Logo
Chapisha ukurasa huu

بسم الله الرحمن الرحيم

Dola ya Kitaifa ndiyo Kikwazo Kikubwa Zaidi katika Kulinda Heshima na Maisha ya Waislamu Iwe nchini India au Gaza

(Imetafsiriwa)

Habari:

Waziri wa Mambo ya Nje na Naibu Waziri Mkuu Ishaq Dar alilaani vikali tukio ambapo Waziri Mkuu wa Bihar Nitish Kumar alivua hijabu ya mwanamke wa Kiislamu Nusrat Parveen katika hafla ya serikali, akilitaja kuwa ‘la kuchukiza sana’. Dar alielezea tukio hilo kama la aibu, akisema lilionyesha haja ya haraka ya kulinda haki za wachache na kupunguza wimbi linaloongezeka la chuki dhidi ya Uislamu. [Tribune]

Maoni:

Sio tukio la kwanza nchini India ambapo mwanamke Muislamu alinyanyaswa na kukosewa heshima. Tangu kuanzishwa kwa India mwaka wa 1947, watawala wa Kibaniani wa India hawajawahi kuthamini maisha, mali na heshima ya Waislamu wanaoishi chini ya mamlaka yao. Tangu mwaka wa 1950, kwa uchache Waislamu elfu kumi wamepoteza maisha yao katika ghasia za kijamii, mara nyingi zikitokea kwa idhini ya watawala wa Kibaniani, bila kujali walikuwa wa chama gani cha kisiasa. Katika ghasia za Gujrat za mwaka wa 2002, makundi ya Mabaniani yalibaka, kupora, na kuua katika kampeni ya vurugu iliyoendelea kwa zaidi ya miezi miwili. Wanawake walikatwa viungo, watoto walichomwa moto, na kina baba walikatwa vipande vipande. Takriban watu 1,000, wengi wao wakiwa Waislamu, waliuawa. Nyumba na biashara za Waislamu wapatao 20,000 na sehemu 360 za ibada ziliharibiwa, na takriban watu 150,000 walihamishwa makaazi yao. Mnamo 1992, makundi ya Mabaniani yalivunja Msikiti wa kihistoria wa Babari na mnamo Januari 2024, Muuaji wa Gujrat, ambaye sasa ni Waziri Mkuu wa India, alizindua ujenzi wa hekalu kwenye magofu ya Masjid Babri.

Kuwapiga na kuwaua wanaume Waislamu kwa tuhuma kwamba wamechinja ng'ombe imekuwa jambo la kawaida. Hata hivyo, sasa kuongezeka kwa ghasia dhidi ya Waislamu wa India kumefikia kilele kipya. Wanashambulia moja kwa moja heshima ya wanawake wa Kiislamu kwa kurarua abaya (vazi pana la nje) au khimar (mtandio).

Sehemu ya kusikitisha zaidi ya msimamo huu wa kivita wa dola ya Kibaniani ni kwamba wakati wowote tukio kama hilo linapotokea, watawala wa Pakistan, ambao wanamiliki majeshi yenye nguvu zaidi katika Ulimwengu wa Kiislamu, wenye silaha za nyuklia, wanalaani tu kitendo hicho na kuitaka ile inayoitwa jumuiya ya kimataifa kuiwajibisha dola ya Kibaniani. Hata hivyo, kamwe hawachukui jukumu la kuifundisha dola ya Kibaniani funzo kama hilo kiasi kwamba kamwe haisubutu kufanya hivyo tena.

Ni ipi sababu ya mwenendo wa aibu kama huo wa Pakistan? Je, haijui umuhimu wa kulinda heshima ya wanawake? Au haijioni kuwa na jukumu la kuzuia uchokozi kama huo, kwa kuwa inawajibika tu kuwalinda watu wanaoishi ndani ya mpaka wa Pakistan?

Katika Uislamu, heshima ya mwanamke lazima ilindwe kwa gharama yoyote. Wakati wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), mwanamke wa Kiislamu alitembelea soko la Banu Qaynuqa (kabila la Kiyahudi) mjini Madina. Sonara mmoja wa Kiyahudi akalifunga gauni lake mgongoni mwaka, likafunua miguu yake aliposimama, na kusababisha kicheko kutoka kwa wanaume wa Kiyahudi waliokuwepo. Mwanamke huyo alipiga kelele, akimvuta mwanamume mmoja wa Kiislamu ambaye alimuua sonara huyo kwa kulipiza kisasi. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) aliwazingira Banu Qaynuqa, akawalazimisha kujisalimisha na kuamuru wahamishwe kutoka Madina.

Mfano huo wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) uliweka kiwango cha ulinzi wa heshima ya wanawake. Kwa sababu ya kiwango hiki, gavana wa Umayyad Khalifa wa Iraq, Hajjaj ibn Yusuf, alimwamuru Muhammad ibn al-Qasim kuvamia Sindh na kuwaokoa wanawake Waislamu waliotekwa na maharamia wa Raja Dahir. Vita vilitokea mwaka wa 712 M, na kusababisha kushindwa na kifo cha Dahir, na ukombozi wa mateka.

Kulingana na kiwango kilichowekwa na Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), Khalifa wa Abbasiya Al Mu'tasim alituma jeshi kumkomboa mwanamke aliyemwita kumkomboa alipokamatwa na Warumi.

Dola ya sasa ya Pakistan haiegemei juu ya Aqida ya Kiislamu ambayo inawajibisha kulinda heshima ya mwanamke wa Kiislamu. Mara nyingi uongozi wa kisiasa na kijeshi wa Pakistan umesema kwamba majeshi ya Pakistan yanawalinda watu wanaoishi ndani ya Pakistan pekee. Hii ndiyo sababu kuu kwamba licha ya uhasama usio na mwisho dhidi ya Waislamu iwe katika Dola ya Kibaniani, katika Kashmir Inayokaliwa kwa mabavu au Palestina, watawala wa Pakistan hawahisi kulazimishwa kujibu kilio na miito yao ya msaada, uokozi na ukombozi.

Fahamu ya dola ya kitaifa inatuzuia kujifunga na kuitikia amri za Mwenyezi Mungu (swt) na Sunnah za Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kuhusiana na ulinzi wa wanawake wa Kiislamu. Kwa hivyo Waislamu wa Pakistan lazima wajiunge na mapambano ya Hizb ut Tahrir kwa ajili ya kusimamisha Khilafah, ambayo itaitikia wito wa wanawake Waislamu wanaokandamizwa nchini India na Kashmir Inayokaliwa kwa mabavu na kutimiza bishara njema ya Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) kuhusu Gazwa-e-Hind. Imesimuliwa na Thawban, mtumwa aliyeachiliwa huru wa Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw), kwamba Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema:

«عِصَابَتَانِ مِنْ أُمَّتِي أَحْرَزَهُمَا اللَّهُ مِنَ النَّارِ عِصَابَةٌ تَغْزُو الْهِنْدَ وَعِصَابَةٌ تَكُونُ مَعَ عِيسَى ابْنِ مَرْيَمَ عَلَيْهِمَا السَّلاَمُ»

“Kuna makundi mawili ya Umma wangu ambayo Mwenyezi Mungu atayawacha huru kutokana na Moto: kundi litakalopigana na India, na kundi litakalokuwa pamoja na ‘Isa bin Maryam, amani ya Mwenyezi Mungu iwe pamoja naye.”

Imeandikwa kwa Ajili ya Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir na
Shahzad Shaikh – Wilayah Pakistan

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.