- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:
Matembezi ya Takbira “Ni Dola ya Khilafah Pekee ndiyo Itakayomaliza Kiburi cha Amerika.”
Baada ya Swala ya Ijumaa ya mwisho ya Ramadhan Tukufu 1447 H, matembezi ya Takbira (Allahu Akbar) yaliyoandaliwa na Hizb ut-Tahrir / Wikayah ya Tunisia yalianza kutoka Msikiti wa Al-Fath katika mji mkuu, Tunis. Umati mkubwa wa Watunisia ulishiriki, wakipiga Takbira na Tahlil, na matembezi hayo yaliendelea kupitia barabara kuu za mji mkuu kuelekea Barabara ya Al-Thawra. Mabango yaliinuliwa, bango kuu likiwa limeandikwa, “Ni Dola ya Khilafah Pekee ndiyo Itakayomaliza Kiburi cha Amerika.” La pili likiandikwa, “Allahu Akbar dhidi ya wote waovu na wenye kiburi,” na la tatu likiandikwa, “Allahu Akbar dhidi ya wote wenye kiburi na ubabe." Mabango mengi madogo yalitangaza, “Khilafah ni mwokozi wa Ummah.” Matembezi hayo yalimalizika mbele ya Ukumbi wa Manispaa kwa mkutano ambapo shababu mmoja wa Hizb ut Tahrir alitoa hotuba. Alieleza kwamba vita vinavyoendeshwa na Amerika na mtoto wake, umbile la Kizayuni, dhidi ya Iran havikufungika tu na kuipokonya silaha Iran na kuiweka chini ya udhibiti wa Marekani. Badala yake, ni sehemu ya mkakati kamili wa Marekani wa kuimarisha mshiko wake kwa Ash-Sham. Amerika inatafuta kuligawanya eneo hilo na kulibadilisha kuwa majimbo yaliyogawanyika kikabila na kidini, hivyo kurahisisha usimamizi wake na kuligeuza kuwa eneo kubwa la uwekezaji kwa makampuni yake. Mradi huu unaambatana na juhudi zisizokoma za kulazimisha mjadala wa dini ya Ibrahim na kupambana na pendekezo lolote la kuregesha Uislamu madarakani na kuufanya kuwa ni mwiko.
Kipindi hiki cha kihistoria ambacho eneo hili linakishuhudia leo kinatoa fursa kwa wana waaminifu wa Ummah huu kukata minyororo, kuangusha viti vya enzi vya usaliti, na kutoa pigo la mwisho kwa Amerika na umbile nyakuzi la Kizayuni—pigo litakalobadilisha mizani za madaraka, kurekebisha mkondo wa historia, na kuregesha kwa Ummah wa Kiislamu mamlaka yake, Khilafah yake, na utawala wa Sharia yake.
Kuondolewa kwa umbile nyakuzi la Kizayuni hakutapatikana chini ya tawala hizi za vibaraka zinazolinda mipaka yake na kuzuia makombora dhidi yake, wala hakutafanywa na muungano wa kidini unaopiga vita mradi wa Kiislamu.
Hili linahitaji dola ongofu (Khilafah kwa njia ya Utume) na uongozi wa dhati na wenye ufahamu, ambao kupitia kwao ahadi ya Mwenyezi Mungu na amri isiyoepukika vitatimizwa kwa kuangamizwa uharibifu wa kiburi cha wale waliokasirikiwa juu yao.
Hivyo, Hizb ut Tahrir inaendelea na kazi yake kote ulimwenguni, ikiamsha Ummah na ufahamu wake wa masuala yake makuu, ikiukomboa kutokana na kiburi cha Marekani, ikiuokoa kutokana na uhalifu wa mfumo huu wa kibepari wa Epstein, na kuurudisha katika nafasi ambayo Mola wake Mlezi ameiweka kwa ajili yake: Umma bora ulioletwa kwa ajili ya watu.
Mjumbe wa Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah ya Tunisia
Ijumaa, 24 Ramadhan Al-Mubarak 1447 H – 13 Machi 2026 M

https://www.hizb-ut-tahrir.info/sw/index.php/dawah/tunisia/5318.html?print=1&tmpl=component#sigProIddf46b7049d

Kwa Maelezo Zaidi Tafadhali Zuru Mitandao ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia:
Tovuti Rasmi ya Hizb ut Tahrir / Wilayah Tunisia
Tovuti Rasmi ya Jarida la Tahrir
Ukurasa wa Facebook wa Jarida la Tahrir
