Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Matukio ya Kisiasa ya Hivi Majuzi nchini Yemen Yanaonyesha Nini?
(Imetafsiriwa)

Gazeti la Al-Rayah - Toleo 565 - 17/09/2025 M

Na: Mhandisi Shafiq Khamis - Wilayah Yemen

Mnamo Alhamisi, 28 Agosti, Waziri Mkuu wa Wizara ya Mabadiliko na Ujenzi, Ahmed Ghaleb Al-Rahwi, aliuawa, pamoja na mawaziri wengine tisa: Waziri wa Sheria na Haki za Binadamu Mujahid Ahmed Abdullah Ali; Waziri wa Uchumi, Viwanda na Uwekezaji Moeen Hashim Ahmed Al-Mahaqri; Waziri wa Kilimo, Uvuvi na Rasilimali za Maji Radwan Ali Ali Al-Rubai; Waziri wa Mambo ya Nje na Wageni Jamal Ahmed Ali Amer; Waziri wa Umeme, Nishati na Maji Ali Seif Mohammed Hassan; Waziri wa Utamaduni na Utalii Ali Qasim Hussein Al-Yafei; Waziri wa Masuala ya Jamii na Leba Samir Mohammed Ahmed Bajaala; Waziri wa Habari Hashim Ahmed Abdul Rahman Sharaf Al-Din; na Waziri wa Vijana na Michezo Mohammed Ali Ahmed Al-Mawlid. Mawaziri wengine kadhaa bado wako katika hali mbaya na ya wastani, akiwemo Jalal Al-Ruwaishan, Naibu Waziri Mkuu wa Masuala ya Ulinzi na Usalama. Umbile la Kiyahudi limeeleza kuwa lilifanya shambulizi hilo, likiwalenga Waziri wa Ulinzi Mohammed Al-Atifi na Mkuu wa Majeshi Mohammed Abdul Karim Al-Ghamari.

Mauaji haya yanaleta kumbukumbu za mauaji ya rais wa serikali ya Iran, Ebrahim Raisi, mnamo 19 Mei 2024, na mkuu wa afisi ya kisiasa ya Hamas, Ismail Haniyeh, mnamo 31 Julai 2024, jijini Tehran. Njama hiyo iliundwa kuwakamata wote kwa mshale mmoja, na pia operesheni ya kulipua mashini za pager nchini Lebanon mnamo Septemba 17 na 18, 2024, ambayo ilifikia kilele cha mauaji ya Hassan Nasrallah, Katibu Mkuu wa Chama cha Iran, katika vitongoji vya kusini mwa Beirut mnamo 27 Septemba 2024, na Hashem Safieddine mnamo 23 Oktoba 2024, katika mashambulizi ya anga yaliyoanzishwa na chombo cha Kiyahudi. Kinachoyaunganisha zaidi ni kwamba yote yanahusishwa na kupenya kwa mawakala wa Mossad kwenye chombo cha ujasusi cha Iran tangu kuanzishwa kwake 1953 hadi leo. Maambukizi yake yameenea katika maeneo yote yenye uhusiano na Tehran. Huenda tukakumbuka habari za kukamatwa kwa wanachama wa Houthi wanaohusishwa na Mossad waliporegea kutoka Jordan mnamo 6 Disemba 2024, kwenye Uwanja wa Ndege wa Sana'a.

Ikilinganishwa mashambulizi ya Mahouthi dhidi ya umbile la Kiyahudi na majibu yake, mashambulizi ya makombora ya Mahouthi dhidi ya shabaha katika Palestina inayokaliwa kwa mabavu katika kipindi cha karibu miaka miwili yalifikia elfu tatu, na kusababisha uharibifu wa kiuchumi, kama vile kufungwa kwa bandari ya Umm al-Rashrash (Eilat), kucheleweshwa kwa safari za ndege katika Uwanja wa Ndege wa Lod (Ben Gurion), na kuzuiliwa kwa meli kufika bandari za Palestina inayokaliwa kimabavu, kupitia Mlango-Bahari wa Bab al-Mandab, bila kusababisha hasara za kibinadamu, isipokuwa kifo kimoja. Wakati huo huo, umbile la Kiyahudi lilijibu ndani ya mwaka mmoja kwa mashambulizi 16 dhidi ya shabaha katika mji mkuu, Sana'a, kama vile uwanja wa ndege, vituo vya umeme vya Dhahban na Hizayz, kituo cha kampuni ya mafuta, na mji wa pwani wa Hodeidah, kama vile bandari na matangi ya mafuta. Mashambulizi ya hivi punde kati ya haya yalisababisha kifo cha nusu ya serikali ya Mahouthi na kujeruhiwa kwa wengine.

Kwa hivyo, Wizara ya Mabadiliko na Ujenzi imetumia miaka miwili duni kwa watu wa Yemen. Mwaka mmoja tangu kuchaguliwa kwake kutawala, ikirithi Wizara ya Wokovu; kuanzia kutangaza mabadiliko makubwa katika sherehe za kuzaliwa Mtume (saw) (Mawlid an-Nabawi) mwaka 1445 H hadi sherehe hizo hizo mnamo mwaka 1446 H, ambayo ilifungika na mipaka uundaji wa mawaziri. Mwaka mwengine madarakani, hadi sherehe ya mwaka huu ya Maulidi an-Nabawi) (saw) mwaka 1447 H, watu wa Yemen wanaendelea kuishi kwa taabu.

Sasa, kwa kuzingatia matukio haya ya hivi majuzi ya kisiasa, je Mahouthi wataachana na ushiriki wa mshirika wao mkuu serikalini, chama cha General People’s Congress, katika kuunda serikali yao mpya ijayo na kuunda wizara ya Mahouthi pekee? Haya yanajiri baada ya Mahakama Kuu ya Kijeshi jijini Sana’a kutoa hukumu ya kifo dhidi ya Ahmed Ali Abdullah Saleh mnamo 31 Julai 2025, na kutaifishwa mali yake, kwa tuhuma za uhaini na kushirikiana na adui. Hii inakuja mwaka mmoja haswa baada ya kuondolewa kwa vikwazo vya kimataifa dhidi yake na Baraza la Usalama mnamo 31 Julai 2024. Hii inafungua njia kwa yeye kuchukua nyadhifa za serikali ijayo nchini Yemen, kufuatia mazungumzo yaliyopangwa kati ya Sana'a na Aden, yaliyosukumwa na dola za kimataifa katika mzozo juu ya Yemen na yalijitokeza katika juhudi za ufuatiliaji za mjumbe wa Umoja wa Mataifa kuzishika, baada ya kusitasita kwa miaka miwili kutokana na vita dhidi ya Gaza? Au watashindwa kufanya hivyo, kwa sababu wahusika wawili halisi wa kimataifa wanaosimamia mzozo wao dhidi ya Yemen wamekubali kugawanya madaraka, baada ya vita vya pande mbili za ndani, na uungwaji mkono wa kikanda kwa kila mmoja, haujaleta ushindi wa uhakika kwa kila mmoja wao?!

Unyanyasaji wa Mahouthi kwa mshirika wao anayetawala, chama cha General People’s Congress, uliendelea na dhoruba ya mkutano wa Sekretarieti Kuu katika makao yake makuu, Taasisi ya Mithaq. Kisha Mahouthi walilazimisha Bunge la Congress kutangaza kughairi sherehe za mwaka huu za kuadhimisha miaka 43, ambayo iliadhimishwa Agosti 24. Kamati Kuu ya chama cha General People’s Congress iliidhinisha, mnamo 28 Agosti 2025, kuvuliwa uanachama kwa Ahmed Ali Abdullah Saleh katika Chama cha Congress, ambacho aliwahi kuhudumu kama makamu wa rais. Azimio hilo pia lilionya mtu yeyote ambaye ataunga mkono adui au kushiriki katika njama zake.

Yemen imeibuka katika nyanja ya kisiasa tangu mwanzoni mwa milenia mpya kama uwanja wa mzozo wa kimataifa, huku Amerika ikizidisha shinikizo na kuilenga kwa lengo la kuiweka chini ya ushawishi wake wa kisiasa, baada ya kuitenganisha na ushawishi wa kisiasa wa Uingereza, ili iwe mwenza wa Saudi Arabia, wakati wa enzi ya Salman bin Abdulaziz na mwanawe Mohammed, au kuisambaratisha ikiwa itathibitisha kuwa kichwa ngumu, ili isiwe tishio kwa Riyadh katika kanda hiyo.

Yemen na watu wake hawatafurahia amani na usalama chini ya shinikizo la mzozo wa kimataifa wa Marekani na Uingereza, ambao haujakoma kwa zaidi ya miongo sita, ukichukua sura na maumbo mbalimbali. Badala yake, watafurahia amani na usalama chini ya kivuli cha Khilafah Rashida ya pili kwa Njia ya Utume. Kwa hiyo, ni lazima waharakishe kufanya kazi na Hizb ut Tahrir ili kuisimamisha.

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.