Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Hizb ut Tahrir / Denmark: Chuki, Uongo na Uvamizii wa Mayahudi!

Waziri Mkuu anajaribu kunasibisha Waislamu na ongezeko la chuki dhidi ya mayahudi kwa kutumia dhana ya “uhamiaji”.

Uhalisia ni kwamba chuki kwa mayahudi na kupambana nao ni suala lenye mizizi ya kina katika historia na utamaduni wa Ulaya.

Ukilitazama kwa pamoja na maadhimisho ya ukombozi wa Auschwitz, viongozi wa Kimagharibi walilizuru jeshi la uvamizi “Israeli” kuonesha huruma zao na uungaji mkono wao, bila kujali ukatili wa wavamizi na uhalifu wao wa mara kwa mara katika eneo walilo vamia.

Dola ya Denmark bila kificho ina uhusiano wa karibu sana na “Israeli”, katika nyanja ya kisiasa na kiuchumi.

Kwa uwazi kabisa serikali inapotosha mjadala kuhusiana na chuki dhidi ya Mayahudi na hujaribu kuzima upinzani na ukosoaji dhidi ya majeshi vamizi ya Israeli.

Serikali ya Denmark na vyombo vya dola vinaendasha mapambano wazi dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Uhuru “mtukufu” wa maoni umefutwa kwa Waislamu hususan linapokuja suala la uvamizi wa kinyama wa ardhi ya Palestina.

Kwa mara nyingine tena unafiki wa kisiasa umezidi kukua na kudhihirisha udhaifu wa utamaduni wa Kimagharibi.

07 Jumadal Akhar 1441 H – Februari 01, 2020 M

[Bofya Picha utizame Video]

Imebadilishwa mara ya mwisho mnamoJumapili, 12 Aprili 2020 06:27
Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.