Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  13 Safar 1447 Na: HTY- 1447 / 03
M.  Alhamisi, 07 Agosti 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Wakati Mahouthi Wakishangilia Uhamasishaji wa Makabila ya Bakil na Hashid na Kupigwa kwa Ngoma za Vita Baina Yao!
(Imetafsiriwa)

Mnamo Jumamosi, 26/07/2025, Sheikh Hamid Mansour Radman aliuawa katika eneo la Al-Hayit, Wilaya ya Ayal Surayh, katika Mkoa wa Amran, na mkwe wake, Hamir Saleh Rattas Falyatah (Abu Udhr) mkuu wa idara ya polisi ya Al-Hayit. Mauaji ya Sheikh Radman yalikuja baada ya kuondoka nyumbani kwake, kufuatia mzozo wa kifamilia. Muuaji anashikilia wadhifa wa mkuu wa idara ya polisi, ambaye wajibu wake ni kulinda maisha, mali, na heshima, na kuhakikisha faraja na usalama wa jamii, kuondoa shida zake, kudumisha amani kote, na kuwazuia wakjukaji na wavamizi dhidi ya maisha ya watu – sio kumuua bamkwe wake kwa kukusudia kwa kumpiga risasi kwenye barabara ya umma!

Hadi sasa, mamlaka ya Houthi haijatekeleza yale ambayo Mwenyezi Mungu amewajibisha katika kukabiliana na muuaji. Wanamkamata kwa nguvu yeyote wamtakaye kutoka kwa wale wanaowapinga kifikra na kiimani au kutoka kwa wale wanaopinga sera yao ya dhulma, lakini kuhusu wahalifu, wauaji na wavamizi dhidi ya maisha ya watu wanaomwaga damu isiyo na hatia bila haki, hawajali suala lao, kwa sababu wao si wachungaji wa kweli na bado hawajabadilika kutoka kwa fikra ya madhehebu hadi kuwa na mtazamo wa serikali, na wala hawawatazami raia kwa mtazamo wa usawa. Badala yake, msingi wa utawala wao umejengwa juu ya ubaguzi, ushabiki, na ubaguzi wa rangi, pamoja na kucheleweshaji, kuahirisha mambo, na kukwama katika kuwafungulia mashtaka wale wanaofanya uhalifu miongoni mwao. Ushahidi mkubwa wa hili ni kumwacha mhalifu Falyatah chini ya ulinzi wao, na kabla yake muuaji wa Sheikh Ahmad Salim al-Sakani, na mbakaji wa msichana Janat, na wengine wengi... Bila kusahau vitendo vya kuua, kulipua nyumba, kuzingira vijiji, na kupiga watu kwa silaha nzito huko Rada’. Upole wao wa kumkamata muuaji, kwa kutekeleza uhalifu, unaonyesha kwamba kuna mengi zaidi ya jambo hilo kuliko inavyoonekana. Ni lazima wajue kwamba kila mtu yuko sawa mbele ya Shariah ya Mwenyezi Mungu, bila kujali kazi ya muuaji au hadhi yake, na kwamba “Mwenye kucheza na bomu litamlipukia, na atakayeweka sumu atainywa, na anayetegemea kisichokuwa Mwenyezi Mungu, Mwenyezi Mungu atamwadhibu kwacho.”

Je, Mahouthi wanasubiri miaka mingi ipite baada ya kuuawa Sheikh Radman ili Muhammad Ali al-Houthi ayasuluhishe makabila katika kesi za mauaji kama propaganda za kundi hilo?!

Tunajua vyema kwamba Mahouthi hawatafuata usemi maarufu wa Khalifa Rashid Abu Bakr al-Siddiq: “Mwenye nguvu miongoni mwenu ni dhaifu kwangu mpaka nichukue haki kutoka kwake...” katika hotuba yake juu ya kushika Khilafah baada ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw). Basi je Mahouthi wanasemaje kuhusu kauli ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw): «لَوْ أَنَّ فَاطِمَةَ بِنْتَ مُحَمَّدٍ سَرَقَتْ لَقَطَعْتُ يَدَهَا» “Lau Fatima binti Muhammad angeiba ningeukata mkono wake.” (Imepokewa na al-Bukhari na Muslim)

Mahouthi kuyaacha makabila mawili ya muuaji na mwathiriwa kuhamasisha watu wao kwa makabiliano yanayoweza kutokea ni uhalifu mkubwa ambao kwao wanabeba mzigo. Wanaweza kuhukumu kwa kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[وَلَكُمْ فِي الْقِصَاصِ حَيَاةٌ يَاْ أُولِيْ الأَلْبَابِ لَعَلَّكُمْ تَتَّقُونَ]

Mtakuwa nao uhai mzuri katika kulipiza kisasi enyi wenye akili, ili msalimike.” [Al-Baqarah:179]. Na familia ya mwathiriwa lazima ishikamane na kauli yake Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[وَلاَ تَقْتُلُواْ النَّفْسَ الَّتِي حَرَّمَ اللّهُ إِلاَّ بِالحَقِّ وَمَن قُتِلَ مَظْلُومًا فَقَدْ جَعَلْنَا لِوَلِيِّهِ سُلْطَانًا فَلاَ يُسْرِف فِّي الْقَتْلِ إِنَّهُ كَانَ مَنْصُورًا]

Wala msiuwe nafsi ambayo Mwenyezi Mungu amekataza isipo kuwa kwa haki. Na aliye uliwa kwa kudhulumiwa basi tumempa madaraka mrithi wake. Lakini asipite mpaka katika kuuwa. Kwani yeye anasaidiwa.” [Al-Isra:33]. Isipokuwa Mahouthi wakiwa wanataka kufikia malengo mengine na kuifanya hukmu kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu kuwa la mwisho ya malengo yao!

Ni miongoni mwa maafa yaliyorithiwa kutoka kwa tawala hizi za kisekula kwamba masuala ya ugomvi wa damu hutumiwa na mfumo unaotawala kila unapotaka na kutiisha wakati wowote unapotaka. Damu ya wasio na hatia, kwao, ni kwa ajili ya kujadiliana na kutimiza matamanio yao ya kubaki kwenye viti vyao vibovu vya madaraka. Serikali iliyopita ilitumia haya mara kwa mara, na Mahouthi sasa wanafuata njia yake.

Ushawishi wa kikabila nchini Yemen ni mkubwa, na makafiri wa Magharibi wanalifahamu hili. Kwa hiyo, wamefanya kazi kupitia watawala wahalifu kuangamiza ushawishi huu na kuwafisidi viongozi wake kwa pesa. Uingereza, kwa hila na udanganyifu, imefanya kazi kupitia wafalme wa Ghuba kutoa pesa kwa wengi wao. Ama Marekani inajitahidi sana kuyavuruga makabila, kuyagawanya, na kuwaondoa viongozi wake kwa njia mbali mbali: baadhi yao kwa kuwapiganisha wao kwa wao, wengine kwa kuwaundia masheikh wanaoshindana kwa wale walio watiifu kwa Uingereza na vibaraka wake, wengine kwa kuwafukuza katika nchi na kutafuta badali yao, kuwafukarisha na kuwadhalilisha, na kuwaondoa, na kwa kuanzisha uhasama baina yao. Huu ndio uhalisia wa kile kilichotokea na kinachotokea kwa wengi wao. Basi ni lini makabila yatajua yale yanayopangwa kwa ajili yao?!

Sisi katika Hizb ut Tahrir/Wilayah ya Yemen tunakuhutubieni, watu mashuhuri wa makabila ya Bakil na Hashid na makabila yote ya Yemen, ili kufahamu mpango wa kugawanywa, kudhoofishwa, na kuvurugwa unaotekelezwa dhidi yenu, na muitikie wito wa Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[وَاعْتَصِمُواْ بِحَبْلِ اللّهِ جَمِيعًا وَلاَ تَفَرَّقُواْ وَاذْكُرُواْ نِعْمَةَ اللّهِ عَلَيْكُمْ إِذْ كُنتُمْ أَعْدَاء فَأَلَّفَ بَيْنَ قُلُوبِكُمْ فَأَصْبَحْتُم بِنِعْمَتِهِ إِخْوَانًا وَكُنتُمْ عَلَىَ شَفَا حُفْرَةٍ مِّنَ النَّارِ فَأَنقَذَكُم مِّنْهَا كَذَلِكَ يُبَيِّنُ اللّهُ لَكُمْ آيَاتِهِ لَعَلَّكُمْ تَهْتَدُونَ]

Na shikamaneni kwa Kamba ya Mwenyezi Mungu nyote pamoja, wala msifarikiane. Na kumbukeni neema ya Mwenyezi Mungu iliyo juu yenu: vile mlivyo kuwa nyinyi kwa nyinyi maadui naye akaziunganisha nyoyo zenu; kwa neema yake mkawa ndugu. Na mlikuwa ukingoni mwa shimo la Moto, naye akakuokoeni nalo. Namna hivi Mwenyezi Mungu anakubainishieni Ishara zake ili mpate kuongoka.” [Aal-i-Imran:103]. Na kushikamana na wito wa Mtume (saw): «مَا بَالُ دَعْوَى الْجَاهِلِيَّةِ؟»  Kisha akasema: «دَعُوهَا فَإِنَّهَا مُنْتِنَةٌ» “Je, kuna nini juu ya mwito wa Kijahiliyah? Uacheni hakika huo ni uvundo” (Imepokewa na al-Bukhari)

Enyi Ndugu: Acheni miito ya kupigana na zuieni njia ya Shetani inayohalalisha damu ya wenzenu. Muuaji lazima akabidhiwe kwa hukmu ya Mwenyezi Mungu itekelezwe juu yake. Lazima mutambue kwamba watawala waliotangulia na wa sasa huko Kaskazini na Kusini mwa Yemen ni waajiriwa wa Makafiri wa Magharibi, wakitekeleza mifumo yake ya kisekula na kumregelea mkruseda Umoja wa Mataifa, wakati Kitabu cha Mwenyezi Mungu kiko mikononi mwetu kikipuuzwa, hakiregelewi isipokuwa katika kisomo kisichovuka koo za wale wanaokihifadhi. Nyinyi wenye uwezo wa kuzipindua tawala za vibaraka na kusimamisha utawala wa Uislamu mahali pao, lazima muifanye sheria ya Mwenyezi Mungu kuwa hukmu baina yenu, iregeleeni, zikataeni sheria za kikafiri na njama za maadui, na muwanusuru wale wanaofanya kazi ya kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, kama Aws na Khazraj walivyomsuru Mtume wa Mwenyezi Mungu mjini Yathrib, kwamba miongoni mwenu awepo Sa’d ibn Mu’adh (ra) ambaye kwa kifo chake Arshi ya Mwingi wa Rehema ilitikisika na Malaika sabiini elfu walihudhuria mazishi yake.

Watoto wenu kutoka makabila ya Bakil na Hashid wako katika sehemu zote za dola hii na katika viwanja vyote vya mapigano nchini Yemen, na hata wakiwa katika nyadhifa za uongozi katika vikosi vya jeshi na usalama. Wana uwezo wa kuwafagilia mbali watawala hawa na kusimamisha utawala wa Uislamu.

Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen inawataka watu wenye imani na hekima kufanya kazi nayo ili kuregesha mfumo kamili wa maisha wa Kiislamu na kuhukumu kwa yale yote aliyoyateremsha Mwenyezi Mungu kwa kusimamisha Khilafah Rashidah ya pili kwa njia ya Utume, ambayo itatekeleza Uislamu miongoni mwao na kuziunganisha ardhi za Waislamu chini ya Rayah (bendera) ya ‘Uqab. Hizb ut Tahrir, inayojulikana na wengi wenu, ina mbinu nzuri, njia iliyonyooka, uwezo na umahiri, na katiba iliyotabanniwa tayari kwa ajili ya kutekelezwa—iliyotokana na Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah za Mtume Wake (saw)—kuanzia siku ya kwanza ya kutangazwa dola. Inafanya kazi miongoni mwenu na pamoja nanyi kwa lengo hili kubwa, na inafanya kazi katika nchi zaidi ya arubaini duniani kote, ikiwemo Yemen, kwa imani, ikitafuta malipo, mapambano, na kujitahidi mpaka yapatikane yale aliyoamrisha Mwenyezi Mungu (swt) yapatikane, na ina watu ambao wamekuwa wakweli kwa yale waliyomuahidi Mwenyezi Mungu mpaka ushindi wa Mwenyezi Mungu upatikane.

Amesema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[يَا أَيُّهَا الَّذِينَ آمَنُواْ اسْتَجِيبُواْ لِلّهِ وَلِلرَّسُولِ إِذَا دَعَاكُم لِمَا يُحْيِيكُمْ وَاعْلَمُواْ أَنَّ اللّهَ يَحُولُ بَيْنَ الْمَرْءِ وَقَلْبِهِ وَأَنَّهُ إِلَيْهِ تُحْشَرُونَ]

“Enyi mlio amini! Muitikieni Mwenyezi Mungu na Mtume anapo kuitieni jambo la kukupeni uzima wa milele. Na jueni kuwa Mwenyezi Mungu huingia kati ya mtu na moyo wake, na kwamba hakika kwake Yeye tu mtakusanywa.” [Al-Anfal:24].

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 735417068
http://www.hizb-ut-tahrir.info
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.