Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  14 Jumada I 1447 Na: H 1447 / 025
M.  Jumatano, 05 Novemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Dharau ya Amerika kwa Raia Wake Yenyewe Yawaacha Wanawake na Watoto na Njaa

(Imetafsiriwa)

SNAP (Programu ya Usaidizi wa Lishe ya Ziada) ni mpango wa shirikisho unaowasaidia watu binafsi, familia, na wale wenye ulemavu kupata manufaa ya kielektroniki ambayo hutumika kwa chakula, vinywaji visivyo na kileo, na mimea kukuza chakula chao wenyewe. Inaripotiwa kuwa kuna Wamarekani milioni 42 ambao hutegemea manufaa ya SNAP kujilisha wao wenyewe na familia zao. 54% ya watu wazima wanaopokea manufaa ya chakula ni wanawake, hasa kina mama wasio na waume, na 39% ni watoto, ambayo ina maana kwamba takriban mtoto 1 kati ya 5 hutegemea manufaa haya ili kuhakikisha hawalali njaa. Kufungwa kwa shirikisho pia kumesababisha baadhi ya majimbo kulazimika kutafuta njia zengine za kufadhili programu za chakula cha mchana bila malipo na zilizopunguzwa za wilaya zao za shule, kwa hivyo watoto wanaotegemea kulishwa wakati wa siku ya shule hawalazimiki kuishi bila chakula. Matokeo yake, maduka mengi ya chakula yaliyoanzishwa kote nchini yanasambaza picha za rafu tupu na kuwaomba watu watoe kadi za zawadi za chakula na maduka ya mboga ili kukidhi mahitaji yanayoongezeka ya chakula.

Tunapaswa kujiuliza inawezekanaje kwamba serikali ya nchi tajiri zaidi duniani inapuuza ukweli kwamba mamilioni ya raia wake walio katika mazingira magumu zaidi hawatakuwa na chakula cha kutosha? Unaweza kuuliza serikali ya Marekani inatumia pesa wapi, hata wakati wa marufuku ya matembezi? Badala ya kuhakikisha Wamarekani wana chakula cha kutosha mezani mwao, wanatuma mabilioni ya dolari kwa umbile la Kiyahudi ili kuwaua Wapalestina. Ni mtawala anayeona ni muhimu zaidi kujenga ukumbi mkubwa wa michezo na wawakilishi wengine ambao wanaona uwekezaji wao binafsi unapewa kipaumbele kuliko ustawi wa watu wanaopaswa kuwawakilisha. Unaona, serikali ya kibepari ya Amerika haikuwahi kuwa katika biashara ya kushughulikia mambo ya raia wake, kwa njia ambayo wanaweza kutoa msaada wa kijeshi na kifedha kwa wale wanaowanyima watoto kote ulimwenguni haki ya usalama, chakula, malazi, na elimu – mahitaji msingi. Kwa hivyo, pia inawaacha watoto Amerika, wakiwa hawana usalama, wenye njaa, na bila elimu na huduma sahihi za kimatibabu.

Dunia, hata wale wanaoishi katika nchi tajiri zaidi, wanahitaji sana mabadiliko katika mfumo wa kisiasa. Mfumo wa kisiasa ambao hautawaacha raia wake wafe njaa huku watawala wakiangalia akaunti zao za kibinafsi za benki zikiongezeka. Mfumo wa kisiasa ambao kiongozi wake, kama Khalifa Umar Ibn al Khattab (ra), atasafiri katika nchi mbalimbali ili kuhakikisha kwamba kila mtoto anaweza kula hata kabla ya kujilisha mwenyewe. Mfumo wa kisiasa ambao utategemea kile ambacho Muumba wa Mola wa Walimwengu amekiteremsha ili kusimamia mambo ya watu. Kuna mfumo mmoja tu wa kisiasa unaoweza kukamilisha mambo hayo na mengineyo – Khilafah ya Kiislamu.

Kitengo cha Wanawake
katika Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.