Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari

H.  30 Jumada I 1447 Na: H 1447 / 030
M.  Ijumaa, 21 Novemba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari

Waislamu Maskini Wanastahili Zaidi Uwekezaji wa Watawala Wapumbavu Kuliko Amerika

(Imetafsiriwa)

Mfalme Mtarajiwa wa Saudi Arabia alifanya ziara nchini Marekani mnamo Jumanne, 18/11/2025, ambapo alionyesha kiwango cha upumbavu wake katika kufuja utajiri wa Ummah, kiwango cha utiifu wake kwa bwana wake Amerika, pamoja na kiwango cha usaliti wake kwa Ummah wa Kiislamu, njama yake dhidi yake, na vita vyake dhidi ya Mwenyezi Mungu (swt) na Mtume Wake (saw) kwa kukubali kujiunga na Makubaliano ya Abraham, yaliyowekwa katika usaliti mwingine ambao unahakikisha njia iliyo wazi ya suluhisho la dola mbili.

Kwa mujibu wa taarifa iliyotolewa na Ikulu ya Marekani, Rais wa Marekani Trump na Bin Salman walifikia mfululizo wa makubaliano ambayo yanaimarisha ushirikiano wa kimkakati kati ya nchi zao mbili, kuongeza fursa za kazi zenye mishahara mikubwa, kuimarisha silsila muhimu za usambazaji, na kuunga mkono utulivu wa kikanda. Taarifa hiyo ilithibitisha kwamba Amerika itakuwa mshirika wa Saudi Arabia katika ushirikiano wa nyuklia wa kiraia, ikibainisha kwamba nchi hizo mbili zilitia saini makubaliano ya mfumo wa kuimarisha ushirikiano katika madini adimu na kuratibu mikakati ya kitaifa ya kupanua silsila za usambazaji wa madini haya. Mbali na makubaliano ya pamoja ya ulinzi na makubaliano ya Saudi Arabia ya kununua ndege aina ya F-35, vifaru 300, na kuongeza uwekezaji wake nchini Marekani kutoka dolari bilioni 600 hadi trilioni moja.

Ni wazi kwamba Trump anauona Ufalme wa Al Saud kama chanzo cha kukusanya kiasi kikubwa cha pesa, na chombo cha kutekeleza sera za kigeni za Amerika. Tangu kuanzishwa kwa umbile la Kiyahudi, utawala wa Al Saud haujafyatua risasi hata moja, kwa hivyo wananunua silaha hizi kwa ajili ya nani ikiwa hawazitumii dhidi ya maadui wa Ummah?! Je, si kwa ajili ya kuwaua Waislamu, na je, vita vya Yemen si mfano hai?! Na kwa nini wanawekeza mabilioni ya dolari kufufua uchumi unaoporomoka wa Amerika, wakijua kwamba mamilioni ya Waislamu katika ufalme wao na ardhi zengine za Waislamu wanakufa njaa?! Na hii si mara ya kwanza kupoteza pesa za Waislamu kusaidia uchumi wa Amerika, au kuzifuja kwenye makasri yao na matamanio yao, au kwenye miradi ambayo haileti faida yoyote kwa Ummah.

Hakika, watawala wa Al Saud ni wapumbavu, kama watawala wengine wa Waislamu; Wanafuja utajiri katika kile ambacho hakiwanufaishi Ummah, na utajiri huu si wao wala wa baba zao, lakini ni haki ya Ummah. Mtume wa Mwenyezi Mungu (saw) amesema: «النَّاسُ شُرَكَاءُ فِي ثَلَاثٍ: فِي الْمَاءِ وَالْكَلَأِ وَالنَّارِ»  “Watu ni washirika katika vitu vitatu: maji, malisho na moto.” (Sunan Ibn Majah 2472)

Kwa hivyo mafuta, gesi, madini, bahari, na mito ni mali ya umma, na asili yake ni kwamba dola inayasimamia kwa uangalifu na kuwawezesha watu kupata haki yao kutoka kwayo. Na kama serikali katika ardhi za Waislamu zingefanya hivyo, hakuna maskini hata mmoja angebaki ndani yake. Lakini watawala wapumbavu huwanyima watu haki zao, huzifuja kwa matamanio yao, na kuwawezesha mabwana zao kutoka kwa maadui wa Ummah kuzikamata.

Enyi Waislamu: Kitendo hiki kinafanywa na wapumbavu pekee, na hukmu kuhusu wapumbavu ni kwamba lazima wazuiliwe, kwa hivyo fanyeni haraka kuwazuia watawala wenu na kuwazuia kutumia mali yenu. Amkeni mfanyeni kazi pamoja na Hizb ut Tahrir ili kusimamisha Khilafah, ili mumridhishe Mola wenu Mlezi kwa kusimamisha Shariah Yake duniani na kubeba Dini Yake kwa watu wote, na ili mrudishe mali yenu ambayo watawala hao Ruwaibidha (watepetevu na duni) wanaifuja, na hivyo muwe na furaha katika maisha haya na Akhera.

Afisi Kuu ya Habari
ya Hizb ut Tahrir

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Afisi Kuu ya Habari
Address & Website
Al-Mazraa P.O. Box. 14-5010 Beirut- Lebanon
Tel: 00961 1 30 75 94 Mobile: 00961 71 72 40 43
www.hizb-ut-tahrir.info
Fax: Telefax
E-Mail: media (at) hizb-ut-tahrir.info

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.