Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake

H.  2 Jumada I 1447 Na: H 1447 / 021
M.  Ijumaa, 24 Oktoba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

“Vita vya Burqa” vya Wananchi Ni Mwangwi wa Kisasa wa Ukoloni wa Ulaya, Uliotumika Kupuuza Mauaji ya Halaiki mjini Gaza na Kumvua Mwanamke wa Kiislamu Kitambulisho Chake cha Kiislamu

(Imetafsiriwa)

Vita vya hivi karibuni vya watu wengi kutoka kwa vyama vya kidemokrasia na serikali za mrengo wa kulia vinavyotaka kupigwa marufuku kwa burqa sasa vinajumuisha Australia, Italia na Ureno. Mataifa haya ni sehemu ya kundi kubwa la nchi adui za Ulaya ambazo tayari zimepiga marufuku burqa. Ufaransa, Ubelgiji, Denmark, na Uswizi zinatekeleza marufuku ya kitaifa katika maeneo yote ya umma, huku Uholanzi na Ujerumani, zikiwa na marufuku ya sehemu inayolenga muktadha maalum kama vile shule au afisi za serikali. Nchini Uingereza, mjadala unalenga wafanyikazi, ambapo chama cha mrengo wa kulia cha Mageuzi cha Uingereza kinasema kwamba burqa kama hizo zinazuia uoanishwaji, mawasiliano, na usalama, zikiziita “nembo za mgawanyiko.”

“Vita hivi vya sasa vya Burqa” si jambo la kisasa, bali ni sura ya hivi karibuni katika historia ndefu ya uadui wa kisekula wa Magharibi dhidi ya Uislamu na Waislamu. Uadui huu wa kihistoria uliodumu kwa muda mrefu unatumiwa ili kuvuruga ukosefu wa usalama mkubwa wa kiuchumi unaohisiwa katika jamii za kisekula, unaosababishwa na mfumo uliofeli wa ubepari wa kimataifa.

Vyama vya mrengo wa kulia—kama vile ‘One Nation’ cha Pauline Hanson nchini Australia, Fratelli d'Italia cha Giorgia Meloni nchini Italia, na chama cha Chega cha André Ventura nchini Ureno—vinatumia burqa kama ishara ya kudhalilisha wanawake Waislamu, kuwaoanisha kwa nguvu, na kugeuza umakini wa umma kutoka kwa migogoro halisi ya kufeli kwa serikali.

Mjadala huu wa karne nyingi kuhusu vazi la Kiislamu la wanawake wa Kiislamu unaakisi ‘misheni ya hadhara’ ya kikoloni ya Ulaya na ‘Mgongano wa Hadhara,’ uliopangiliwa upya kwa hadhira ya karne ya 21 iliyoachwa na wasiwasi na hasira na mfumo wa kiuchumi wa kibepari ulioharibika na kufilisika. Ni mkakati uliopigiwa hesabu ili kuelekeza maumivu halisi ya kiuchumi katika vita vilivyotengenezwa dhidi ya Uislamu na Waislamu.

Ufemonalisti, ambapo wanasiasa hutumia lugha ya haki za wanawake kwa kejeli ili kuhalalisha sera za chuki dhidi ya Uislamu kama vile marufuku ya burqa, pia unarudi nyuma kwenye Uorientali wa enzi ya ukoloni, ambao ulionyesha ulimwengu wa Kiislamu na wanawake wa Kiislamu kama walio nyuma, wanaotishia na wanaohitaji kuokolewa.

Mapendekezo ya marufuku ya burqa nchini Italia na Australia yanawalenga wanawake Waislamu, ambao tayari ni waathiriwa wakuu wa mashambulizi ya chuki dhidi ya Uislamu.

Nchini Australia, data kutoka kwa Sajili ya Chuki dhidi ya Uislamu ya Australia (Islamophobia Register) (Ripoti ya kila Mwaka 2024) inaonyesha kwamba 75% ya mashambulizi ya chuki dhidi ya Uislamu yanawalenga wanawake na wasichana. Vile vile, ripoti ya Shirika la EU la Haki za Msingi (FRA) inasema kwamba 65% ya Waislamu nchini Italia wanakumbana na ubaguzi, huku wanawake Waislamu wakiwa walengwa zaidi.

Wakati huo huo, nchini Ureno, chuki dhidi ya Uislamu ni jambo linaloongezeka linalohusishwa moja kwa moja na chama cha mrengo wa kulia cha Chega, kinachoongozwa na André Ventura, ambaye anauita Uislamu kama tishio kwa kitambulisho cha Wareno na Wakristo wa “Magharibi”. Marufuku ya burqa katika nchi hizi ingeidhinisha kisheria ubaguzi ambao wanawake Waislamu tayari wanakabiliwa nao.

Zaidi ya hayo, unafiki wa vyama vya kisiasa vya mrengo wa kulia vinavyojigamba kuhusu mavazi ya Kiislamu huku serikali za Australia, Italia, na Ureno zikiongoza janga la vurugu za wanaume hauwezi kupuuzwa.

• Nchini Australia, mwanamke mmoja anauawa na mwenzi wake karibu kila wiki (Taasisi ya Uhalifu ya Australia, 2023-24).

• Nchini Italia, mwanamke mmoja huuawa kila baada ya siku tatu, na kufichua kiwango cha mgogoro wa aibu (Wizara ya Mambo ya Ndani ya Italia, 2024).

• Nchini Ureno, unyanyasaji wa majumbani ndio uhalifu unaoripotiwa zaidi, huku 85% ya waathiriwa wakiwa wanawake.

Kupuuza mgogoro huu huku wakishughulika na kipande cha kitambaa kunaonyesha unafiki wa wazi wa dola hizi zinazodai kuwalinda wanawake.

Marufuku hii ya burqa ni chaguo la makusudi la tabaka la kisiasa kupuuza wasiwasi halisi wa kibinadamu wa umma. Ingawa mamia ya maelfu ya watu wameandamana kuvuka Daraja la Bandari ya Sydney nchini Australia, katika viwanja vya umma (piazza) kote Italia, na katika mitaa ya Lisbon kupinga mauaji ya halaiki ya Waislamu mjini Gaza yanayofanywa na umbile haramu halifu la Kizayuni, wanasiasa badala yake wanatabanni vita vya kithaqafa vya ‘sisi dhidi yao’.

Shambulizi hili la moja kwa moja dhidi ya vazi la wanawake Waislamu, ambalo hutumia mbinu ya kunasibisha usalama ili kuibandika burqa kama tishio la kuwepo kwa usalama, kitambulisho cha kitaifa, na maadili ya kisekula, husababisha serikali kuhalalisha mradi wa kulazimisha wa uoanishaji kwa nguvu ambao unawataka wanawake Waislamu kuacha kitambulisho chao cha Kiislamu ili kuendana na vitambulisho vya kisekula, vya kitaifa.

Ni muhimu kama wanawake Waislamu, kwamba tuendelee kushikamana na imani zetu za Kiislamu. Tunapaswa kukumbuka ahadi kutoka kwa Muumba wetu Mwenyezi Mungu (swt) ya thawabu zinazowasubiri wale walio na subira na msimamo thabiti katika Dini yao wakati wa shida na matatizo. Mwenyezi Mungu (swt) asema,

[إِنَّ الَّذِينَ قَالُوا رَبُّنَا اللَّهُ ثُمَّ اسْتَقَامُوا فَلَا خَوْفٌ عَلَيْهِمْ وَلَا هُمْ يَحْزَنُونَ * أُوْلَئِكَ أَصْحَابُ الْجَنَّةِ خَالِدِينَ فِيهَا جَزَاء بِمَا كَانُوا يَعْمَلُونَ]

“Hakika walio sema: Mola wetu Mlezi ni Mwenyezi Mungu; kisha wakatengenea, hawatakuwa na khofu, wala hawatahuzunika. Hao ndio watu wa Peponi, watadumu humo, kuwa ni malipo kwa waliyo kuwa wakiyatenda.” [Al-Ahqaf: 13-14].

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Kitengo cha Wanawake
Address & Website
Al-Mazraa Sanduku la Posta. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: ws-cmo@hizb-ut-tahrir.info

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.