Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  2 Muharram 1447 Na: H 1447 / 001
M.  Ijumaa, 27 Juni 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Trump na Netanyahu Wanajigamba na Kujisifu Huku Watawala Wetu Wakikaa Kimya Mithili ya Wafu Makaburini Mwao!
(Imetafsiriwa)

Vita kati ya Iran na umbile la Kiyahudi vimemalizika, na jinai za Mayahudi mjini Gaza hazikukoma wakati wa vita hivyo, wala hadi wakati huu. Marekani ilifanya ujanja wa kiusanii, ikidai kuwa imeangamiza uwezo wa nyuklia wa Iran. Hatua hii imekuja baada ya Waziri wa Mambo ya Nje wa Iran kukutana na wale wanaojiita mawaziri wa Troika wa Ulaya, ambao walikuwa sehemu ya mazungumzo ya nyuklia ya Iran kabla ya Marekani kujitoa katika mazungumzo hayo wakati wa muhula wa kwanza wa Trump. Iran pia ilifanya mbwembwe za kiusanii kwa kurusha makombora kadhaa katika Kambi ya Kimarekani ya Al Udeid nchini Qatar, baada ya kuifahamisha Marekani kuhusu hilo, kama Trump mwenyewe alivyosema.

Wakati wa matukio hayo, watawala wa Waislamu walitoa shutma na tuhma za mara kwa mara kwa umbile la Kiyahudi na Marekani inayokiuka ubwana wa Iran, na Iran kukiuka ubwana wa Qatar. Ilhali miongoni mwa watawala hao wamo wale walioruhusu ndege za kivita za Kiyahudi na Marekani kupita katika anga zao ili kuishambulia Iran, na wengine waliotungua makombora na droni za Iran zinazoelekea umbile la Mayahudi!

Baada ya matukio hayo, ambayo wachambuzi wa mambo waliyaeleza kuwa ni kama mchezo wa kuigiza, na ambayo yalikuwa wazi kwa watazamaji wengi, hata watu wa kawaida, Trump alipaza sauti yake akijigamba juu ya yale aliyoyatimiza kuhusiana na faili la nyuklia la Iran, akijigamba juu ya uwezo wake wa kusitisha vita kati ya umbile la Kiyahudi na Iran. Netanyahu alifuata, kwa kiburi akiogopa kuizuia Iran kupata silaha ya nyuklia na kujivunia ushindi wake juu yake.

Ama Iran, na nchi nyingine za Kiislamu, watawala wao hawaathiriwi na lolote kati ya haya. Wana wasiwasi na kitu chengine kabisa! Watawala wa Iran, ambao walipuuza kujitayarisha kwa vita na walionekana kushangazwa na mashambulizi ya umbile la Kiyahudi, licha ya kuongezeka kwa uhasama hapo awali na vitisho vya mara kwa mara vya kuishambulia Iran, hawakufanya maandalizi muhimu. Waliruhusu ndege za Kiyahudi kutawala anga ya Iran, wakifanya wapendavyo, kuua na kuharibu wapendavyo. Baada ya kila shambulizi, huwasha ulinzi wa anga. Ni maovu kiasi gani wanayoyafanya! Kisha wanakubali kusitisha vita ingawa wao ndio walioshambuliwa. Sasa, wakikabiliana na majigambo ya Trump na Netanyahu, hawasemi neno hata moja, wala hawaonyeshi azma hata kidogo ya kiume.

Ama watawala wengine wa nchi za Kiislamu, hali yao imesalia kutobadilika, inayoashiriwa na khiyana na kula njama dhidi ya watu wao, kuwaruhusu maadui wa Ummah na wa watu wao wenyewe kuzurura kwa uhuru katika ardhi zao, wakiua na kuharibu wapendavyo. Hapo awali walikuwa wameruhusu umbile la Kiyahudi kuharibu Gaza, kufanya mauaji ya halaiki, kuhamisha makaazi, na kuwaweka njaa watu. Zaidi wanachotoa ni shutma au laana. Mbora wao anataka kulipeleka suala hilo kwenye vyombo vya kimataifa ambavyo vyenyewe vinakula njama dhidi ya Waislamu. Matendo yao ni maovu yalioje!

Je, watawala hao hawana uanaume?! Je, hawana hisia zozote za ushujaa, fahari, au utu?! Je, hakuna chochote katika msamiati wao isipokuwa kushutumu na kulaani? Je, hakuna chochote katika msamiati wao kama: «لَا يُصَلِّيَنَّ أَحَدٌ الْعَصْرَ إِلَّا فِي بَنِي قُرَيْظَة» “Asiswali mtu Swala ya Alasiri ila kwa Bani Quraidha.”

Je, hakuna chochote katika msamiati wao kama: "Kutoka kwa Harun al-Rashid hadi kwa Nikephoros, mbwa wa Roma"? Je, hakuna chochote katika msamiati wao wa maana ya heshima ya al-Mu'tasim? Je, hakuna chochote katika msamiati wao cha ujasiri na ushujaa wa Salahuddin? Je, hakuna chochote katika msamiati wao kuhusu uamuzi wa Abdul Hamid?

Enyi Waislamu: Watawala wenu wamefichuliwa jinsi walivyo. Imedhihirika kwenu kwamba wanatumikia maslahi ya adui zenu, sio yenu. Wako tayari kukutoeni kafara kwa adui zenu ili kutunza viti vyao vibovu vya utawala, na wamefanya hivyo mara kwa mara. Gaza inasimama kama uthibitisho wa wazi zaidi. Na sasa Iran iko mbele ya macho yenu, ikitanguliwa na Somalia, Iraq, Yemen, Libya, na Syria. Kama msemo unavyosema: "Kamba bado ingali inavuta," kwa hivyo mutafanya nini? Je, mutakaa kimya kuwahusu hadi lini?

Ni wakati wa kufanya uamuzi wenu, kusema neno lenu, na kuwang'oa hawa watawala vibaraka. Fanyeni kazi na Hizb ut Tahrir, kiongozi mwenye ikhlasi na mkweli ambaye hatakudanganyeni, na ambaye anashikilia mradi wa mwamko halisi, ili mupate kuregesha hadhi na heshima yenu, murudi kama mabwana wa dunia, na kubeba mwenge wa uongofu kwa wanadamu wote.

Afisi Kuu ya Habari

ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.