Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Wilayah Yemen

H.  17 Jumada I 1447 Na: HTY- 1447 / 08
M.  Jumamosi, 08 Novemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Kwa Kuongezeka kwa Ajali za Barabarani, Pindi Uchungaji unapokuwa Haupo na Kubadilishwa na Kulaumu na Kurushiana Lawama!

(Imetafsiriwa)

Mnamo Jumatano, 5 Novemba 2025, ajali mbaya ya barabarani ilitokea katika Barabara ya Al-Arqoub katika wilaya ya Shuqra, jimbo la Abyan, kusini mwa Yemen, ambayo ilisababisha kuchomeka kwa basi la usafiri wa umma lililokuwa njiani kuelekea Aden, likitoka mji wa Jeddah, mali ya Kampuni ya Saqr Al-Hijaz, na lililokuwa limebeba abiria 42.

Ajali hiyo ilitokea wakati basi hilo lilipogongana na gari jengine kutokana na wembamba na hali mbaya ya barabara. Cha kusikitisha, kutokuwepo kwa vizima-moto kulisababisha moto kuwaka kwa masaa manne mfululizo na kuwazuia abiria kutoroka kutoka basi hilo. Kutokana na ajali hii mbaya, furaha ya familia 17 za marehemu ilizimwa. Furaha yao ilibadilishwa na huzuni, na vigelele vya furaha vya kuwasili kwao vilibadilishwa na machozi kwa kufiwa na wapendwa wao waliokuja kuwatembelea. Nyoyo za familia saba zilivunjika walipoona jamaa zao waliojeruhiwa na kuchomeka moto katika vitanda vya hospitali. Kilichowasukuma waathiriwa hawa kuvumilia magumu ya usafiri na maumivu ya kutengana na familia zao ni haja yao kubwa katika nchi ambayo huduma imezorota na watu wake wanalazimika kufanya kazi mbali. Hii ni kwa sababu utajiri wa nchi hii huenda kwa wakoloni makafiri jijini London na Washington, ambapo watoto wao wanaufurahia, huku Waislamu nchini Yemen wakiishi katika taabu na unyonge!

Mamlaka rasmi hazikufika hadi saa 10:00 AM, masaa saba baada ya ajali! Hawa ni wachungaji wa aina gani?! Mamlaka zilikana kuwajibika kwa ajali hiyo, zikitoa visingizio mbalimbali na kuwalaumu waathiriwa kwa kuendesha gari kwa kasi, uzembe wakati wa kuendesha gari, upitaji hatari wa magari, na kuendesha gari dhidi ya mtiririko wa trafiki. Ili kutuliza rai jumla ya umma, Rashad al-Alimi, katika maongezi mawili ya simu na gavana wa Abyan na Waziri wa Afya, alitoa maagizo dhaifu ya kusaidia familia za waathiriwa, kuwezesha uhamishaji wa kesi za dharura hadi hospitalini kwa matibabu, kufanya ukarabati wa mara kwa mara kwenye barabara za umma, na kuongeza hatua za usalama barabarani ili kupunguza kujirudia kwa ajali!

Pande mbili zinahusika na uwajibikaji kwa janga hili na kutokea kwake. Wa kwanza ni: Kampuni ya mabasi, ambayo ilishindwa kutoa vifaa vya usalama kwenye magari yake na kupuuza majukumu yake ya ukarabati. Uzembe huu ulisababisha basi kushika moto kabla ya ajali, kulingana na manusura aliyezungumza baada ya kupelekwa hospitalini. Wa pili ni Baraza la Rais, kutokana na usimamizi wake duni, ikiwemo upanuzi na ukarabati duni wa barabara, na ukosefu wa vifaa vya huduma ya kwanza kwenye barabara kuu. Ajali za barabarani nchini Yemen zinachukua uhai mwaka mzima. Data rasmi zinaonyesha kuwa ajali za barabarani katika maeneo ya udhibiti wa Baraza la Rais zilisababisha vifo 64 na zaidi ya majeruhi 290 mwezi uliopita pekee. Lau ajali hii isingekuwa ya kutisha sana na isiyofichwa kwa siri kama zile zilizopita, isingeonekana.

Utawala wa Uislamu ni tofauti kabisa na utawala wa leo. Amiri wa Waumini, Umar ibn al-Khattab (Mwenyezi Mungu awe radhi naye), alisema, “Kama nyumbu angejikwaa Iraq, ningeogopa kwamba Mwenyezi Mungu angeniuliza kuhusu hilo: ‘Kwa nini hukuitengeneza barabara, ewe Umar?’” Hatujawahi kuona watawala wabaya zaidi kuliko watawala hawa wa Yemen. Wao ni wezi na watumwa wa wakoloni makafiri kwa kila maana ya neno. Hakuna hata nyumba moja katika nchi hii iliyoathiriwa ambayo haijapata mateso kutokana na uovu na upotovu wao. Matendo yao ni mabaya kiasi gani!

Enyi Watu Wetu, Watu wa Imani na Hekima: Mateso yenu yataendelea hadi lini huku mkibaki kimya na bila kufanya kazi dhidi ya utawala ambao haujali shida zenu na majanga na misiba inayowapata? Kwa nini msiungane na kufanya kazi pamoja na Hizb ut Tahrir ili kung'oa utawala huu, kuutupa kwenye kaburi la sahau, na kuubadilisha na Khilafah Rashida ya pili, iliyosimamishwa kwa njia ya Utume?

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Yemen

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
Address & Website
Tel: 735417068
http://www.hizb-ut-tahrir.info
E-Mail: yetahrir@gmail.com

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.