Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  10 Dhu al-Hijjah 1443 Na: HTY- 1443 / 21
M.  Jumamosi, 09 Julai 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Makombora na Droni za Baraza la Kisiasa la Sana'a zinalenga kila mtu isipokuwa Waamerika
Baraza la Rais la Aden Hupokea Waamerika kwa Kulazimishwa

(Imetafsiriwa)

Gazeti la kila siku la Al-Thawra, linalochapishwa jijini Sana'a, liliripoti habari ya kuwasili kwa balozi wa Marekani nchini Yemen, Stephen Magen, kutoka Jeddah hadi Hadramout, na mkutano wake na viongozi wa eneo hilo. Hivyo je, makombora ya balestiki ya Mahouthi yalishindwa kufika mkoa wa Hadramout ndani ya Yemen, na kuwapiga wanajeshi wachache tu wa Kiamerika, licha ya kuwa tayari walikuwa wamefika sehemu nyingi katika falme za Al Saud na Al Zayed, kwa kupitia mipaka ya Sykes na Picot, na sauti za Mahouthi ziliimba asubuhi na jioni, kiangazi na kipupwe, “Kifo kwa Amerika”?!

Mahouthi lazima watambue kwamba Amerika na mabalozi wake, kutoka Krajesky hadi Firestein, na balozi wake wa sasa, Stephen Fagin, sio wadhamini, bali kwa kweli ni wapiganaji halisi. Mabalozi wake na vyombo vyake vya kimataifa vinaonekana waziwazi na havifichiki kwa mtu yeyote. Ni "jambo la kutiliwa shaka"! Ikiwa kauli mbiu ya "Kifo kwa Amerika" ingekuwa ya kihakika, roketi na maandamano hayangeacha macho yao yakitazama au kope zao zikipepesa. Miaka minane imepita tangu vita hivyo, na leo tunashuhudia mapatano, na hakuna hata damu moja ya Mwamerika iliyomwagika!

Mahouthi mara nyingi husema kuwa al-Qaeda ndio bendera ambayo wanajeshi wa Marekani wanajificha nyuma yake ndani ya Yemen. Kwa hiyo wanasubiri nini?! Vikosi vya Marekani vilivyoko ndani ya Yemen, hasa katika makao makuu ya kikosi cha ulinzi wa pwani "Qarat al-Persa" jijini Hadramout, na jijini Ma'ashiq Aden, viko ndani ya masafa ya makombora na droni zao.

Je, Mahouthi wanalipimaje suala la Amerika? Wacha tuchukulie kwamba kauli mbiu sio kifo kwa Amerika. Je, Waamerika sio majeshi yanayokalia kwa mabavu nchini Yemen, na kwa miaka mingi ya vita mmetangaza hivyo? Kwa nini jeshi na kamati za raia zisiwalenge kwa mapigano na makabiliano hata kwa mbali, kwa makombora na droni?! Swali ambalo tunawauliza wafuasi wa Houthi kwa matumaini kwamba tutapata jibu lenye ufahamu wa kisiasa kutoka kwao. Au je Mahouthi wanaendelea kuwasaidia Wamarekani katika kulikalia kwa mabavu eneo ya kusini mwa Yemen, wakifuata nyayo za Iran katika ushirikiano wake na Marekani katika kuikalia kwa mabavu Afghanistan na Iraq?!

Hatusemi maneno haya kumtoa hatiani Al-Alimi na baraza lake kwamba ni muundo wa Magharibi. Badala yake, wote wawili wako katika mbio za uovu. Baraza la Rais na vitengo vyote ni sawa katika maeneo ya kusini, mashariki na kati mwa Yemen. Walipitiliza mno katika dhulma na ukandamizaji, kama wale wa kaskazini mwa Yemen. Kwa hivyo, enyi wafuasi, ni lazima mtafakari juu ya matendo ya viongozi hawa ili kwamba kifiniko kifunuliwe kwenu, na kupima matendo yao kwa mujibu wa itikadi yenu. Kisha ni lazima muende pale anapokuamrisheni Mwenyezi Mungu, kwa hivyo uhalalishaji huu hautakuwa na manufaa mikononi mwa Mwenyezi Mungu Mtukufu Siku ya Kiyama.

Imani na ukafiri havikutani, na imani ya kweli ndiyo itakayoitoa Marekani katika ardhi za Kiislamu, nje ya Bahari ya Atlantiki, chini ya dola ya Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, Mwenyezi Mungu akipenda.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.