Ijumaa, 06 Rabi' al-awwal 1447 | 2025/08/29
Saa hii ni: (M.M.T)
Menu
Main menu
Main menu

Ubwana Unaofifia: Mpango Mpya wa Mafuta wa Pakistan, Vita vya Kale na Sera ya AI

Mnamo Julai, Rais Trump wa Amerika alichapisha kwenye jukwaa lake la Ukweli wa Jamii. “Hivi punde tumemaliza mkataba na nchi ya Pakistan, ambapo Pakistan na Marekani zitafanya kazi pamoja katika kuendeleza hifadhi yao kubwa ya mafuta.” Mkataba wa mafuta ni sehemu ya mkataba mpana wa kibiashara kati ya nchi hizo mbili, ambapo Marekani imekubali kupunguza ushuru kwa bidhaa za Pakistan kutoka 29% hadi 19%, huku ikitishia kuweka ushuru wa adhabu kwa India, isipokuwa New Delhi imalize uagizaji mafuta ghafi kutoka Urusi.

Soma zaidi...

Waafghani Baina ya Nyundo ya Siasa za Pakistan na Kinoo cha Agenda ya Kikanda

Tangu mwaka wa 2023, serikali ya Pakistan imezidisha uhamishaji wa wakimbizi wa Afghanistan, hatua inayolenga kuishinikiza serikali ya mpito ya Afghanistan inayoongozwa na Taliban jijini Kabul kuwasilisha kikamilifu matakwa ya Amerika. Mawimbi ya Waafghani kuhamishwa kwenda Pakistan yana mizizi ya kihistoria tangu Jihad dhidi ya Muungano wa Kisovieti katika miaka ya 1980, vita vya wenyewe kwa wenyewe vilivyofuata, na uvamizi wa Marekani na kuikalia kijeshi Afghanistan kuanzia 2001 hadi 2021. Pakistan kihistoria imetoa kina cha kimkakati kwa Waislamu wa Afghanistan, shukran kwa mafungamano ya karibu ya kabila yanayovuka Mstari wa Durand.

Soma zaidi...

Musiiangushe Gaza, Enyi Waislamu

Ni masikitiko kwa usaliti! Maumivu yake yanaumiza moyo. Hakika, usaliti ni mchungu zaidi kwa nafsi kuliko maumivu ya njaa, kifungo, na mateso. Wananchi wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina wakiwemo watu wa Gaza wanautaka Umma wa Kiislamu kuwanusuru na kuwakomboa, kwa sababu udugu wa Kiislamu unawataka Waislamu kuwanusuru wanaodhulumiwa miongoni mwao.

Soma zaidi...

Vifungu vya Tovuti

Viunganishi

Magharibi

Ardhi za Waislamu

Ardhi za Waislamu