Logo
Chapisha ukurasa huu

Afisi ya Habari
Amerika

H.  7 Jumada I 1447 Na: 05 / 1447 H
M.  Jumatano, 29 Oktoba 2025

Taarifa kwa Vyombo vya Habari
Himaya Yashambulia Gaza - Sami Hamdi na Kifo cha Upinzani

(Imetafsiriwa)

Baada ya umbile la Kizayuni kuifahamisha Marekani kuhusu uamuzi wake wa kuanza tena operesheni zake za uhalifu mjini Gaza, zaidi ya wakaazi 109 wa Ardhi Iliyobarikiwa ya Palestina - wakiwemo watoto 46 - waliuawa shahidi, na wengine wengi walijeruhiwa tangu Jumanne jioni, 28 Oktoba 2025, katika mashambulizi ya anga yaliyofanywa kote Ukanda wa Gaza. Mabomu hayo yalilenga nyumba za raia na shule inayowahifadhi watu waliokimbia makaazi yao huko Beit Lahia, kaskazini mwa Gaza.

Kufuatia wimbi la hivi karibuni la mashambulizi ya umbile hilo la Kizayuni, Makamu wa Rais wa Marekani J.D. Vance alisema mnamo Jumanne, “Trump alifanikiwa kupata amani ya kihistoria katika Mashariki ya Kati, lakini hiyo haimaanishi kwamba hakutakuwa na mapigano madogo madogo hapa na pale.” Taarifa kama hizo zinaonyesha dharau kali ya utawala wa Marekani kwa damu ya Waislamu, ikiona mauaji ya watoto 46 wasio na hatia kama kitu kidogo – “mapigano madogo” tu - huku ikichukulia kuchelewesha kuregesha miili ya mateka kama uhalifu usiosameheka unaohalalisha mauaji zaidi. Kulingana na Wizara ya Afya ya Gaza, jumla ya mashahidi katika Ukanda wa Gaza sasa imeongezeka hadi 68,643, wengi wao wakiwa wanawake na watoto, tangu mwanzo wa uvamizi mnamo 7 Oktoba 2023.

Undumakuwili wa utawala wa Marekani na unafiki wa wazi vimezidi kuwa visivyovumilika. Udanganyifu, ahadi zilizovunjwa, na upendeleo vimekuwa alama za mkakati wake wa kisiasa. Huku Amerika inasalia kuwa msaidizi mkuu na mratibu halisi wa mauaji huko Gaza katika kipindi cha miaka miwili iliyopita, bila aibu ilijitokeza katika Mkutano wa Sharm el-Sheikh wa “Amani” kama “mpatanishi asiyeegemea upande wowote,” “mtengenezaji wa amani,” na “mdhamini wa amani”!

Ilitarajiwa – kwa hakika, karibu na yakini – kwamba Amerika na kambi yake ya kijeshi mlinzi na mtetezi, umbile la Kizayuni, ilikuwa ikishawishi upinzani kupitia kusainiwa kwa makubaliano ya Sharm el-Sheikh ya kukabidhi mateka na mabaki ya wafu, lakini iliasi makubaliano hayo na kuanza tena kuwaua wasio na hatia. Hii haishangazi kutoka kwa watunga sera wa Amerika, ambao hawajawahi kuheshimu agano au makubaliano na upande wowote wa kimataifa – achilia mbali inapotenda kama wadhamini wa umbile ambalo uozo wa maadili yake ni mbaya zaidi kuliko ule wa bwana wake Amerika.

Kama alivyosema Mwenyezi Mungu Mtukufu:

[أَوَكُلَّمَا عَاهَدُوا عَهْدًا نَبَذَهُ فَرِيقٌ مِّنْهُمْ بَلْ أَكْثَرُهُمْ لَا يُؤْمِنُونَ]

Je! Ati ndio kila wanapo funga ahadi huwapo kikundi miongoni mwao kikaivunja? Bali wengi wao hawaamini.” [Al-Baqarah: 100].

Idhini iliyotolewa na utawala wa Marekani kwa umbile la Kizayuni kutekeleza mauaji zaidi katika Ardhi Iliyobarikiwa pia inawakilisha mashtaka dhidi ya viongozi na marais waliohudhuria na kushuhudia Mkataba wa Sharm el-Sheikh – wa kwanza miongoni mwao viongozi wa ulimwengu wa Kiislamu, Misri, Pakistan, Uturuki, Indonesia, na wengineo.

Kimya chao mbele ya mauaji haya, kama ilivyokuwa kwa wale waliowatangulia, si kitu chengine ila ni ushirika na usaliti mpya. Uwepo wao katika mkutano wa Sharm el-Sheikh ulikuwa ule wa mashahidi wa uongo kwa makubaliano ambayo hayakuhakikishwa na bwana wao Trump wala na vibaraka wenyewe.

Utawala wa Marekani, chini ya utawala wa “Mfalme” Trump, unatafuta kuthibitisha tena mkakati wake wa udhibiti wa kimataifa, ukimwonyesha “Mfalme” kama yule anayeamuru Palestina na watu wake, na kwa wote wanaowahurumia wasio na hatia huko, sera ya ukandamizaji kupitia mauaji au mateso. Mojawapo ya madhihirisho haya ilikuwa kukamatwa na kufungwa kwa mwanaharakati na mwandishi wa habari Sami Hamdi wakati wa ziara yake ya kuzungumza nchini Amerika baada ya kuelezea uhalifu wa uvamizi huko Gaza kama mauaji ya halaiki.

Kukamatwa kwa Hamdi si tukio la pekee bali ni taswira ya kutisha ya mmomonyoko mpana wa vima na maadili kuelekea kwenye ubabe. Vitisho, kunyamazishwa na kuharamishwa kwa waandishi wa habari, wanaharakati, wasomi na makundi ya Kiislamu yanayokosoa sera za kigeni za Marekani kunafichua unafiki wa “utawala wa sheria” na “nchi ya watu huru”.

Kwa hili, utawala wa Marekani haujapanua tu rekodi yake ilojaa damu ya kuongoza na kuunga mkono mauaji mjini Gaza lakini pia umesaliti kanuni ambayo unadai kusimama juu yake – “uhuru wa kujieleza”, ambao hapo awali ulizingatiwa kuwa mtakatifu nchini Amerika. Je, akili zenye busara miongoni mwa wanafikra, wasomi, na wanaharakati wa Marekani zitaamka kabla hazijachelewa kuiokoa nchi yao kutoka kwa viongozi ambao wameupinga ulimwengu mzima na kukanyaga kila kima cha kibinadamu na akhlaki chini ya kiatu chake cha kibeberu?!

Afisi ya Habari ya Hizb ut Tahrir Amerika

Hizb-ut Tahrir: Afisi ya Habari
Amerika
Address & Website
Tel: 

Template Design © Joomla Templates | GavickPro. All rights reserved.