Uacheni Umma Ufanye Uamuzi Wake, Enyi Watawala Waoga!
- Imepeperushwa katika Afisi Kuu ya Habari
- Kuwa wa kwanza kutoa maoni!
- |
Hatukushangazwa, wala Umma wa Kiislamu haukushangazwa na ukaribishaji wa watawala wasaliti wa Waislamu wa mpango wa rais wa Marekani Donald Trump wa kuipoteza Gaza, kwani wao wametuzoezesha sisi kuwa waoga, badala ya kula njama na wakoloni makafiri dhidi ya masuala yetu. Trump alikuwa amekutana na baadhi yao jijini New York kando ya mikutano ya Baraza Kuu la Umoja wa Mataifa, mnamo Jumanne tarehe 23/9/2025, na wakamsifu na kutangaza kumtegemea yeye kumaliza vita dhidi ya Gaza. Mara tu Trump alipotangaza mpango wake wa ukoloni, waliharakisha kuukaribisha. Wasingewezaje kuukaribisha, wakati hakuna hata mmoja wao aliyesubutu kufanya vyenginevyo, kwa kuwa wamepoteza ari na ushujaa wa wanaume.