Afisi ya Habari
Wilayah Yemen
| H. 10 Dhu al-Hijjah 1447 | Na: HTY- 1447 / 20 |
| M. Jumatano, 27 Mei 2026 |
Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Ufisadi wa Mfumo Huzalisha Ufisadi katika Masuluhisho
Sera ya Ufukarishaji: Zawadi ya Idd al-Adha kutoka kwa Watawala kwa Watu wa Yemen
(Imetafsiriwa)
Serikali ya Shaea Al-Zandani mnamo Jumanne, 19/05/2026, ilianzisha hatua mpya ya kiuchumi ambapo ilipandisha bei ya dolari ya ushuru wa forodha kwa zaidi ya 100%, kutoka riyali 750 hadi riyali 1,550, na kuongeza bei ya chombo cha dizeli cha lita 20 kwa 24.5%, ikiruka kutoka riyali 29,500 hadi 36,000. Kisha ilijaribu kuwaziba macho watu wa Yemen kwa kuidhinisha posho ya gharama ya maisha ya 20% kwa wafanyikazi wa sekta ya umma, pamoja na kuwapa nyongeza yao ya kila mwaka inayostahili kwa miaka ya 2021-2024, na kufanya marekebisho ya viwango vya kazi ambayo yalikuwa yamesimamishwa kwa zaidi ya miaka 13.
Hizi zilikuwa hatua za kwanza zilizochukuliwa na Wizara ya Shaea Al-Zandani tangu kuundwa kwake baada ya matukio ya kijeshi yaliyoshambulia kusini mwa Yemen mwanzoni mwa 2026, matukio ambayo yalisababisha Aidarous Al-Zubaidi kukimbilia Abu Dhabi mnamo Januari 2026. Je, hii ni zawadi kweli kwa watu wa Yemen kwa mnasaba wa Idd al-Adha iliyobarikiwa?
Ni uzembe wa aina gani huu? Kupuuza mateso ya watu! Wanapandisha bei mara nyingi, kisha huwatupia watu mabaki ambayo hayatoshi kudumisha familia hata kwa siku chache, kana kwamba wanawafanyia watu ihsani waliochoka na njaa, umaskini, na uchochole.
Hili ni ongezeko la tatu la bei ya dolari ya ushuru wa forodha: kutoka riyali 250 hadi riyali 500 mnamo Julai 2021, kisha kutoka riyali 500 hadi riyali 750 mnamo Januari 2023. Je, hatua yoyote kati ya hizi ilileta manufaa kwa maisha ya watu? Au kinyume chake, je, hazikusababisha madhara makubwa kutokana na kupanda kwa bei pamoja na kupanda kwa dolari, ambayo leo ni sawa na riyali 1,550, pamoja na kupanda kwa bei ya dizeli na petroli mwezi uliopita, ambayo yote husababisha ongezeko la jumla la bei za bidhaa na huduma? Je, ongezeko la 20% linaweza kukabiliana na kupanda kwa bei za mahitaji ya msingi? Na kisha ni nani atakayewahudumia watu ambao si wafanyikazi wa serikali na ambao hawatapokea ongezeko hili lolote? Sera hizi zinakuja baada ya benki kuu kushindwa kupata pesa taslim ambazo zingewezesha wizara ya Shaea Al-Zandani kulipa mishahara ya wafanyikazi wa sekta ya umma, jeshi, na huduma za usalama, na kutimiza majukumu yake kwa wale walio chini ya uangalizi wake.
Hatujui ni kwa nini kuna msisitizo kama huo wa sera za kiuchumi za kibepari zinazoendelea ambazo zilianza kabla ya kuanza kwa karne mpya, zilizoharibu riziki na rasilimali, na hazijafanikiwa kubadilisha hali ya maisha ya watu kuwa bora, sembuse kuboresha uchumi ambao hali yake inazidi kuwa mbaya siku baada ya siku. Hatua hizi zinazorudiwa zinazolazimishwa na wizara mtawalia za serikali inayoitwa “uhalali” zinafanywa na Mfuko wa Fedha wa Kimataifa, ambao umejitokeza tena baada ya kutokuwepo kuchukua jukumu la uchumi wa kusini mwa Yemen kwa lengo la kuuharibu, si kuurekebisha, na kudhibiti utajiri na rasilimali za nchi. Haya ni maagizo maovu ya kibepari yaliyokusudiwa udhibiti zaidi juu ya ardhi hii na watu wake.
Katika onyesho lisilo la kawaida la kutojali hali mbaya ya maisha, mkuu wa baraza la watu wanane, siku tatu tu baada ya kuongeza bei ya dolari za ushuru wa forodha na dizeli, aliwapongeza watu wa imani katika Siku ya Umoja wa Yemen—wakati wanakufa kutokana na njaa, wamekandamizwa na kupanda kwa bei, wamezidiwa na migogoro, na wanatazama huduma zikiporomoka mbele ya macho yao, huku wenye nguvu wakiishi katika anasa na ufadhilishwaji. Wengi wao hata wanaishi na familia zao nje ya nchi huku watu wakibeba maumivu.
Enyi watu wetu nchini Yemen kwa jumla, na haswa katika maeneo yaliyo chini ya serikali ya Al-Zandani: watawala hawa hahisi mateso yenu, wala hawahisi maumivu yenu. Wanaishi katika minara ya pembe za ndovu. Kiwango chao cha maisha si kama chenu. Mishahara yao ni ya fedha za kigeni na mara nyingi zaidi kuliko yenu, mishahara ambayo hutoweka mikononi mwenu mara tu munapoipokea. Hali itabaki kama ilivyo hadi mutakapoamka na kile tunachokulinganieni muelewe, na kutofautisha kati ya mfumo wa uchumi wa kibepari ambao umekuharibuni na mfumo wa kiuchumi katika Uislamu, ambao ulimfanya mtawala kuwa mchungaji anayewajibika kwa wale walio chini ya uangalizi wake, si mtoza ushuru anayewapora na kuongeza umaskini wao.
Kwa upande mwingine, watu wa Yemen wanaoishi chini ya udhibiti wa Mahouthi hawako katika hali nzuri zaidi. Badala yake, serikali zote mbili zinashindana katika jinsi zilivyo na madhara. Hazijajiwekea mipaka katika sera za umaskini na njaa, lakini zimeharibu kila kipengee cha maisha, na kuifanya Yemen isiweze kustahimiliwa kuishi ndani yake: kuanzia umaskini na njaa, hadi hofu na kifungo, hadi kuporomoka kwa huduma, na zaidi ya yote, kuondoa sheria ya Mwenyezi Mungu na kuhukumu kwa njia nyingine isiyokuwa ile aliyoiteremsha Mwenyezi Mungu (swt). Hili ni wazi kwa yeyote mwenye kuona na kufahamu. Ni uovu ulioje wanayofanya.
«مَا مِنْ وَالٍ يَلِي رَعِيَّةً مِنَ الْمُسْلِمِينَ فَيَمُوتُ وَهُوَ غَاشٌّ لَهُمْ إِلَّا حَرَّمَ اللَّهُ عَلَيْهِ الْجَنَّةَ»
“Hakuma WALI (mtawala) yeyote ambaye ameteuliwa juu ya Waislamu atakaye kufa nah uku akiwadanganya isipokuwa Mwenyezi Mungu amemharamishia Pepo.”
Na Hizb ut Tahrir, Kiongozi asiyewadanganyi watu wake inakulingamieni kufanya kazi nayo kwa ajili ya kusimamisha Khilafah Rashida ya pili kwa njia ya Utume, ambayo viongozi wake hawataridhika hadi watu watakaporidhika mbele yao.
«اللَّهُمَّ مَنْ وَلِيَ مِنْ أَمْرِ أُمَّتِي شَيْئاً فَشَقَّ عَلَيْهِمْ فَاشْقُقْ عَلَيْهِ، وَمَنْ وَلِيَ مِنْ أَمْرِ أُمَّتِي شَيْئاً فَرَفَقَ بِهِمْ فَارْفُقْ بِهِ»
“Ewe Mwenyezi Mungu, yeyote utakayetawalishwa mambo ya Umma wangu chochote akawadhikisha nawe mdhikishe, na yeyote atakayetawalishwa mambo ya Umma wangu chochote akawafanyia wepesi nawe mfanyie wepesi.”
Khilafah pekee ndiyo itakayouokoa Umma huu, kueneza kheri, kutoa mahitaji msingi kwa wale walio chini ya uangalizi wake, na kuwawezesha kupata utulivu na riziki. Lakini leo, chini ya watawala madhalimu, hali zinaendelea kuwa mbaya zaidi siku hadi siku.
[وَمَنْ أَعْرَضَ عَنْ ذِكْرِي فَإِنَّ لَهُ مَعِيشَةً ضَنْكًا]
“Na atakaye jiepusha na mawaidha yangu, basi kwa yakini atapata maisha yenye dhiki.” [Surat Taha:124]
Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir
katika Wilayah Yemen
| Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari Wilayah Yemen |
Address & Website Tel: 735417068 http://www.hizb-ut-tahrir.info |
E-Mail: yetahrir@gmail.com |