Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  15 Safar 1444 Na: HTY- 1444 / 02
M.  Jumapili, 11 Septemba 2022

 Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Mgomo wa Walimu nchini Yemen Kutokana na Ustawi duni wa Mamlaka una matokeo mabaya
(Imetafsiriwa)

Chama cha Walimu na Walezi wa Kusini mwa Yemen, ambacho kiko chini ya mamlaka ya Baraza la Uongozi wa Rais, kilitoa taarifa kikitangaza mgomo mkubwa na kufungwa kwa shule zote za umma tangu mwanzo wa mwaka mpya wa shule mnamo 7 Agosti. Hii inatokana na kile ambacho Chama hicho kinaona kuwa ni ghiliba ya serikali na mamlaka za mitaa zilizo na haki na stahiki za mwalimu na ukiukaji wake wa ahadi zote za awali kwa Chama hicho.

Iwapo tutautazama kwa makini uhalisia wa elimu nchini Yemen, tutagundua kuwa serikali hizi zimefanya jinai mbili dhidi yake. Kwanza ni kuwa iliwakandamiza walimu na kutowathamini; mishahara yao ndio midogo zaidi, matokeo yake hali yao ya kifedha imekuwa ngumu sana. Wanapata shida badala ya kuishi kwa utulivu ili kuwa wabunifu na kujenga kizazi imara. Ama jinai ya pili, ni katika mitaala ya kielimu ambayo msingi wake hautofautiani na ule wa nchi nyingine za dunia, nayo ni fikra ya kutenganisha dini na maisha, ambayo inazingatiwa kuwa miongoni mwa fikra ambazo Magharibi huzitumia katika vita vyake kwa Uislamu. Ikiongezewa na mwelekeo wa hadhara ya kirasilimali ya Kimagharibi kupitia mukhtasari wa mitaala ya elimu iliyowekwa na UNESCO katika ngazi ya dunia, ikiwemo Yemen, ili kutumikia maslahi ya Magharibi kafiri na usekula wake.

Nchini Yemen, kutokana na mzozo wa kimataifa juu yake, haki za watu zilipotea, ikiwemo mishahara ya walimu, ambayo ilisababisha hasara ya kizazi kizima cha vijana, iwe ni kutafuta riziki au kuwindwa na kusukumizwa viwanja vya vita ili kuwa chachu ya mzozo unaowahudumia tu Magharibi kafiri na maslahi yake pekee, au wao na walimu wao wanakuwa windo mikononi mwa Mashirika yasiyo na huruma na mwanamume au mwanamke. Je! serikali za maangamizi huko Sanaa na Aden hazijui hili?! Au wanafahamu na wameafikiana kwa hiari kwa kubadilishana kifurushi cha dolari chafu ambazo hazitawaokoa, kwa yale waliyokabidhiwa na kuwajibika kwayo, mbele ya Muumba wao (swt), Siku ya Kiyama, ambayo Mwenyezi Mumgu (swt) anaeleza katika Kitabu chake kitukufu:

[وَعَنَتِ الْوُجُوهُ لِلْحَيِّ الْقَيُّومِ وَقَدْ خَابَ مَنْ حَمَلَ ظُلْماً]

“Na zitadhalilika nyuso mbele ya Aliye Hai Milele, Mwangalizi Mkuu. Na atakuwa ameharibikiwa mwenye kubeba dhulma.” [Ta-Ha: 111].

Ingawa maombi yao ni machache na rahisi, na hayafikii khumusi ya kile kinachotumiwa na mawaziri wa hoteli katika serikali ya Aden, au manyapara wa serikali ya Sanaa, hali ya mwalimu nchini Yemen imefikia kuwa mbaya sana.

Ummah mzima wa Kiislamu, wakiwemo watu wa Yemen na walimu wake, haujakosa utajiri wa kimada kuishi kwa heshima na fahari, wala haujakosa uwezo wa kuendeleza mipango, mikakati na mbinu za ubunifu, wala haujakosa uwezo wa kunyonya njia za kisasa za kiufundi, wala ubunifu katika maendeleo yake. Mtiririko wa wanazuoni wa Kiislamu katika nchi za Magharibi unashuhudia hilo. Bali, tatizo lisilotibika ni kusalimisha uamuzi wa kisiasa wa Ummah wetu mikononi mwa maadui zake kupitia kwa watawala na wanasiasa wasaliti, na baadhi ya mabatili walioridhika kula makombo ya meza za fikra mbaya za Magharibi. Hivyo basi, msingi uliojengwa juu yake mtaala wa elimu ni lazima uwe ni imani ya Kiislamu, hivyo nyenzo zote za masomo na mbinu za kufundishia ziwekwe katika hali ambayo hairuhusu elimu kukengeuka kutoka katika msingi huu, kwa sababu sera ya elimu katika Uislamu ni ujengaji aqliya na nafsiyya ya Kiislamu ili kufikia lengo la elimu, ambalo ni kuunda shakhsiya ya Kiislamu, na wajibu wa kupeana mahitaji ya kimsingi ya watu binafsi, na kuwawezesha kupata mahitaji ya ziada kwa kadiri inavyowezekana kwa raia wote wa dola, wakiwemo walimu. Hizb ut Tahrir imeeleza sera ya elimu chini ya Dola ya Khilafah ndani ya kijitabu kinachoelezea sera hii, ambacho kinapatikana kwenye tovuti rasmi za hizb kwa wale wanaotaka kuitazama. Sera hiyo ambayo haitakuwepo ardhini isipokuwa katika kivuli cha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume ambayo Hizb ut Tahrir inaifanyia kazi, kwa hiyo tunawalingania watu wa Yemen, watu wa Iman na Hekima kufanya kazi kwa ajili ya kheri hii kubwa na kuachana na serikali vibaraka za kihalifu ambazo uvundo wake wa ufisadi umeenea. Tunamuomba Mwenyezi Mungu (swt) aharakishe kuwasili kwa siku hiyo ambapo sera hii itatekelezwa na kutabikishwa kivitendo.

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 735417068
http://www.hizb-ut-tahrir.info
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.