- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:
Jukwaa la Mazungumzo: “Ni Wakati sasa wa Kituo cha Kisiasa Kujikomboa kutokana na Utegemezi wa Wakoloni wa Magharibi”
Kamati ya Mawasiliano ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Tunisia iliandaa jukwaa la mazungumzo lenye kichwa “Ni Wakati sasa wa Kituo cha Kisiasa Kujikomboa kutokana na Utegemezi wa Wakoloni wa Magharibi” siku ya Jumapili, 23 Novemba 2025, katika ukumbi wa mikutano wa hizb katika makutano ya Sukra Ariana katika mji mkuu.
Jukwaa hili, lililowasilishwa na Ustadh Habib, walishiriki ndani yake Mhandisi Yasser Al-Anwar na Ustadh Abdul Raouf Al-Amri, na lilihudhuriwa na hadhira kubwa ya wakaazi wa eneo hilo. Jukwaa lilifunguliwa kwa kusoma aya kutoka Quran Tukufu.
Katika hotuba yake ya ufunguzi, Mhandisi Yasser Al-Anwar alizungumzia ufafanuzi wa mwamko wa kweli, ambao lazima utoke katika mtazamo sahihi—yaani, kutoka kwa msingi sahihi wa aqida unaokinaisha akili na kuleta amani moyoni. Alisisitiza kwamba mwamko wa kweli haupimwi tu kwa maendeleo ya nyenzo na kiteknolojia, bali pia kwa maadili mema na kuinuliwa kwa ubinadamu kutoka hali ya kuwepo kama wanyama tu, na kwamba Waislamu waliamka kupitia itikadi ya kiroho na kisiasa, ambayo kwayo mfumo kamili wa maisha ya binadamu, jamii, na dola ulichipuza, na hivyo kuanzisha hadhara iliyoendelea zaidi katika historia ya binadamu.
Kisha, Ustadh Abdul Raouf Al-Amiri alielezea katika uingiliaji wake kwamba Umma wa Kiislamu umeshuka kutoka hadhi yake ya awali, ambayo ulikuwa nayo ulipokuwa chini ya chombo chake cha kisiasa, “ua la dunia,” na ambao uliongoza ubinadamu kwenye usalama na utulivu. Aliongeza kwamba watu wa Umma huu wamejaribu kuinuka tena, lakini kutokana na utawala wa kifikra, kiuchumi, na kisiasa wa Magharibi juu ya ardhi za Waislamu, hawajafanikiwa kwa sababu mwamko sahihi upo katika kuikumbatia aqida ya Kiislamu na hukmu na suluhisho yanayotokana nayo—suluhisho msingi la mwamko wa kweli.
Katika uingiliaji wake wa pili, Mhandisi Yasser Al-Anwar alisema kwamba mzozo kati ya dola ni mzozo wa kanuni na maadili, na ndio mzozo hatari zaidi. Alisema kwamba hadhara ya Kimagharibi inategemea kanuni ya kutenganisha dini na maisha, ambayo imeifanya kuwa hadhara ya mali na muozo wa kimaadili, badala ya hadhara wa binadamu. Hivi ndivyo taasisi ya kisiasa leo inavyoitabanni chini ya jina la demokrasia. Alisema kwamba taasisi ya kisiasa leo ina wajibu wa kurudi kwenye kanuni za Uislamu na kuzifanya kuwa kipimo na mahali pa kianzio cha fikra yake na mradi wake wa kisiasa: “Khilafah kwa njia ya Utume.”
Katika uingiliaji wake wa pili, Ustadh Abdul Raouf Al-Amiri alizungumzia jinsi Magharibi ilivyocheza karata ya harakati za “Kiislamu”, na kuzileta madarakani. Baada ya kushindwa kwao, Magharibi iliendeleza fikra kwamba Uislamu wa kisiasa ulikuwa mradi uliofeli, ingawa harakati hizi zilitabanni fikra za kisekula. Aligusia harakati za Kiislamu zilizotabanni Uislamu katika utawala, kama vile Taliban, Hamas, na Muungano wa Mahakama za Kiislamu nchini Somalia. Alisema kwamba sababu za kufeli kwao ni ukosefu wao wa ufahamu wa kisiasa kuhusu uhalisia, kuingia kwao katika masharti na misingi iliyowekwa na mfumo uliopo, na kutokuwepo na ukosefu wa mradi ulio wazi na uliofafanuliwa vyema wa kuutekeleza. Katika maelezo yake ya kumalizia, Ustadh Yassar Al-Anwar alifafanua kwamba ahadi ya Mwenyezi Mungu na bishara njema za Mtume wetu mtukufu kuhusu kusimama kwa dola ya Khilafah Rashida huwalazimisha Waislamu kufanya kazi ili kutimiza ahadi hii. Alieleza kwamba baada ya kusimama kwake, Khilafah Rashida itafanya kazi ya kuondoa vikwazo vyote, udanganyifu, na magumu, na kutoa maisha ya heshima kwa raia wake. Itakuwa kiongozi katika nyanja zote, ikilinda kiini cha Uislamu kutokana na njama za maadui zake.
Katika kumalizia kwa jukwaa hilo, Ustadh Abdul Raouf Al-Amiri alisema kwamba wale wanaotafuta mabadiliko hawapaswi kutegemea uhalisia wa sasa wa ufisadi. Badala yake, lazima waendelee kutoka kwa msingi walioutabanni na waujaaliye ndio mwelekeo wa kuutekeleza—yaani, hukmu na masuluhisho yaliyovuliwa kwa nguvu ya dalili kutoka kwa Kitabu cha Mwenyezi Mungu na Sunnah ya Mtume Wake. Hili linaweza kupatikana tu kupitia kiapo cha utiifu cha Umma kwa Khalifa mmoja Muongofu ambaye anatimiza mahitaji ya kisheria ya utawala, anatabikisha hukmu za Uislamu, na anabeba ujumbe wake wa mwongozo kwa wanadamu wote.
Na kwa hili, Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Tunisia inaendelea na kazi yake isiyochoka ya kuwasilisha mradi wake kwa Ummah na kuubebesha wajibu wake uliloamriwa na Mwenyezi Mungu kusimamisha dini ya Mwenyezi Mungu ardhini, ambayo Muumba wake ameichagua kwa ajili yake, ili iwe kama alivyosema katika Kitabu Chake Kitukufu:
(كُنْتُمْ خَيْرَ أُمَّةٍ أُخْرِجَتْ لِلنَّاسِ تَأْمُرُونَ بِالْمَعْرُوفِ وَتَنْهَوْنَ عَنِ الْمُنْكَرِ وَتُؤْمِنُونَ بِاللَّهِ))
“Nyinyi mmekuwa bora ya umma walio tolewa watu, kwa kuwa mnaamrisha mema na mnakataza maovu, na mnamuamini Mwenyezi Mungu.”
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari katika Wilayah ya Tunisia
Jumapili, 2 Jumada al-Akhirah 1447 H, sawia na 23 Novemba 2025 M

https://www.hizb-ut-tahrir.info/sw/index.php/dawah/tunisia/5159.html?print=1&tmpl=component#sigProId1e3e39eb53

Kwa maelezo zaidi tafadhali zuru mitandao ya Hizb ut tahrir / Wilayah Tunisia:
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia
Tovuti Rasmi ya Jarida la Tahrir
Ukurasa wa Facebook wa Jarida la Tahrir
