli zao za mwisho mahakamani, vijana hawa walimhutubia Rais Mirziyoyev na vikosi vyake vya usalama (Huduma ya Usalama wa Taifa), wakizungumza kwa mtazamo wa juu wa Kiislamu. Kwa kawaida, mashirika ya usalama ya utawala wa Uzbekistan, ambao hutetemeka kwa sauti ya ukweli, hawakuweza kustahamili hotuba hii! Kwani licha ya jinai zilizotendwa, na ambazo zingali zinafanywa na utawala dhidi ya Uislamu na Waislamu, ambazo zitaandikwa katika kurasa za historia, umeshindwa kuwavunja Waislamu wetu wenye mapenzi yasiyo na kifani kwa Uislamu, na haujaweza kuwavunja Mashababu wa Hizb ambao wamejitolea maisha yao na mali zao kwa ajili ya kushikamana na neno la Mwenyezi Mungu, na kwa mapenzi ya Mwenyezi Mungu, utawala huo hautaweza kamwe.

Fauka ya hayo, Mashababu hao walikabiliwa na kiwango kisicho na kifani cha mateso, shinikizo, na vurugu wakati wa mchakato wa uchunguzi ambao uliendelea hadi kesi hiyo iliposikilizwa. Je, vyombo vya usalama, ambavyo mikono yao imetapakaa damu ya vijana wengi wa Kiislamu waliodhulumiwa tangu enzi za dhalimu Karimov, havitafakari juu ya hesabu ya kesho?! Je, hawafikirii kwamba dua za waliodhulumiwa – ambazo zinajibiwa kwa hakika – zitaathiri familia zao, watoto wao, na wapenzi wao?!

Mtume wa Mwenyezi Mungu (swt) amesema:

«اتَّقِ دَعْوَةَ الْمَظْلُومِ فَإِنَّهَا لَيْسَ بَيْنَهَا وَبَيْنَ اللهِ حِجَابٌ» “Iogope dua ya mwenye kudhulumiwa kwani hakuna pazia baina ya dua yake na Mwenyezi Mungu.” Na akasema:

 «إِنَّ اللهَ لَيُمْلِي لِلظَّالِمِ حَتَّى إِذَا أَخَذَهُ لَمْ يُفْلِتْهُ» “Mwenyezi Mungu humpa muhula dhalimu, lakini pindi anapomshika hamuachi.” Na akasema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[فَأَذَّنَ مُؤَذِّنٌ بَيْنَهُمْ أَن لَّعْنَةُ اللهِ عَلَى الظَّالِمِينَ] “Basi mtangazaji atawatangazia: Laana ya Mwenyezi Mungu iwapate walio dhulumu.” [Surat Al-A’raf:44]

Leo, kuna fursa kwa utawala wa Uzbekistan na vyombo vyake vya usalama kuacha dhulma wanayoifanya, lakini kesho itakuwa imechelewa sana – kwani mapambazuko ya nusra na ushindi ulioahidiwa na Mwenyezi Mungu, Aliyetukuka, yamekaribia, kwa idhini Yake. Na ole wao ikiwa hawatajiokoa na fedheha ya dunia hii na adhabu kali ya Akhera!

[وَاللهُ غَالِبٌ عَلَى أَمْرِهِ وَلَكِنَّ أَكْثَرَ النَّاسِ لَا يَعْلَمُونَ]

“Na Mwenyezi Mungu ndiye Mwenye kushinda katika jambo lake, lakini watu wengi hawajui.” [Surat Yusuf:21]

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Uzbekistan

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Uzbekistan
Address & Website
Tel: 

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.