- |
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- ukubwa wa font punguza ukubwa wa font zidisha ukubwa wa font
بسم الله الرحمن الرحيم
Mpango wa Mosaic: Kubadilisha Chapa Mkakati Uliofeli na Jaribio Jipya la Kuidhibiti Taliban
(Imetafsiriwa)
Habari:
Baraza la Usalama la Umoja wa Mataifa hivi karibuni lilifanya kikao maalum kujadili hali ya Afghanistan. Katika mkutano huu, Roza Otunbayeva, mkuu wa Misheni ya Misaada ya Umoja wa Mataifa nchini Afghanistan (UNAMA), aliwasilisha mfumo mpya wa kina unaoitwa "Mpango wa Mosaic." Alisisitiza kuwa mpango huu haulengi "kusawazisha hali nchini Afghanistan," bali unalenga kuendeleza maslahi ya kweli ya watu wa Afghanistan.
Maoni:
Kuzinduliwa kwa mpango huo mpya kunajiri kutokana na kufeli kwa mpango wa awali wa Umoja wa Mataifa, ulioandaliwa na Feridun Sinirlioğlu. Juhudi hizo zilifikia mkwamo katika pande mbili muhimu: kwanza, kukosekana kwa maafikiano ya kimataifa kuhusu jinsi ya kukabiliana na Taliban; na pili, Taliban kumkataa Mjumbe Maalum aliyeteuliwa na Umoja wa Mataifa, ambaye alikuwa amepewa jukumu la kutekeleza mpango huo. Kwa kuzingatia vizuizi hivyo, Umoja wa Mataifa sasa umeanzisha mpango mpya chini ya kichwa “Mosaic.”
Ili kutekeleza mkakati wa awali, mikutano ya Doha ilikuwa imeitishwa, iliyodumu kwa raundi tatu. Hata hivyo, kama ilivyoelezwa tayari, mchakato huo ulikwama kutokana na changamoto zilizotajwa hapo juu. Sasa, mwaka mmoja baadaye, mchakato wa Doha umeanza tena. Mnamo 30 Juni na 1 Julai 2025, Qatar iliandaa mkutano wa tatu wa Kamati ya Kupambana na Dawa za Kulevya na mkutano wa pili wa kiufundi kati ya Taliban na wawakilishi wa kimataifa wa sekta ya kibinafsi. Haya yalifanyika kama sehemu ya awamu ya nne ya Mchakato wa Doha na ndani ya mfumo wa utekelezaji wa Mpango wa Mosaic.
Ingawa mkusanyiko wa hivi punde ulikuwa wa kiufundi kimaumbile, unatazamwa sana kama utangulizi wa mazungumzo ya kisiasa yajayo. Kulingana na taarifa ya 2 Mei 2025 ya Stéphane Smith, msemaji wa UNAMA, Mpango wa Mosaic umeundwa katika nguzo kuu mbili:
Kuanzishwa kwa makundi ya utendakazi kushughulikia changamoto za dharura zinazowakabili watu wa Afghanistan, kama vile juhudi za kukabiliana na dawa za kulevya na kuimarisha sekta ya kibinafsi;
Kushughulikia vikwazo vilivyoko vinavyozuia kurudi kwa Afghanistan katika jumuiya ya kimataifa, hasa kujitolea kwa haki za binadamu na kuheshimu sheria ya kimataifa.
Ingawa Mosaic inaletwa kama mpango mpya, kimsingi ni toleo lililosahihishwa upya la mpango wa awali. Malengo ya kimkakati bado hayajabadilika, ila mbinu tu za utekelezaji na ushiriki zinafanyiwa marekebisho. Kama Roza Otunbayeva alivyoeleza wakati wa kikao cha hivi karibuni cha Baraza la Usalama kuhusu Afghanistan:
"Ushirikiano na Afghanistan wenye madhumuni unalenga nchi ambayo ina amani yenyewe na majirani zake, ambayo inashikamana na majukumu yake ya kimataifa, na ambayo inajioanisha tena ndani ya jumuiya ya kimataifa – sio ambayo inasalia kunaswa ndani ya mizunguko inayojirudia rudia ya vurugu."
Kauli hii inaashiria kwa uwazi kwamba lengo kuu la mpango huo linabaki kuwa kujitenga kwa taratibu kwa Taliban kutoka kwa ruwaza yao ya Kiislamu, na hatimaye kuoanishwa kwao ndani ya mfumo wa kisekula wa ulimwengu.
Kipengele kinachobainisha cha Mpango wa Mosaic ni mkakati wake wa "hatua kwa hatua". Chini ya muundo huu, ikiwa Taliban itapiga hatua moja kuelekea jumuiya ya kimataifa, nchi za Magharibi zitajibu kwa hatua sawia. Sera hii imejengwa juu ya udhibiti wa taratibu na ushawishi unaodhibitiwa. Hata hivyo, Taliban hadi sasa wameshindwa kupendekeza mpango wazi na madhubuti wa kutabikisha utawala wa Kiislamu au mfumo kamili wa kisiasa wa Kiislamu. Ulimwengu wa Magharibi umepatiliza ombwe hili, kuwasongeza Taliban karibu na muundo wao wenyewe.
Kinyume chake, Hizb ut Tahrir, harakati ya kimfumo na kisiasa ya Kiislamu, inatoa ruwaza ya kina, halali, na ya kweli kwa ajili ya kusimamisha Khilafah Rashida—mradi unaoegemezwa kikamilifu katika kanuni za Kiislamu. Tofauti na mwelekeo ziada wa Magharibi, mpango huu sio hatua kwa hatua. Umeasisiwa kwa ajili ya Uislamu na kwa kanuni za Uislamu. Kwa mujibu wa mantiki ya Kiislamu, wakati mwengine nia ya dhati pekee inatosha kwa Mwenyezi Mungu Mtukufu kutoa mafanikio na kufungua njia. Wakati mwengine, ikiwa mja atajikurubisha hatua moja tu, Mwenyezi Mungu (swt) hujikurubisha kwake kwa hatua nyingi zaidi. Kama ilivyoelezwa katika Hadith tukufu (Hadith Qudsi):
«إِذَا تَقَرَّبَ العَبْدُ إِلَيَّ شِبْرًا، تَقَرَّبْتُ إِلَيْهِ ذِرَاعًا، وَإِذَا تَقَرَّبَ إِلَيَّ ذِرَاعًا، تَقَرَّبْتُ إِلَيْهِ بَاعًا، وَإِذَا أَتَانِي يَمْشِي، أَتَيْتُهُ هَرْوَلَةً»
“Pindi mja Wangu akijikurubisha kwangu kwa shubiri moja, mimi najikurubisha kwake kwa dhiraa moja; na pindi akijikurubisha kwangu kwa dhiraa moja, mimi najikurubisha kwake kwa yadi moja; na akinijia akitembea, mimi humjia mbio.” (Imepokewa na al-Bukhari na Muslim)
Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Yosuf Arsalan
Mwanachama wa Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir katika Wilayah Afghanistan