- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:
Matembezi ya Ukombozi: “Gaza inakufa kwa Njaa huku Watawala Mabwege Wakiuzingira na Kufuja Mali za Umma”
Matembezi yalioandaliwa na Hizb ut Tahrir / Wilayah ya Tunisia yalitoka katika mji mkuu wa Tunis, baada ya swala ya Ijumaa, mnamo tarehe 03 Dhu al-Hijjah 1446 H sawia na tarehe 30 Mei 2025 M kuanzia Msikiti wa Al-Fath kunusuru watu wa Palestina na Msikiti wa Al-Aqsa ulio mateka, ambayo yaliitishwa na watu wa Zaytouna Tunisia chini ya kichwa: “Gaza inakufa kwa Njaa huku Watawala Mabwege Wakiuzingira na Kufuja Mali za Umma” matembezi hayo ambayo yalihudhuriwa na umati mkubwa wa watu wa Tunisia ya kijani, yalianza kwa takbira na tahlil na yalizunguka barabara kuu za mji mkuu zinazoelekea Barabara ya Al-Thawra. Mabango yaliinuliwa, bango kuu likiwa na kichwa cha matembezi, na bango jengine likiandikwa "Msaada wa Marekani kwa umbile la Kizayuni dolari bilioni 22, tani 90,000 za zana za kijeshi."
Matembezi hayo yalihitimishwa mbele ya ukumbi wa michezo wa manispaa, ambapo wahudhuriaji waliobarikiwa walikusanyika kwenye ukumbi huo waliimba kauli mbiu zikiwataka maafisa wanyoofu na wanajeshi kuwanusuru ndugu zao wanaokandamizwa mjini Gaza. Hii ilifuatwa na hotuba iliyotolewa na shababu Najm al-Din Shuaybin, ambamo alitaja misimamo ya wanaume ambao walijitahidi katika historia nzima kutetea matukufu ya Umma, dini, heshima na ardhi, kama vile Salah al-Din al-Ayyubi, Khalid ibn al-Walid, Umar ibn al-Khattab na watu wa kawaida katika zama za matatizo na balaa ambazo ziliupitia umma wa Kiislamu. Vile vile aliwahisabu maafisa na askari wanyoofu katika majeshi ya Waislamu kwa kushindwa kwao kuwanusuru ndugu zao, na adhabu inayowangoja kutoka kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu ikiwa wataendelea na msimamo huu wa aibu, na malipo makubwa yanayowangojea kama watatekeleza wajibu wao wa kidini, ambao ni kuwapindua watawala wa madhara na kusimamisha utawala wa Uislamu, na kisha kutangaza Jihad nchini Palestina na hivyo kupatikana kwa hadi ya Mwenyezi Mungu na bishara njema ya Mtume Mtukufu (saw).
Matembezi haya ni miongoni mwa makumi ya matembezi yaliyoandaliwa na Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Tunisia dhidi ya vita vya halaiki dhidi ya ndugu zetu wa Gaza, ili kuthibitisha kwamba Hizb ut Tahrir/Wilayah Tunisia imejitolea kwa watu wake nchini Palestina na kwamba inaendeleza ulinganizi wake wa kusimamisha hukmu ya Uislamu kupitia kusimamisha Dola ya Khilafah, ahadi ya Mwenyezi Mungu na bishara njema ya Mtume Mtukufu (saw).
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilaya ya Tunisia
Ijumaa, 03 Dhu al-Hijjah 1446 H sawia na 30 Mei 2025 M
- Picha za Amali ya Matembezi -
https://www.hizb-ut-tahrir.info/sw/index.php/dawah/tunisia/4696.html?print=1&tmpl=component#sigProIdaef61704e0
- Alama Ishara za Amali -
#طوفان_الأقصى
#الجيوش_إلى_الأقصى
#الأقصى_يستصرخ_الجيوش
#AksaTufanı
#OrdularAksaya
#ArmiesToAqsa
#AqsaCallsArmies
Kwa maelezo zaidi tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut tahrir / Wilayah Tunisia:
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia
Ukurasa wa Facebook wa Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia
Tovuti Rasmi ya Jarida la Tahrir
Ukurasa wa Facebook wa Jarida la Tahrir