Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

 Dola ya Kiislamu, Ukafiri wa Wazi na Dar ul Kufr

(Imetafsiriwa)

Fahamu ya utawala sio suala la muundo wa kisasa. Ni la zamani kama ilivyo fahamu ya mujtamaa. Mujtamaa muda wote zilihitaji kusimamiwa, ambapo hilo linawezekana tu kupitia mamlaka au utawala wa sheria. Mamlaka kama hayo yalipatikana muda wote kupitia historia, ima kupitia machifu wa kikabila, kama ilivyokuwa kipindi cha nyuma, au mamlaka ya dola za kitaifa kama ilivyo katika wakati wetu wa sasa. Watu kimaumbile huwa wanahitajia kiongozi watakaye mtii. Kwa kweli, utiifu ni moja ya sifa muhimu sana kwa wanadamu. Utiifu hujidhihirisha wenyewe kuanzia utotoni kwa sura ya utiifu kwa wazazi ambapo watoto huwazingatia kuwa ni wenye kuwatakia kheri. Matukio ya kihistoria yaliopokelewa katika Quran Tukufu, ambacho ni chanzo sahihi zaidi cha kihistoria kilichoshushwa kupitia wahyi, yanaonyesha wazi uwepo wa watawala katika nyakati hizo. Basi kwa vipi Uislamu, ukiwa ni mfumo kamili wa maisha uliokamilika, isitoe miongozo na sheria juu ya kile kilicho cha uhalisia zaidi kwa watu katika maisha yao ya pamoja, sheria zenye kutumika kwa kipindi chote kijacho? Kwa kweli, katika uhalisia, aya nyingi za Quran na Hadith kwa namna ya kipekee zimeshughulika na suala la mamlaka na utawala. Nususi mara nyingi zinatumia istilahi kama sultan, hukm na mulk zikikusudia mamlaka na utawala. Matamshi yote haya ni yenye kuhusiana katika maana, na yanakusudiwa kuwa ni uwezo au mamlaka ya kulazimisha hukmu. Neno hukm humaanisha maamuzi au hukumu na hakim ni mtawala anayelazimisha hukumu. Pia, tunaona maneno mengine kama amir, imarah, imam na khalifah katika nususi.

Tamko الدَولَۃ الاِسلامیة lina maana ya dola ya Kiislamu. Neno riyasat (dola) katika lugha ya Kiurdu linatokana na maneno ya Kiarabu ras na rais. Neno rais lina maana ya kiongozi au chifu. Kwa mfano, Abdullah bin Abi Salul anajulikana kama ni rais ul Munafiqiin (yaani chifu au kiongozi wa Wanafiki). Japokuwa tamko la dola ya Kiislamu mara nyengine hutumika kama Khilafah, vyanzo vya sheria ya Kiislamu na vitabu vya fiqhi havitumii tamko la dola ya Kiislamu kwa maana ya Khilafah. Badala yake, wanavyuoni hutumia dar ul Islam kumaanisha mamlaka ya Kiislamu katika mahusiano yake na dola nyenginezo za dar ul Harb. Sababu ni kuwa matamshi haya ni mapana na yenye maana sana kwa upande wa vidokezi vyake na matokeo yake. Matamshi haya yanaelezea uhalisia maalum unaopatikana katika Shariah; yaani, yanagusia uhalisia ambao tayari upo katika Shariah na sio kitu ambacho kimebuniwa na wanazuoni wenyewe. Hivyo, dar ul Islam moja kwa moja humaanisha Khilafah, isipokuwa katika wakati ambapo wilaya yake yoyote inapokuwa katika uasi. Hata hivyo, hukmu juu ya wilaya zilizo asi ni kuwa zinahitajiwa tena kuwa sehemu ya Khilafah kwa kipindi cha karibuni au kwa baadaye. Aya hii kutoka kwa Mwenyezi Mungu (swt) pia inatilia nguvu uhalisia wa Kisharia wa dar ul Islam:

[وَعَدَ اللّٰهُ الَّذِیْنَ اٰمَنُوْا مِنْكُمْ وَ عَمِلُوا الصّٰلِحٰتِ لَیَسْتَخْلِفَنَّهُمْ فِی الْاَرْضِ كَمَا اسْتَخْلَفَ الَّذِیْنَ مِنْ قَبْلِهِمْ۪-وَ لَیُمَكِّنَنَّ لَهُمْ دِیْنَهُمُ الَّذِی ارْتَضٰى لَهُمْ وَ لَیُبَدِّلَنَّهُمْ مِّنْۢ بَعْدِ خَوْفِهِمْ اَمْنًاؕ-یَعْبُدُوْنَنِیْ لَا یُشْرِكُوْنَ بِیْ شَیْــٴًـاؕ-وَ مَنْ كَفَرَ بَعْدَ ذٰلِكَ فَاُولٰٓىٕكَ هُمُ الْفٰسِقُوْنَ]

“Mwenyezi Mungu amewaahidi wale walioamini miongoni mwenu na wakatenda mema, ya kwamba atawafanya Makhalifah katika ardhi kama alivyowafanya Makhalifah wa kabla yao, na kwa yakini atawasimamishia Dini yao aliyowapendelea, na atawabadilishia amani baada ya khofu yao. Wawe wananiabudu Mimi, wala wasinishirikishe na chochote. Na watakao kufuru baada ya hayo, basi hao ndio wapotovu.” [Surah An-Nuur 24:55]. Aya hii inataja vitu viwili: (1) kuisimamisha Dini na (2) kuibadilisha hofu kwa amani. Na haya kwa kweli ndio masharti mawili ya dar ul Islam, yaani, utekelezaji wa Uislamu na mamlaka kwa Waislamu. Matamshi ya dar ul Islam yalikuwa maarufu wakati wa Maswahaba.

Imam Abu Yusuf katika kitabu chake Kitab ul Kharaj alichapisha mkataba ulioandikwa kuwa Khalid bin Walid (ra) aliwekeana na watu wa Hira, أیُّما شیخ ضعف عن العمل، أو أصابتہ آفۃ من الآفات، او کان غنیاً فافتقر، وصار أھلُ دینہ یتصدَّقون علیہ طُرِحَت عنہ جزیتہ، و عِیلَ من بَیتِ مالِ المسلمین، و عیالُہ، ما أقام بدار الھجرۃ و دارالاسلام، فان خرجوا الی غیر دارالھجرۃ و دارالاسلام فلیس علی المسلمین النفقۃ علی عیالھم  “Mzee mtu yeyote asiyeweza kufanya kazi, au akapatwa na maradhi, au alikuwa tajiri kisha akawa fukara na ikawa watu wa dini yake wanampatia msaada, jizya huondolewa kwake, na mahitaji yake na ya familia yake yatatoka katika Bayt ul Mal ya Waislamu muda wa kwamba anaishi katika dar ul Hijra na dar ul Islam. Na pindi akitoka nje ya dar ul Hijra na dar ul Islam basi mahitaji yao hayatokuwa juu ya Waislamu.”

Licha ya istilahi hizi, uhalisia wa dola yoyote kwa kawaida ni kuwa انها كيان تنفيذي لمجـمـوعـة المفاهيم والمقاييس والقناعات التي تقبلتها مجموعة من الناس “Ni umbo la utekelezaji mjumuiko wa fahamu, vigezo na makinaifu ambayo hutabanniwa na pote la watu.” Kwa maana nyengine, wakati kundi la watu linaloishi katika eneo fulani linapofuata mjumuiko wa fikra, vigezo na makinaifu, dola huzaliwa. Hii inaweza kuwa ni dola ndogo kama Madinah au dola iliyovuka mipaka ya bara kama Muungano wa Kisovieti, dola ya himaya, jamhuri ya kidemokrasia, Dola ya Kiislamu au baadhi ya dola nyengine zilizoegemea kwenye ukafiri.

Fahamu ya dola ya Kiislamu inatafautiana kwa namna nyingi na fahamu ya dola za kimaeneo, ambayo kihistoria huwa zaidi imechipuka kutoka kwenye elimu za Kimagharibi na utaratibu wa kisiasa, kuliko kutoka kwenye Uislamu. Fahamu ya dola za kisasa za kimaeneo ni kitu ambacho Wamagharibi wamekieneza duniani kote kwa mamia ya miaka. Kwa miongo kadhaa iliyopita, Amerika imekuwa ikijaribu kuitilia nguvu zaidi fahamu hii kupitia Umoja wa Mataifa na taasisi nyengine kadhaa. Kwa Wamagharibi, dola kimsingi ni kipande cha ardhi ambapo watu na serikali yao wanaishi kwa kudumu. Kwa hiyo dola kwao wao ni nchi au nchi asili zenye mipaka maalum, na ambapo mamlaka yapo kwa watu wanaoishi hapo. Pia, serikali ni ya kijumuiya na sio ya kibinafsi. Hivyo nchi, watu wake na watawala wake wanaunda dola. Kinyume na hivi, katika Uislamu dola hazina mipaka ya kudumu kwa sababu ujumbe wa Uislamu lazima usambae duniani kote, ili mamlaka ya Uislamu yaenee kwenye maeneo mengine, mipaka pia lazima itanuke. Neno watan kimsingi linaashiria mahala ambapo mtu anaishi kwa kudumu, yaani, nyumba yake na mtaa wake. Mamlaka kamili yapo kwenye Shariah na sio kwa watu, watawala na watu wote wanalazimika kwayo. Pia, utawala katika Uislamu ni wa mtu mmoja mmoja na sio wa jumuiya. Na kwa hivyo mtawala – aitwaye khalifah – ana nguvu zote zihusianazo na utawala, kwa hivyo khalifah kimsingi ni dola.

Kwa sababu ya tafauti hii katika fahamu ya dola, baadhi ya Waislamu wanaelemea katika kuamini kuwa kutumia neno “dola ya Kiislamu” kumaanisha Dar ul Islam au Khalifah sio sawa kwa sababu dola ni kitengo cha mpango wa dunia wa Kimagharibi. Hii sio sahihi. Neno ‘dola’ lenyewe ni istilahi isiyoegemea kokote inayohitaji sifa fulani. Inaweza kukusudiwa mji wenye hadhi ya dola wa Ugiriki au dola ya himaya ya Roma, au inaweza kuwa ni dola ya kikabaila au ya kisoshalisti, au dola ya Kiislamu au ya kitaifa. Hii ni sawa na neno ‘sheria’ (law), ambalo pia ni istilahi ya Kimagharibi, lakini inaweza kutumiwa katika muktadha wa Uislamu pia, kwa kuwa kimsingi inamaanisha hukmu ambayo inashurutishwa na mamlaka, ambayo ni fahamu inayopatikana kwenye Uislamu vilevile. 

Suala moja linazuka hapa nalo ni, kwa kuwa dola ya Kiislamu pia inasimamishwa kwenye eneo na lina wakaazi wake, je haiwi sawa na dola ya kisasa ya Kimagharibi ya kieneo? Jibu ni kwamba sio hivyo. Dola ya kitaifa ya Ujerumani muda wote itajifunga na ardhi ya Ujerumani na watu wake, ikiwa na mji mkuu katika ardhi ya Ujerumani. Hata hivyo, dola ya Kiislamu muda wote inatanuka na haijifungi na ardhi au kabila. Ndio utaona mji mkuu wa Khilafah ulipatikana katika maeneo tafauti katika zama tafauti, ima Madinah, Baghdad au Istanbul.

Kundi la waliberali wa Pakistan wanaonyesha kuwa fikra angavu kuhusu dola inatokana na Wamagharibi. Hii ni kwa sababu wanazingatia kuwa dola ya kisasa ni ile inayoendana na fahamu ya dola ya kieneo ambayo muundo wake unaegemea juu ya falsafa ya kisiasa kwa ajili ya utawala. Ikiwa dola haina baraza la wawakilishi linalowakilisha nguvu ya watu na kama hakuna mgawanyo wa mamlaka ya bunge, mahakama na serikali, basi itakuwa kama dola isio na uasili kama falme zilizopita ambazo hazitimizi matakwa ya hivi leo. Kwa kuwa ufahamu wao wa Uislamu ni wa kijuujuu tu umewapelekea kufikiria kuwa muundo huu wa kitaasisi umekosekana, wamehitimisha kuwa nidhamu ya utawala ya Kiislamu ni nidhamu ya kale yenye kufaa kwa ajili ya jamii za kikabila tu, lakini pia haikutimiza matakwa ya dunia ya kisasa.

Hata hivyo, ukweli ni kuwa uendaji sambamba wa mamlaka ya taasisi katika dola za kidemokrasia za kisasa na mgawanyo changamani wa nguvu za mamlaka kwa kweli umepelekea matatizo na mizozo lukuki. Hii inaonyesha kutoweza kwa akili ya binadamu kutoa nidhamu inayoweza kusimamia mambo ya watu. Hata hivyo, kiburi cha urazini wa Wamagharibi kinazuia ufahamu wa ukweli huu. Tatizo hili liko kama lile la nidhamu ya kiuchumi ya Wamagharibi, ambayo katika ufahamu wake na utekelezaji wake huwa ni mgumu sana na wenye kuingiliana. Hata hivyo, wanauchumi wa kirasilimali hawawezi kuona kwamba sababu ya ugumu huu sio kutokana na akili ya mwanadamu kwamba imejiingiza kwenye kitu cha kutatanisha, bali ni kwa sababu ya kutoweza kupanga mambo ya kiuchumi ya watu.

Wale walioathiriwa na usasa wa Kimagharibi nchini Pakistan wanaamini kuwa Uislamu hautoi fikra ya kudumu ya hukmu na utawala, wala hilo sio lengo lake. Wanaamini kuwa ilikuwa ni bahati tu kwamba Mtume (saw) amekuwa mtawala wa Madinah, kwa kuwa wengi ya Mitume (as) kabla yake hawakusimamisha dola. Wanasema pia kuwa kutosimamisha dola hakujawazuia Mitume (as) kutangaza kile walichoteremshiwa na Mwenyezi Mungu (swt) kwa watu. Wanadai kuwa jukumu la Mitume (as) ni kufikisha tu Wahyi na sio kutawala. Wanasema pia kuwa Uislamu wa kisiasa ni ubunifu wa wanafikra wa Kiislamu wa sasa wakati Waislamu waliposimama dhidi ya ukandamizaji na uvamizi wa Makafiri na kuanza kuunganisha suluhisho lao kwa matatizo wanayoyakabili Waislamu ulimwenguni na kukosekana kwa utabikishaji wa Uislamu kama utawala wa sheria. Wanasema, fikra hizi baadaye zilienea kwa haraka miongoni mwa jamii za Waislamu kwa kiwango ambacho imekuwa kawaida kwa Waislamu kufikiria kuwa kusimamisha dola ya Kiislamu ni moja ya maagizo ya dini.

Jaribio la mwanzo kubwa la kukataa wazo la kuwa Uislamu unayo fikra ya dola lilifanywa na Ali Abdul Razzaq, msomi wa Chuo Kikuu cha Al-Azhar, mwaka mmoja baada ya ushawishi wa Uingereza kuiangusha Khilafah, alipoandika kitabu mnamo 1925 chenye jina al-Islam wa usul al-hukm (Uislam na Misingi ya Utawala). Katika kitabu hiki alitetea hoja ya kuwa Uislamu hautoi nidhamu yoyote ya utawala. Haikushangaza kuwa mwanafunzi huyu wa Muhammad Abdu hatimaye alichaguliwa kuwa mkuu wa Chuo Kikuu cha Al-Azhar nchini Misri!

Wanafikra wa kisasa pia wanakataa istilahi dar ul Islam na dar ul Harb, wakidai kuwa istilahi hizi zimeundwa na baadhi ya wanazuoni kuelezea hali za wakati wao. Hata hivyo, kauli hii haiangalii ukweli wa kuwa wanazuoni wanaunda istilahi kuelezea fikra maalum. Fikra haiji kwa sababu ya istilahi. Lakini, fikra hii tayari inapatikana miongoni mwa vyanzo vinavyotokana na Uislamu. Mfano wa hili ni istilahi ya hadith sahih na dhaif. Fikra ya mamlaka katika Uislamu, na hukmu mbalimbli zinazoihusu, kama hukmu zinazohusiana na mahusianao ya mamlaka hii pamoja na wasiokuwa Waislamu, tayari zinapatikana katika nususi za kishariah na sio matokeo ya kubuniwa kwa istilahi kama dar ul Islam na dar ul Harb. Zaidi ya hivyo ni kuwa istilahi dar ul Islam, dar ul Shirk, dar ul Muhajiriin tayari zipo kwenye hadith mbalimbali na zilikuwa zikitumika mara kwa mara wakati wa Maswahaba, japokuwa wanazuoni walijadili zaidi kwa undani na wakazitolea hukmu kwa upana. Sababu ya wanafikra wa kisasa kuzikataa istilahi hizi ni kuwa wanataka kukataa ukweli wa kuwa Uislamu ni mfumo kamili wa maisha. Kwao wao, dola iliyoegemea itikadi ya Waislamu pekee bila ya uingiliaji kutoka kwa makafiri ni jambo la uongo kwao. Sababu nyengine ya kuziwacha istilahi hizi ni kuwa wanataka kuikataa fikra ya muendelezo na upanuzi wa jihad. Hii ni kwa sababu kuigawa dunia katika dar ul Islam na dar ul Harb inafungua mjadala wa dola ya Kiislamu kupigana jihad na kuzigeuza dar ul Harb kuwa dar ul Islam. Kwa mujibu wa wanafikra wa kisasa, kwa kuwa dola za kikafiri zilizoizunguka dola ya Kiislamu wakati huo kwa kawaida walikuwa katika vita na Waislamu, wanazuoni walitangaza maeneo yote hayo kuwa dar ul Harb. Kwa hivyo wakadai kuwa, haikumaanisha kwamba kuna vita vya kuendelea na kudumu baina ya Waislamu na Makafiri ambavyo vinapaswa kuendelea hadi dunia yote igeuzwe kuwa dar ul Islam.

Hata hivyo, Ummah, uwe ni Waarabu au wasiokuwa Waarabu, umeendeleza juhudi zao za kuweka utawala safi ulio juu ya msingi wa Uislamu, kuachana na ushawishi wa fikra za usasa za Wamagharibi ambazo ni ngeni kwa Uislamu. Mjadala hivi leo baina ya Ummah na Wanazuoni wake sio katika suala la ima Uislamu unayo fikra ya utawala na mamlaka ama la, bali ni juu ya kuamua kama dola maalum imegeuka kutoka kuwa ya Kiislamu na kuwa si ya Kiislamu, na njia gani zitumike kuirejesha kuwa ya Kiislamu. Mfano, Syed Abul-Ala Maududi alifanya mjadala huu wa mageuzi ya dola ya Kiislamu kuelekea kuwa isiyo ya Kiislamu katika Khilafat o Malookiat, na kuhitimisha kuwa dola chini ya Umayya haikuwa Khilafah sahihi. Kipindi cha mwanzo na cha pili cha utawala wa Taliban Afghanistan pia kiliwasha mjadala Pakistan juu ya kuwa wakati gani dola isiyo ya Kiislamu inageuka kuwa dola ya Kiislamu. Wakati mjadala huu unaonyesha kuwa usimamishaji wa dola ya Kiislamu au Khilafah hivi sasa imekuwa ni lengo jumuishi la Waislamu, lakini pia inaonyesha kukosekana uwazi kwa jamii ya wasomi wa Kiislamu juu ya suala hili.

Hebu na tuijadili zaidi nukta hii, kwa sababu jibu la swali la ima Khilafah zilizopita zilikuwa sahihi ama la hutegemea juu ya jibu la swali linalohusiana na mazingira ambayo dar ul Islam imevunjwa. Vile vile, kuamua ima mamlaka yaliosimamishwa hivi leo na kujiita kuwa ya Kiislamu kuwa ni kweli ya Kiislamu pia inategemea juu ya masharti ya lazima kwa dar ul Harb kugeuka kuwa dar ul Islam.

Kuhusiana na suala la kuvunjika kwa dar ul Islam, haya ni matokeo ya uvunjaji wa masharti angalau moja au yote mawili yanayohitajika kwa dar ul Islam. Sharti la mwanzo ni kuwa mamalaka ya nchi lazima yabakie kwa Waislamu na sio kwa makafiri. Sharti la pili ni kuwa masuala ya watu lazima yaendeshwe kwa mujibu wa Uislamu na sio ukafiri. Mamlaka ya utawala hapa inamaanisha kuwa masuala yote yahusuyo dola ikiwa ya ndani na ya nje yawe chini ya mikono ya Waislamu. Na ukafiri hapa humaanisha ukafiri usio na shaka na ulio wa wazi, yaani kusiwepo hata chembe ya shaka ndani yake na isiwe uoni tu wa wanasheria. 

Tunapoangalia Khilafah zilizopita, ni wazi kuwa zilikamilisha masharti yote haya mawili. Mamlaka yalikuwa chini ya mikono ya Waislamu wakati huo na masuala ya watu yalishughulikiwa kwa mujibu wa taratibu za kisharia za Kiislamu, japokuwa dalili za baadhi yake zilikuwa dhaifu katika kipindi fulani. Ukandamizaji wa watawala haumaanishi kuwa utabikishaji ni wa kikafiri. Kama mtawala anatumia vibaya mamlaka yake kuwakandamiza waasi, au ananyakua bila ya uhalali mali ya mtu, au anajinufaisha yeye na familia yake kutokana na mali ya Ummah, au kumtaka mtu kutomtii Mwenyezi Mungu (swt), basi atakuwa ni mwenye hatia ya kutenda haramu. Hata hivyo, hii haiingii katika ukafiri wa wazi (kufr buwah). Kuna tafauti baina ya kusitisha hukmu maalum kwa kuwapendelea jamaa na ukauita Uislamu kuwa ni njia ya maisha ya zama za nyuma na kwamba haufai kwa ajili ya dunia ya sasa. Pia kuna tafauti baina ya kunywa ulevi na kuruhusu ulevi, riba na uzinifu na kamari. Imepokewa kupitia kwa Hudhayfah bin Yaman kuwa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema,

«يَكُونُ بَعْدِي أَئِمَّةٌ لاَ يَهْتَدُونَ بِهُدَاىَ وَلاَ يَسْتَنُّونَ بِسُنَّتِي وَسَيَقُومُ فِيهِمْ رِجَالٌ قُلُوبُهُمْ قُلُوبُ الشَّيَاطِينِ فِي جُثْمَانِ إِنْسٍ قَالَ: قُلْتُ: كَيْفَ أَصْنَعُ يَا رَسُولَ اللَّهِ إِنْ أَدْرَكْتُ ذَلِكَ قَالَ:‏ تَسْمَعُ وَتُطِيعُ لِلأَمِيرِ وَإِنْ ضُرِبَ ظَهْرُكَ وَأُخِذَ مَالُكَ فَاسْمَعْ وَأَطِعْ»

“Kutakuwa na watawala baada yangu hawatoongoza kwa uongozi wangu wala kufuata Sunnah zangu. Kutakuwa na watu miongoni mwao nyoyo zao zitakuwa kama za mashetani ndani ya miili ya wanadamu”. Mtu akauliza, “Ewe Mtume wa Mwenyezi Mungu! Nini nifanye pindi nitakapomdiriki mtawala huyo?” Akasema, “Msikize na umtii amir hata akikupiga mgongoni kwako na kuchukua mali yako, basi sikiza na utii.” [Muslim]. Imepokewa kutoka kwa Abu Dhar kuwa Mtume (saw) amesema,  

«يَا أَبَا ذَرٍّ كَيْفَ أَنْتَ عِنْدَ وُلَاةٍ يَسْتَأْثِرُونَ عَلَيْكَ بِهَذَا الْفَيْءِ قَالَ وَالَّذِي بَعَثَكَ بِالْحَقِّ أَضَعُ سَيْفِي عَلَى عَاتِقِي فَأَضْرِبُ بِهِ حَتَّى أَلْحَقَكَ قَالَ أَفَلَا أَدُلُّكَ عَلَى خَيْرٍ لَكَ مِنْ ذَلِكَ تَصْبِرُ حَتَّى تَلْقَانِي»

“Ewe Abu Dharr! Utafanya nini kutakapokuwepo na watawala wataojilimbikizia mali badala ya kuitoa kwa watu?” Akasema, Ninaapa kwa yule aliyekutuma kwa haki, Nitaweka panga begani mwangu na kumpiga nalo hadi nikutane nawe.” Akasema, “Nikujuilishe lililo bora kwako kuliko hilo? Kuwa na subira hadi ukutane na mimi.” [Ahmad]

Ikiwa mtawala binafsi yake atakengeuka sheria za Kiislamu lakini akawa anazitekeleza hadharani, ikiwa mtawala anamuamrisha afisa wa serikali kutenda jambo linalokwenda kinyume na Uislamu, ikiwa mtawala anadhihirisha ukafiri wa wazi, ikiwa mtawala amejichukulia mamlaka kwa nguvu, na ikiwa mtawala anaendesha mambo ya watu kinyume na misingi ya Kiislamu, haya yote ni yenye utafauti ambapo kuna hukmu fafanuzi katika Shariah kuhusiana nayo. Wale wanaojaribu kubatilisha uungaji mkono wa uhalisia wa Uislamu wa Khilafah zilizopita juu ya msingi wa matukio machache ya kihistoria yanayochujwa, kwa upande mwengine, wanatumia misingi isiyo sahihi kuisoma historia, na kwa upande mwengine, wamepuuza upande wa kisheria wa Uislamu. Pia, wameathiriwa na fahamu za Wamagharibi juu ya dola. Badala ya kutegemea juu ya dalili zenye uthibitisho juu ya kuwa nchi za Waislamu wakati wa zama hizo zilikuwa dar ul Islam ama la, watu hawa hutumia vyanzo sahihi na visivyo sahihi kukusanya orodha ya matendo ya dhulma na ufisadi yaliofanywa na baadhi ya Makhalifah wakati huo ili kuwashawishi wasomaji kuchukua uoni wao kuhusiana na suala hili.

Ni muhimu pia kufahamu hapa kuwa dola haibatiliki kutoka kuwa Khilafah wakati Khalifah akitekeleza ukafiri wa wazi (kufr buwah). Ili kufahamu tafauti baina ya kufr buwah inapodhihirika yenyewe katika dola ya Kiislamu na dar ul Islam kuvunjwa, ni muhimu kwanza kufahamu kufr buwah inamaanisha nini. Tunapoangalia hadith zinazohusiana na mtawala akitekeleza kufr buwah tunaona kuwa hazikutaja kufr buwah, lakini pia zimetaja matakwa ya dalili zisizo na shaka za kuifanya kufr buwah imetokea. Hivyo Mtume (saw) hakutosheka tu juu ya kauli, «إِلا أَنْ تَرَوْا كُفْرًا بَوَاحًا» “Isipokuwa mukiuona ukafiri wa wazi” lakini pia akaongeza «عِندَكُم مِن الله تَعَالى فِيه بُرهَان» “Ambapo muna burhaan (hoja) ndani yake kutoka kwa Mwenyezi Mungu.” [Bukhari]. Neno Burhan linatumika tu kwenye dalili isiyo na shaka. Kwa hivyo kama kutakuwa na shaka kuwa jambo ni kufr ama la, basi istilahi kufr buwah ambayo Mtume (saw) amewataka Waislamu kunyanyua panga zao dhidi yake haitotumika. Pili, istilahi kufr buwah imekuja kwa neno la sifa jumla (نکرة موصوفة), na hivyo linatumika tu juu ya chochote ambacho kinaweza kuwa kufr buwah, na sio vitu maalum. Neno buwah linatokana na maneno bah na bawahan ambayo tafsiri yake ni ‘kujitokeza’. Kwa hivyo kufr buwah ni kufr “iliyo wazi na dhahiri.” Kuna namna mbili ambapo inaweza kutokea:

  1. Mtawala kuikataa aqida ya Kiislamu na kuwa kafiri na akaonyesha ukafiri wake wazi wazi.
  2. Baadhi ya Waislamu wanaoishi katika dar ul Islam wakiritadi lakini mtawala akaendelea kuwakubali kuwa Waislamu. Hii ni kwa sababu hadith imetaja kufr buwah kuwa ni sifa jumla (نکرة موصوفہ), kwa hivyo sio lazima kuwa na mtawala tu ndio aonyeshe ukafiri. Lakini kama yeyote atatenda, itazingatiwa kuwa ni kufr buwah. Masharti pekee ni kuwa ukafiri uwe umejionesha ndani ya dola na hakuna juhudi za kuuzuia. Hata hivyo, wasiokuwa Waislamu na Mustamanin wanaoishi ndani ya dar ul Islam katika hali yao ya ukafiri na sehemu zao za ibada wamevuliwa humu, kwa sababu ya hukmu za Jizya na amani yao.
  3. Mtawala anapokataa amri ya wazi ya kisharia ya Uislamu, kama kutangaza kuwa pombe ni halali kwa sababu Mwenyezi Mungu hakuiharamisha, huku akijaribu kulazimisha hili kwa uwazi. Hii inaingia katika kipengele cha kufr buwah, kwa sababu hapa mtawala anaipinga waziwazi Quran, ambalo hilo ni ukafiri, kama Shaykh Taqi al-Din alivyoeleza katika sehemu ya kwanza ya kitabu chake Nidham-ul-Islam, “Kwa hivyo kuikanusha Sheria kwa jumla, au ufafanuzi wake uliokatikiwa, ni ukafiri sawa sawa ziwe ni ahkamu zenye kuambatana na ibada au maingiliano (mu’malat) au nidhamu ya kuadhibu waasi au vyakula. Kukanusha Aya: وَأَقِيمُوا الصَّلاَةَ Simamisheni swala [2:43] ni kama kukanusha Ayaوَأَحَلَّ اللهُ الْبَيْعَ وَحَرَّمَ الرِّبَا Mwenyezi Mungu amehalalisha biashara na kuharamisha riba [2:275] ni sawa kama kukanusha Aya  وَالسَّارِقُ وَالسَّارِقَةُ فَاقْطَعُوا أَيْدِيَهُمَا  Mwizi, mume au mke, wakateni mikono yao [5:38] na ni kama kukanusha Aya  حُرِّمَتْ عَلَيْكُمْ الْمَيْتَةُ وَالدَّمُ وَلَحْمُ الْخِنزِيرِ وَمَا أُهِلَّ لِغَيْرِ اللهِ بِهِ Imeharamishwa kwenu nyamafu na damu na nyama ya nguruwe na kilichochinjwa si kwa ajili ya Mwenyezi Mungu [5:3]. Vilevile, kama mtawala amesitisha hukmu ya wazi katika Uislamu kwa misingi ya kuwa haitumiki katika wakati wa sasa, au mtawala anachukua sheria ambayo yeye anahisi ni bora zaidi kuliko sheria ya Kiislamu, basi hii ni kuonyesha kufr buwah, na aya ifuatayo inamhusu,[وَمَنْ لَمْ يَحْكُمْ بِمَا أَنْزَلَ اللَّهُ فَأُولَئِكَ هُمُ الْكَافِرُونَ] “Na wasiohukumu kwa aliyo teremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri.” [Surah Al-Maidah 5:44].

Tafauti baina ya kuonyesha kufr buwah katika dar ul Islam na kuvunjwa dar ul Islam ni kipindi ambacho majaribio yanafanyika kuilazimisha kufr buwah waziwazi, ili kuivunja dar ul Islam. Mara baada ya majaribio haya kufanikiwa na mambo ya watu yakaanza kushughulikiwa kwa mujibu wa sheria hizi mpya na zikaanza kutawala jamii kiasi kwamba kuzipinga ikawa ni uhalifu, basi dar ul Islam itageuka kuwa dar ul Kufr. Hivi leo tunaona hali kama hiyo katika maeneo ya Waislamu, ambapo dola zinaegemea kwenye fikra za kikafiri kama haki ya kutunga sheria, uhuru wa kiliberali, usawa baina ya wanaume na wanawake na haki za msingi za binadamu. Madikteta au wabunge wanatengeneza sheria zinazoegemea fikra hizi na sheria hizi hutabikishwa kwa nguvu na dola, na mahakama hufanya maamuzi kulingana nazo. Hivyo, masuala ya watu yanadhibitiwa kulingana na fikra hizi za kikafiri.

Baadhi ya watu wanadai kuwa huu sio uoni sahihi kwa kuwa dola imeshabainisha katika katiba kuwa mamlaka yapo kwa Mwenyezi Mungu (swt) na kwamba mtawala hawezi kutekeleza chochote kilicho kinyume na Uislamu. Kwa hivyo mtawala akitenda kosa na kwenda kinyume na katiba, basi hili huwa sio kosa la dola, na dola inabakia kuwa ya Kiislamu. Hata hivyo, hii sio hoja ya sawa, kwa sababu katika Uislamu hakuna tafauti baina ya serikali na dola. Mwenyezi Mungu (swt) anasema,

[وَمَنۡ لَّمۡ يَحۡكُمۡ بِمَاۤ اَنۡزَلَ اللّٰهُ فَاُولٰٓٮِٕكَ هُمُ الۡكٰفِرُوۡنَ]

“Na wasiohukumu kwa aliyo teremsha Mwenyezi Mungu, basi hao ndio makafiri.” [Surah al-Maidah 5:49]. Hukmu hapa inahusiana na maamuzi ya mtawala, bila kujali maamuzi hayo kuwa ni kwa sababu ya katiba au sababu nyengine. Pia, Uislamu umefafanua vizuri kufr buwah kuwa inaweza kuwa yenye chanzo chochote, ima inaonyeshwa na katiba, matendo ya mtawala, au watu wanaoishi ndani ya dola. Hii ni ziada ya ukweli kwamba vingi ya vifungu vya Katiba vinatokana na fikra za kikafiri, kama haki ya mwanadamu ya kutunga sheria, haki za msingi za mwanadamu, ushirikiano wa kiimani, usawa baina ya wanaume na wanawake, kukubaliana na Umoja wa Mataifa na sheria za kimataifa.

Kuna tafauti katika kuonyesha kufr buwah katika dar ul Islam na dar ul Islam kuvunjwa, hivyo hukmu juu ya kila suala kati ya masuala haya katika Shariah ni tafauti, kwani inaeleweka kuwa hukmu inabadilika pindi uhalisia wa kitu unapobadilika. Tuzingatie hadithi hii ili kufahamu tafauti hii:

«بَايَعْنَا رسول الله -صلى الله عليه وسلم- على السَّمع والطَّاعَة في العُسْر واليُسْر، والمَنْشَطِ والمَكْرَه، وعلَى أَثَرَةٍ عَلَينا، وعلى أَن لاَ نُنَازِعَ الأَمْر أَهْلَه إِلاَّ أَن تَرَوْا كُفْراً بَوَاحاً عِندَكُم مِن الله تَعَالى فِيه بُرهَان، وعلى أن نقول بالحقِّ أينَما كُنَّا، لا نخافُ فِي الله لَوْمَةَ لاَئِمٍ»

“(Imepokewa kutoka kwa ‘Ubada Ibn Samit kuwa) Tumetoa bay’ah kwa Mtume (saw) juu ya kusikiza na kutii katika uzito na wepesi, katika furaha na huzuni, na hata wengine wakipendelewa zaidi yetu, na kwamba hatutazozana katika mambo ya wenye kutawala. Isipokuwa mkiona kufr buwah mlio na Ushahidi wa wazi (burhan) kwayo kutoka kwa Mwenyezi Mungu...” Hadithi hii inaelezea hali mbili: hali ya mwanzo ni wakati ambapo haitakiwi kunyanyua panga dhidi ya mtawala, bali ni kumtii katika furaha na huzuni na uzito na wepesi, muda wa kwamba hakutenda kufr buwah, na hali ya pili ni ambapo imeruhusiwa kuasi dhidi ya mtawala kwa sababu anatenda kufr buwah waziwazi. Hii ni kusema, kuwa hadithi hii inaelezea mpangilio ambapo mwanzoni kuna dar ul Islam na mtawala anatawala kwa kile alichokiteremsha Mwenyezi Mungu (swt), licha ya kuwa baadhi ya watu hawapendi kile anachofanya, lakini baadaye anaanza kutenda kufr buwah na hivyo watu kumnyanyulia panga zao. Hii ndio sababu kwa nini Hizb ut Tahrir haishiki silaha dhidi ya watawala hawa kuwa ndio msingi, kwa sababu uhalisia wa ardhi za Waislamu hivi leo sio kama zimetawaliwa kwa Uislamu na kisha kuvuka kuwa za kikafiri, bali uhalisia ni kuwa zote zipo katika dar ul Kufr. Zipo sawa na hali ya Makkah wakati wa Mtume (saw), ambapo ukafiri ndio uliotawala na watu wakiendesha mambo yao kulingana na hali hiyo. Mtume (saw) hakunyanyua panga dhidi yao bali aliendesha mapambano ya kifikra na kisiasa dhidi yao. Mfano wa kufr buwah uliotokea katika dar ul Islam ni pale Mustafa Kamal aliyeibadili Khilafah kuwa dola ya kisekula ya kidemokrasia na kuanza kutawala kulingana na fikra za kikafiri. Hicho kingekuwa ni kipindi ambapo mtu angesimama dhidi yake na kumuua, angetekeleza amri ya Mtume (saw) na angeinusuru Uturuki kugeukia kuwa dar ul Kufr.

Pamoja na hivyo, maneno, «أَن لاُ نُنَازِعَ الأَمْر أَهْلَه» “na kwamba hatutazozana katika mambo ya wenye kutawala.” yanatumika ambapo yanaonyesha kuwa hadithi hii ni kuhusiana na watu ambao Uislamu unawatambua kuwa watawala halali, yaani watu wanaofaa kutawala kwa sababu Waislamu wametoa bay’ah kwao ili watabikishe Uislamu. Na hadithi hii ndio inawaongoza Waislamu juu ya nini cha kufanya pindi watawala hawa wakianza kutekeleza kufr buwah. Kwa upande mwengine, watawala wa sasa katika ardhi za Waislamu kwanza sio watawala halali kwa mujibu wa Uislamu, kwa hiyo hadith hii haiwahusu wao.

Licha ya kuwa ni wazi kwamba Pakistan sio dar ul Islam, Ulamaa wengi bado wanasitasita katika kutamka hilo. Kwa ujumla wanatoa sababu mbili kwa hili. Ya mwanzo ni kuwa kama watatangaza Pakistan kuwa ni dar ul Kufr basi wanaamini kwamba itakuwa wajibu kunyanyua silaha dhidi ya watawala wa sasa, ambapo itapelekea fitnah katika jamii. Ya pili ni kuwa kama tutakubali kuwa ardhi zote ni dar ul Kufr, basi Waislamu hawatolazimika kuyalinda na kuyahifadhi maeneo haya kutokana na makafiri, kwa kuwa sio tena dar ul Islam. Hoja za Ulamaa wa sasa hivi zina kasoro kwa sababu ya kukosa ufahamu sahihi kuhusiana na tafauti katika hukmu kwa ajili ya dar ul Islam na dar ul Kufr, na masharti ambapo moja hugeuka kuwa nyengine. Kwa mfano, nchi za Uingereza na Pakistan zote ni dar ul Kufr. Hata hivyo, usalama wa Pakistan bado uko mikononi mwa Waislamu, wakati katika Uingereza upo mikononi mwa makafiri. Haitakiwi kwa Waislamu kuuweka usalama wao chini ya makafiri. Usalama unapatikana kupitia mamlaka na nguvu za kijeshi katika nchi. Kuwapatia usalama wa Waislamu makafiri ni kuwapa mamlaka juu ya Waislamu. Katika Uislamu, haitakiwi kwa Waislamu kuwaruhusu makafiri kuwamiliki kwa sababu Mwenyezi Mungu (swt) amesema katika Quran,

[وَلَنۡ يَّجۡعَلَ اللّٰهُ لِلۡكٰفِرِيۡنَ عَلَى الۡمُؤۡمِنِيۡنَ سَبِيۡلاً]

“Wala Mwenyezi Mungu hatowapa makafiri njia ya kuwashinda Waumini.” [Surah An-Nisa 4:141]. Na Mwenyezi Mungu (swt) amewaamrisha Waislamu kuwa viongozi wao watokane miongoni mwao:

[یٰۤاَیُّهَا الَّذِیْنَ اٰمَنُوْۤا اَطِیْعُوا اللّٰهَ وَاَطِیْعُوا الرَّسُوْلَ وَاُولِی الْاَمْرِ مِنْكُمْ]

“Enyi mlioamini! Mtiini Mwenyezi Mungu, na mtiini Mtume na wenye madaraka katika nyinyi.” [Surah An-Nisa 4:59]. Kwa hivyo ubwana lazima uwe kwa Waislamu na hii haitegemei amri ya kutawala kwa mujibu wa Uislamu, japokuwa amri zote hizi zinahitaji kutekelezwa. Kutohukumu kwa Uislamu ni dhambi, lakini dhambi moja sio udhuru halali kwa dhambi jengine, kwa kuutoa usalama wetu kwa makafiri. Pia Quran Tukufu inawataka Waislamu kuwakabili makafiri sawasawa pindi wanapofanya uchokozi,

[فَمَنِ اعۡتَدٰى عَلَيۡكُمۡ فَاعۡتَدُوۡا عَلَيۡهِ بِمِثۡلِ مَا اعۡتَدٰى عَلَيۡكُم]

“Anayekushambulieni naye mshambulieni, kwa kadiri alivyokushambulieni.” [ Surah Al-Baqarah 2:194]

Jibu la swali la wakati gani dola inakuwa ya Kiislamu ni kuwa kuna masharti mawili ya lazima ambayo yamekwisha elezwa hapo juu. Nayo ni, mamlaka ya dola lazima yawe kwa Waislamu na mambo ya watu yasimamiwe kwa mujibu wa Uislamu. Masharti haya mawili yalijulikana vyema na wanazuoni waliotangulia. Hata hivyo, katika dunia ya sasa, kwa kuwa Waislamu wamepoteza ufahamu wao wa kile kinachomaanisha kutawaliwa kwa mujibu wa Uislamu, hivyo Hizb ut Tahrir imepaswa kuelezea kwa ufafanuzi misingi iliyopo ya Dola ya Kiislamu. Imebidi kuelezea kama inawezekana kwa dola kuwa dola ya kitaifa, na kwa nini ni muhimu kwa sera yake ya kigeni kujengwa juu ya kuueneza Uislamu kupitia da’wah na jihad, pamoja na kama inaruhusiwa kwa Waislamu kuwa na dar ul Islam zaidi ya moja. Vile vile, Hizb ut Tahrir imeweka wazi fikra msingi za Kiislamu zinazounda misingi ya hukmu na utawala. Kama ambavyo kafiri hawezi kuwa muumini kwa kutekeleza tu Uislamu kwa sababu ya kufikiri kwake kuwa fikra za Kiislamu ni zenye msaada na manufaa, dola vile vile haiwi moja kwa moja ya Kiislamu kwa kudai na kutangaza tu kuufuata Uislamu, lakini kiuhalisia ikawa inavunja kwa uwazi hukmu za Kiislamu. Hii ndio sababu Hizb ut Tahrir ilianzia kielelezo chake cha katiba ya Dola ya Khilafah kwa kusisitiza kuwa msingi wa dola ya Kiislamu ni Aqida, na kuweka wazi kuwa msingi wa dola ni fikra na fahamu zake. Katiba ya dola yoyote inaifanya kuwa wazi fikra inayoitegemea. Kwa hivyo, kama dola inadai hivi leo kuwa ni dar ul Islam basi ni lazima iwakilishe katiba yake kwa Ummah, kwa dalili za Kishariah zinazoipa nguvu kila kifungu chake. Hizb ut Tahrir inaamini kuwa muundo wa dola na hukmu zilizofafanuliwa zilizomo kwenye vitabu vyake ni sahihi, huku ikikubali uwezekano wa utafauti wa rai. Kama ambavyo Imam Hassan (ra) alijiweka upande kwa kumuachia Amir Muawiyah ili kuweka umoja wa Ummah, japokuwa aliamini kuwa yeye alistahiki zaidi nafasi ya ukhalifah, Hizb vilevile ipo tayari kukubali chama chengine chochote kitachosimamisha dar ul Islam, katika hukmu ambazo ni tafauti na za Hizb ut Tahrir muda wa kuwa zimevuliwa kutoka kwenye Uislamu. Wakati Uislamu unakubali hitilafu za kielimu baina ya Waislamu, upeo wa haya ni mpana sana. Kwa hivyo, yeyote mwenye muongozo mbadala wa dola ya Kiislamu uliovuliwa kutoka vyanzo vya Kiislamu kupitia Ijtihad, na ulio tafauti na ule wa Hizb ut Tahrir, na auwasilishe.

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na

Usman Adil – Wilayah Pakistan

 

#أقيموا_الخلافة

#الخلافة_101

#ReturnTheKhilafah

#YenidenHilafet

#TurudisheniKhilafah

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.